Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

CHANIKA is the best
Kwanini?

Sehemu zinazopimwa kwa futi hata siyo pa maana.

Eneo la mita 20 kwa mita 20 mnajikuta mpo watu wawili.

Kiwanja kimoja kinapimwa futi 50 kwa 40 maana yake ni mita 12 kwa 17 chenye mita za mraba 204 wakati cha mita 20 kwa mita 20 kina ukubwa mita za mraba 400.

Hali kama hiyo ipo eneo lote la Wilaya ya Temeke (Mbagala ikiwemo), Homboza, Mkuranga-Vikindu, Kisemvule, na mikoa ya Kusini.

Kinachokuja hapo ni uswazi na vijumba vichafu.

Waswahili hawana utamaduni wa kujenga vyoo bora kwa hiyo hata ukijenga chako kizuri bado mtaa utakuwa mchafu na wewe utakuwa mchafu tu.
 
Me kuna wadau wako huko kiwanja mpak 20mil vipo mpka 100mil hii ni barabarani

Bei ya kiwanja inategemea. Kiwanja chenyewe kiko katika mazingira gani.
Sikatai lakini kwa Chanika hizo ni bei za heka siyo bei za viwanja vya kibiashara.

Mf;Kariakoo kiwanja 30x25 ni 1bill+ wakati hiyo hiyo B ukienda nayo Kibaha unanunua kijiji,na mil 20 ya Chanika Kibaha au Bagamoyo utapata 40x40.
 
Nafikiri ulitakiwa kutaja Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe na Mkuranga kwa sababu kwa sasa miji inakuwa kuelekea huko japo ukuwaji ndio unatofautiana, binafsi siyo tu kupewa bure bali hata ungeniambia nitoe hela kununua kiwanja kati ya hizo wilaya nilizokutajia, bila kupepesa macho ningechagua Bagamoyo hata kama cha Huko ndio kingekuwa na bei kubwa kuliko hizo sehemu nyingine
 
Back
Top Bottom