Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Nimekusoma vizuri mtaalam wangu
 
Priority ni Kibaha
 
Labda mleta mada kapewa kaambiwa achague kiwanja kimoja kati ya hizo sehemu

Ova
Swadakta... hii ndo itakuwa comment bora ya muda wote katika uzi huu

Ebu chukua 5 πŸ€œπŸ€›
 
Maisha popote kokote unaweza ukaishi tu ni wewe tu umejipangaje

Ova
Mkuu ina maana ukijipanga vizuri unaweza kuishi mburahati, tandale au kigogo katikati ya waswahili bila shida yoyote?
 
Asante sana kwa mada hii bila shaka itanipa mwanga,
Maana niko njia panda kwamba kati ya
Kongowe,
Chanika
Au Kibaha wapi ninunue kiwanja cha kuja kuweka makaazi.
 
Inamaana wewe Kibaha imekukalia kushoto mkuu, au unamaanisha huko kuna hadhi kubwa hivyo sikutakiwa kupataja katika list hii?
 
Kwanini mkuu kwani hujui Kwa Sasa CHANIKA ni chaguo namba 1 Kwa wajenzi kwine huko mbwembwe tu
Ok mkuu, hapa naona kila muwamba ngoma anavutia upande wake. Kuna mmoja amesema Vikindu ndo mpango mzima, kwengine kote michosho tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ha ha ha nami nilielewa Mkuu tuko pamoja. Miaka kadhaa ijayo Kibaha itakuwa sehemu ya DarπŸ˜…
Wengi tunatarajia hilo kutokea ili angalau mkoa upanuke kama mikoa mingine πŸ˜πŸ˜‚
 
Hicho Kiwanja anakupa nani-bure zama hizi? 'ncheke mie, amka unaota 'blaza' πŸ˜€

Changa Pesa yako nunua na jenga pale Roho yako itapopachagua.
Kusikiliza ya walimwengu hakuna ambapo hapatakosolewa.

Sijui naeleweka?
 
Mkuu nashukur sana tena sana kwa ushauri wako wenye kuelimisha na kutia moyo.

Kama ulivyosema, ni kweli mimi binafsi lengo langu limetimia kutokana na michango mbali mbali niliyokutana nayo humu. Lakini nimegundua kwamba kuna watu wengine nao walikuwa na mawazo kama yangu, lakini walikuwa wanashindwa kujua ni wapi wanapoweza kwenda kupata ushauri kuhusu sehem sahihi ya wao kununua kiwanja na kujenga kwa ajili ya makazi ya familia.

Hivyo tunapita pita humu kujifunza mengi zaidi kuhusiana na fursa mbali mbali za maeneo hayo.

Kutokana na michango niliyosoma humu, nafikiri Vikindu pia ni sehemu nzuri ukilinganisha na Chanika ambapo watu wanasema kuwa ni mbagala "B".
 
Ukiangalia kwenye taarifa nzima ya habari chanika ndio mahali hapajaripoti mafuriko ukilinganisha na maeneo mengine yes kuna baadhi ya maeneo machache sana yalipata maji e.g jirani na Nermat hotel
Naam...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…