Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Nitachagua kibaha sababu ni mji unakua kuna nafasi naweza kufanya maendeleo mengine kama kufuga ni rahisi kupata masoko upande wa kibamba na chalinze maana kibaha ipo hapo kati.
Vikindu nafasi ipo ila ukuaji wake sio kama kibaha, chanika mmh huko pashakua uswazi na bagamoyo bado hapajaendelea kivilee.
 
Wengi wanaosapoti Kibaha wanapaangalia pale Maili Moja, Kwa Mfipa, Kwa Mathias hadi Kongowe tena barabarani. Hivi mmewahi kuingia huko ndani ndani kwenye viwanja vinakouzwa? Ni uzaramoni haswaaaaa, ni uswahili sana.

As for Bagamoyo, ule mji mimi hapana. Haujawahi kunivutia.
Labda maeneo kama Zinga huku nyuma kabla hujafika Bagamoyo kwenyewe. Bagamoyo ni mji usioendelea kwa miaka mingi.

Chanika, sehemu nzuri mwisho pale Taliani. Huko mbele sijui Zingiziwa, kwa Mpango sjui wapi huko ni mateso tu. Na uswahilini sana.

Vikindu, ubaya wa Vikindu ina jamii mchanganyiko lakini wamekaa vikundi vikundi. Unaweza kwenda sehemu wamejaa Wapare watupu mtaa mzima viwanja vyote wanamiliki wao. Kuna sehemu unaenda wamejaa Wamakonde watupu, ipo sehemu ina Wandengereko tupu. Hawa wengi ni zao la machinga wa Mbagala na waliouza nyumba za urithi au zao wenyewe Tandika na Mbagala/Magomeni wamekimbilia huko.

Ceteris Paribus, Kibaha is promising. Ile barabara kutoka pale Maili Moja wanataka iwe njia 4 hadi Chalinze so kutakuwa magoli sana. Maroli hayatakuja mjini kwa sababu Kwala wanajenga bandari kavu.

Kumbuka mkoa wa Pwani ndio mkoa pekee Tz usiokuwa na Manispaa.
 
Kwa sehemu iliyochangamka kama Chanika na ilivyokuwa maarufu mpaka leo kuwa na kiwanja cha 1.7 mill huko ni sawa na kutoa bure.

Tungetegemea huko viwanja visipungue 8mill hadi tunavyoongea hapa
Me kuna wadau wako huko kiwanja mpak 20mil vipo mpka 100mil hii ni barabarani

Bei ya kiwanja inategemea. Kiwanja chenyewe kiko katika mazingira gani.
 
Nenda Chanika mkuu imekuwa sana na mahitaji sio tatizo
 
Well done mkuu
 
Ok brother acha ushauri wako niufanyie kazi.
 
Hakuna afadhali hata sehemu moja...

Wanaotaja Kibaha wanaitazama Maili moja tu labda, lakini Kibaha ni kubwa na ndani ndani kuna mambo ya kiduanzi na ushirikina kama ilivyo Bagamoyo na Vikindu, na palipo na ushirikina sahau maendeleo...
Mbona watu wanadai sehemu kubwa ya Kibaha kwa sasa imejengeka, uswahili umepungua maana wale waswahili wenyewe original wengi wameshakufa, na wengine wameuza maeneo yao au viwanja vyao na kuwaachia wageni mji.

Sasa nashangaa wewe unapapinga mkuu!
 
Ni bora pale chanika,baada ya wiki mbili nitakua nishakitia sokoni nirudi kupanga mjini😎
Kwani hata maeneo mengine si unaweza kukitia sokoni tena kwa bei kubwa zaidi ya Chanika au kwako wewe unaona Chanika kunauzika zaidi ya maeneo mengine?
 
Bagamoyo
 
Ok boss, naona Kibaha inazidi kuibuka kidedea katika mjadala wetu, sio kama Chanika na Vikindu yake.
 
We kaka una akili sana nyingi Wacha niku follow
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…