Story za humu Siku hizi bora hata Facebook πππππππππ
Ukiwakosa hawa utakutana na taarifa za MMU tupuππππ
Na ndo zinakua trending
Hapana,
Hapa kuna hoja nyingi za kifalsafa na kihesabu ambazo wewe ndiye unaweza kuwa hujaziona.
Kuna hoja kubwa ya instant gratification inavyoweza kukukosesha mambo makubwa unayoweza kuyapata kwa delayed reward. Hili ni jambo ambalo Watanzania wengi wanasumbuliwa nalo, ndiyo maana wengi kuweka pesa katika masoko ya hisa au sehemu nyingine ambapo pesa inakua kwa interest ni shida.
Kuna zoezi la hesabu tu kujua sequence and series mambo ya arithmetic progression, geometric progression na realistic limits za peogression hizo ina person's natural lifetime.
Kwa sisi tunaopenda historia, uzi huu unatukumbusha ombi la mtu mmoja aliyemuomba mfalme amuwekee mchele kwenye set ya chess yenye vyumba 64 (kama ya drafti) punje moja chumba cha kwanza, punje ya pili chumba cha pili, punje nne chumba cha tatu, akiendelea ku double mpaka chumba cha 64.
Mfalme hakuelewa hesabu akaona kazi ndogo, kumbe dunia nzima hakuna mchele wa kutosha kuweka hivyo.
Mwishowe jamaa akauawa na mfalme kwa sababu mfalme aliona huyu mtu kamdhalilisha kaonesha mfalme hajui hesabu.
Uzi una mambo mengi makubwa kifalsafa na kimahesabu, lakini kama hujui utaishia kuudharau.