Wengi wanaosapoti Kibaha wanapaangalia pale Maili Moja, Kwa Mfipa, Kwa Mathias hadi Kongowe tena barabarani. Hivi mmewahi kuingia huko ndani ndani kwenye viwanja vinakouzwa? Ni uzaramoni haswaaaaa, ni uswahili sana.
As for Bagamoyo, ule mji mimi hapana. Haujawahi kunivutia.
Labda maeneo kama Zinga huku nyuma kabla hujafika Bagamoyo kwenyewe. Bagamoyo ni mji usioendelea kwa miaka mingi.
Chanika, sehemu nzuri mwisho pale Taliani. Huko mbele sijui Zingiziwa, kwa Mpango sjui wapi huko ni mateso tu. Na uswahilini sana.
Vikindu, ubaya wa Vikindu ina jamii mchanganyiko lakini wamekaa vikundi vikundi. Unaweza kwenda sehemu wamejaa Wapare watupu mtaa mzima viwanja vyote wanamiliki wao. Kuna sehemu unaenda wamejaa Wamakonde watupu, ipo sehemu ina Wandengereko tupu. Hawa wengi ni zao la machinga wa Mbagala na waliouza nyumba za urithi au zao wenyewe Tandika na Mbagala/Magomeni wamekimbilia huko.
Ceteris Paribus, Kibaha is promising. Ile barabara kutoka pale Maili Moja wanataka iwe njia 4 hadi Chalinze so kutakuwa magoli sana. Maroli hayatakuja mjini kwa sababu Kwala wanajenga bandari kavu.
Kumbuka mkoa wa Pwani ndio mkoa pekee Tz usiokuwa na Manispaa.