Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kwanini?

Sehemu zinazopimwa kwa futi hata siyo pa maana.

Eneo la mita 20 kwa mita 20 mnajikuta mpo watu wawili.

Kiwanja kimoja kinapimwa futi 50 kwa 40 maana yake ni mita 12 kwa 17 chenye mita za mraba 204 wakati cha mita 20 kwa mita 20 kina ukubwa mita za mraba 400.

Hali kama hiyo ipo eneo lote la Wilaya ya Temeke (Mbagala ikiwemo), Homboza, Mkuranga-Vikindu, Kisemvule, na mikoa ya Kusini.

Kinachokuja hapo ni uswazi na vijumba vichafu.

Waswahili hawana utamaduni wa kujenga vyoo bora kwa hiyo hata ukijenga chako kizuri bado mtaa utakuwa mchafu na wewe utakuwa mchafu tu.
Nimekusoma vizuri mtaalam wangu
 
NiFirstaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Priority ni Kibaha
 
Maisha popote kokote unaweza ukaishi tu ni wewe tu umejipangaje

Ova
Mkuu ina maana ukijipanga vizuri unaweza kuishi mburahati, tandale au kigogo katikati ya waswahili bila shida yoyote?
 
Asante sana kwa mada hii bila shaka itanipa mwanga,
Maana niko njia panda kwamba kati ya
Kongowe,
Chanika
Au Kibaha wapi ninunue kiwanja cha kuja kuweka makaazi.
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini
 
Nafikiri ulitakiwa kutaja Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe na Mkuranga kwa sababu kwa sasa miji inakuwa kuelekea huko japo ukuwaji ndio unatofautiana, binafsi siyo tu kupewa bure bali hata ungeniambia nitoe hela kununua kiwanja kati ya hizo wilaya nilizokutajia, bila kupepesa macho ningechagua Bagamoyo hata kama cha Huko ndio kingekuwa na bei kubwa kuliko hizo sehemu nyingine
Inamaana wewe Kibaha imekukalia kushoto mkuu, au unamaanisha huko kuna hadhi kubwa hivyo sikutakiwa kupataja katika list hii?
 
Kwanini mkuu kwani hujui Kwa Sasa CHANIKA ni chaguo namba 1 Kwa wajenzi kwine huko mbwembwe tu
Ok mkuu, hapa naona kila muwamba ngoma anavutia upande wake. Kuna mmoja amesema Vikindu ndo mpango mzima, kwengine kote michosho tu 😂😂😂
 
Ha ha ha nami nilielewa Mkuu tuko pamoja. Miaka kadhaa ijayo Kibaha itakuwa sehemu ya Dar😅
Wengi tunatarajia hilo kutokea ili angalau mkoa upanuke kama mikoa mingine 😍😂
 
Hicho Kiwanja anakupa nani-bure zama hizi? 'ncheke mie, amka unaota 'blaza' 😀

Changa Pesa yako nunua na jenga pale Roho yako itapopachagua.
Kusikiliza ya walimwengu hakuna ambapo hapatakosolewa.

Sijui naeleweka?
 
Kama ulivyosema kuwa kila mwamba ngoma ngozi huvilutia kwake. Wengi wapendekaeza tu eneo bia kutoa sababu za msingi.
Ila mkuu kuchagua mahali au eneo kunatokana na hitaji au lengo kuu. Mimi naamini katika michango ya watu hapa nadhani kuna iliyogusa lengo lako.
Yuko mmoja ambaye nadhani amechanganua kila maeneo bila upendeleo akielezea uzuri na ubaya wa kila eneo. Huyu amemaliza kila kitu. Kazi kwako.
Sasa katika malengo yako angalia wapi panafaa kutokana na ufafanuzi alioeleza.
Kila la heri. Ila karibu Vikindu, hutajuta.
Mkuu nashukur sana tena sana kwa ushauri wako wenye kuelimisha na kutia moyo.

Kama ulivyosema, ni kweli mimi binafsi lengo langu limetimia kutokana na michango mbali mbali niliyokutana nayo humu. Lakini nimegundua kwamba kuna watu wengine nao walikuwa na mawazo kama yangu, lakini walikuwa wanashindwa kujua ni wapi wanapoweza kwenda kupata ushauri kuhusu sehem sahihi ya wao kununua kiwanja na kujenga kwa ajili ya makazi ya familia.

Hivyo tunapita pita humu kujifunza mengi zaidi kuhusiana na fursa mbali mbali za maeneo hayo.

Kutokana na michango niliyosoma humu, nafikiri Vikindu pia ni sehemu nzuri ukilinganisha na Chanika ambapo watu wanasema kuwa ni mbagala "B".
 
Ukiangalia kwenye taarifa nzima ya habari chanika ndio mahali hapajaripoti mafuriko ukilinganisha na maeneo mengine yes kuna baadhi ya maeneo machache sana yalipata maji e.g jirani na Nermat hotel
Naam...
 
Back
Top Bottom