Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kama ni BAGAMOYO ni chaguo sahihi kwenu,basi msisite kufika katika kampuni yetu ya PMG and ASSOCIATE Co.ltd kupata fursa ya viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali.
Kwa maelezo zaidi piga simu 0674376678
Ok mkuu nina imani wahitaji wamelisoma tangazo lako. Ila umeshalilipia tangazo lako, au umetumia mseleleko tu wa ganda la ndizi 😂😂😂
 
1. Bagamoyo - kuanzia mapinga mpaka Kiromo, hapa kiromo ndio kuna special economic zone, na bandari- kwa sasa usivuke round about, labda kwa uwekezaji wa baadaye, bagamoyo mjini waachieni wazawa

2. Kibaha
Shukran sana kwa mchango wako mkuu. Wajanja tumeokoteza faida fulan katika comment yako.
 
Inamaana wewe Kibaha imekukalia kushoto mkuu, au unamaanisha huko kuna hadhi kubwa hivyo sikutakiwa kupataja katika list hii?
Kibaha sasa hivi ni almost kama Dar tu na Chanika pia ni Dar ile sio Pwani, hivyo niliona kama kuzilinganisha na Bagamoyo na Mkuranga kusingeleta uwiano kidogo, kwahiyo inatakiwa tulinganishe Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe na Mkuranga
 
Tunajadilije hoja ya kufikirika ambayo kiuhalisia haitakuja kutokea kuwepo?

Hata nikijitamanisha kuchagua ni nini kitaninufaisha na uchaguzi wangu huo?
Anyway tuseme una hela unahitaji kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi na familia yako, halafu baada ya kuhangaika kutafuta viwanja unakutana na dalali ana kwambia kuna viwanja vinapatikana Bagamoyo, Vikindu, Kibaha na Chanika. Bei ni moja na ukubwa 40×40.

Wewe utapendelea kwenda kununua na kujenga wapi kati ya hayo maeneo tajwa?
 
Hicho Kiwanja anakupa nani-bure zama hizi? 'ncheke mie, amka unaota 'blaza' 😀

Changa Pesa yako nunua na jenga pale Roho yako itapopachagua.
Kusikiliza ya walimwengu hakuna ambapo hapatakosolewa.

Sijui naeleweka?
Soma tena hapo chini
Anyway tuseme una hela unahitaji kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi na familia yako, halafu baada ya kuhangaika kutafuta viwanja unakutana na dalali ana kwambia kuna viwanja vinapatikana Bagamoyo, Vikindu, Kibaha na Chanika. Bei ni moja na ukubwa 40×40.

Wewe utapendelea kwenda kununua na kujenga wapi kati ya hayo maeneo tajwa?
 
Kwanini nipewe kiwanja cha bure mimi mwanaume rijali?

Hapo umenyoosha vizuri.
 
Kibaha sasa hivi ni almost kama Dar tu na Chanika pia ni Dar ile sio Pwani, hivyo niliona kama kuzilinganisha na Bagamoyo na Mkuranga kusingeleta uwiano kidogo, kwahiyo inatakiwa tulinganishe Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe na Mkuranga
Good, hapa nimekuelewa vizuri my brother. Lakini cha kushangaza bado kuna watu wanazikubali Bagamoyo na kuachana na Kibaha au Chanika ya Dar, vilevile kuna watu wanaikubali Vikindu kuliko hayo maeneo mengine.

Hapo ndo utajua ule msemo unaosema "wewe ukiona cha nini mwenzako anawaza atakipata lini".
 
Chani babu kuko njema ktk nyanja zote miundo mbinu huduma za kijamii kama usafili hospital mahakama vituo vya police NK nk
Kuna watu wanadai Chanika usafiri mpaka uwe mtu wa kuamka mapema yani kuanzia saa 11 hadi saa 1 ya asubuhi. Ukifika kituoni kinyume na hapo basi utarajie kuchelewa zaidi ndani ya basi kwa sababu ya foleni.
 
Kwani wasiokuwa Waswahili wanakaa wapi?
Humu JF Kila mtu mambo safi!
Sinza yote ni full squatter, Magomeni, Temeke Buguruni, Tabata yote haijapimwa..

Niambieni nyie mnakaa wapi kusikokuwa na uswahilli, hakuna misikiti, watoto hawalii!

Au mnajenga humu humu mitandaoni?

Shenzy typ!
Unagongwa na vigagula wewe, Tabata maeneo yake mengi tu yamepimwa. Tuna nyumba ipo kwenye mipango miji from 1980s. Hio Tabata unayosemea squatter ni ile ya nyuma ya Mawenzi kunaitwa Upogoroni kushuka hadi mwananchi pamoja na maeneo yanyopakana na bonde la mchicha.
 
Back
Top Bottom