Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Wengi wanaosapoti Kibaha wanapaangalia pale Maili Moja, Kwa Mfipa, Kwa Mathias hadi Kongowe tena barabarani. Hivi mmewahi kuingia huko ndani ndani kwenye viwanja vinakouzwa? Ni uzaramoni haswaaaaa, ni uswahili sana.

As for Bagamoyo, ule mji mimi hapana. Haujawahi kunivutia.
Labda maeneo kama Zinga huku nyuma kabla hujafika Bagamoyo kwenyewe. Bagamoyo ni mji usioendelea kwa miaka mingi.

Chanika, sehemu nzuri mwisho pale Taliani. Huko mbele sijui Zingiziwa, kwa Mpango sjui wapi huko ni mateso tu. Na uswahilini sana.

Vikindu, ubaya wa Vikindu ina jamii mchanganyiko lakini wamekaa vikundi vikundi. Unaweza kwenda sehemu wamejaa Wapare watupu mtaa mzima viwanja vyote wanamiliki wao. Kuna sehemu unaenda wamejaa Wamakonde watupu, ipo sehemu ina Wandengereko tupu. Hawa wengi ni zao la machinga wa Mbagala na waliouza nyumba za urithi au zao wenyewe Tandika na Mbagala/Magomeni wamekimbilia huko.

Ceteris Paribus, Kibaha is promising. Ile barabara kutoka pale Maili Moja wanataka iwe njia 4 hadi Chalinze so kutakuwa magoli sana. Maroli hayatakuja mjini kwa sababu Kwala wanajenga bandari kavu.

Kumbuka mkoa wa Pwani ndio mkoa pekee Tz usiokuwa na Manispaa.
Asante boss kwa uchambuzi murua kabisa. Kifupi nafikiri unamaanisha kuwa Kibaha ni bora kiasi kuliko maeneo mengine tajwa hapo juu.
 
Me kuna wadau wako huko kiwanja mpak 20mil vipo mpka 100mil hii ni barabarani

Bei ya kiwanja inategemea. Kiwanja chenyewe kiko katika mazingira gani.
Du Chanika hii hii bei ya kiwanja Mil 100 mkuu 😳😳
 
Mbona watu wanadai sehemu kubwa ya Kibaha kwa sasa imejengeka, uswahili umepungua maana wale waswahili wenyewe original wengi wameshakufa, na wengine wameuza maeneo yao au viwanja vyao na kuwaachia wageni mji.

Sasa nashangaa wewe unapapinga mkuu!

Wanaokwambia hivyo wauliza Kibaha ipi, wakikutajia Maili moja basi sawa, kinyume na hapo Kibaha ni kubwa sana na bado ni ile ile...
 
Soma alama za nyakati, katika mkoa wa Pwani, Kibaha ndio kuna muelekeo zaidi. Future iko huko.
Naiona bomoabomoa kibaha Miaka 25 ijayo.

Sabb mji ule unatawaliwa na matamanio ya kuishi watu wengi.

Hapa nielewe wewe huwez kuitunishia pesa. Watawaondoa tu. Watasongizia factory zone na madudekibao.

Vikindu na Bagamoyo inategemea na City master plan.
 
Nakushauri njoo Bagamoyo haraka sana.

Mji unakua kwa kasi viwanda vinajengwa kwa wingi.

kuna usafiri wa uhakika usiosumbua wa kuingia na kutoka Dar pia ni njia ya karibu ya kuelekea mikoa ya kaskazini.

Bila kusahau kuna fursa ya bandari ya Bagamoyo inayotarajiwa kuanza kujengwa mwaka huu mwezi wa 6 au 8.

Wanaojua kuzinusa fursa wanahamia kwa kasi sana Bagamoyo.

Karibu Bagamoyo hujachelewa.
 
Wengi wanaosapoti Kibaha wanapaangalia pale Maili Moja, Kwa Mfipa, Kwa Mathias hadi Kongowe tena barabarani. Hivi mmewahi kuingia huko ndani ndani kwenye viwanja vinakouzwa? Ni uzaramoni haswaaaaa, ni uswahili sana.

As for Bagamoyo, ule mji mimi hapana. Haujawahi kunivutia.
Labda maeneo kama Zinga huku nyuma kabla hujafika Bagamoyo kwenyewe. Bagamoyo ni mji usioendelea kwa miaka mingi.

Chanika, sehemu nzuri mwisho pale Taliani. Huko mbele sijui Zingiziwa, kwa Mpango sjui wapi huko ni mateso tu. Na uswahilini sana.

Vikindu, ubaya wa Vikindu ina jamii mchanganyiko lakini wamekaa vikundi vikundi. Unaweza kwenda sehemu wamejaa Wapare watupu mtaa mzima viwanja vyote wanamiliki wao. Kuna sehemu unaenda wamejaa Wamakonde watupu, ipo sehemu ina Wandengereko tupu. Hawa wengi ni zao la machinga wa Mbagala na waliouza nyumba za urithi au zao wenyewe Tandika na Mbagala/Magomeni wamekimbilia huko.

Ceteris Paribus, Kibaha is promising. Ile barabara kutoka pale Maili Moja wanataka iwe njia 4 hadi Chalinze so kutakuwa magoli sana. Maroli hayatakuja mjini kwa sababu Kwala wanajenga bandari kavu.

Kumbuka mkoa wa Pwani ndio mkoa pekee Tz usiokuwa na Manispaa.
Sio Pwani tuu, Njombe, Geita, Simiyu zina manispaa?
 
Back
Top Bottom