Ukiambiwa upewe Billion 2 sasa hivi au upewe elfu 10 ambayo itakuwa inaji-double kila siku, utachagua nini?

Ukiambiwa upewe Billion 2 sasa hivi au upewe elfu 10 ambayo itakuwa inaji-double kila siku, utachagua nini?

ndio najaua
So kama unajua maana ya ku double ina maana hiyo bilioni 2 sio kitu kwenye 10k itakayo double kila siku..

Ukiingiza kwenye formula baada ya siku 365 wewe ni tajiri wa kwanza duniani na mbinguni...

Ndani ya siku 30 tu wewe ni trilionea.

Siku 365 hiyo hesabu itakua haipo hapa wala mbinguni hata Mungu atakua ajaigundua....
 
Hapo utachagua kipi kati ya elfu 10 ambayo itakuwa ina double kila siku, au billion 2 ya papo hapo ?
Nachagua elfu 10 ambayo inajidouble kila siku (yani leo 10000, kesho 20000, kesho kutwa 40000 na kuendelea

Kwa nini? Kwa sababu itanichukua siku chache tu kufika hiyo Bilioni 2 na hata kuzidi


Day 1
Tsh 10,000

Day 2
Tsh 20000

Day 3
Tsh 40000

Day 5
Tsh 160,000

Day 10
Tsh 5,120,000

Day 15
Tsh 163,680,000

Day 17
Tsh 655,360,000

Day 18
1,310,720,000

Day 19
2,621,440,000 ✅

Hadi kufikia siku ya 19 nitakuwa nimevuka bilioni 2 na zitaendelea kuongezeka soon itafikia Trilioni

So answering your imaginary question, ni heri kupata elfu 10 day 1 na iendelee kuji double kila siku
 
Ikiwa hiyo 10000 ni dollar basi haya ndio mahesabu ya AI

View attachment 3582443
Nadhani AI imekosea
Kufikia 2.6B inachukua only 19 days, na sio 28
PXL_20260501_144735232~2.jpg
 
Nachagua elfu 10 ambayo inajidouble kila siku (yani leo 10000, kesho 20000, kesho kutwa 40000 na kuendelea

Kwa nini? Kwa sababu itanichukua siku chache tu kufika hiyo Bilioni 2 na hata kuzidi


Day 1
Tsh 10,000

Day 2
Tsh 20000

Day 3
Tsh 40000

Day 5
Tsh 160,000

Day 10
Tsh 5,120,000

Day 15
Tsh 163,680,000

Day 17
Tsh 655,360,000

Day 18
1,310,720,000

Day 19
2,621,440,000 ✅

Hadi kufikia siku ya 19 nitakuwa nimevuka bilioni 2 na zitaendelea kuongezeka soon itafikia Trilioni

So answering your imaginary question, ni heri kupata elfu 10 day 1 na iendelee kuji double kila siku
Hamna, sio 10,20,40,80,160,320--->.

Anasema ni 10,20,30,40,50,60--->.

Hapa kwa mwezi ni shilingi 4,650,000 za kitanzania kama sijakosea kujumlisha.

Kwahiyo kufika bilioni 2 si chini ya miezi 4 au zaidi(Japo nimekadiria)

Ila kivyangu nitachagua B2 kesh!!
 
Hapana,

Hapa kuna hoja nyingi za kifalsafa na kihesabu ambazo wewe ndiye unaweza kuwa hujaziona.

Kuna hoja kubwa ya instant gratification inavyoweza kukukosesha mambo makubwa unayoweza kuyapata kwa delayed reward. Hili ni jambo ambalo Watanzania wengi wanasumbuliwa nalo, ndiyo maana wengi kuweka pesa katika masoko ya hisa au sehemu nyingine ambapo pesa inakua kwa interest ni shida.

Kuna zoezi la hesabu tu kujua sequence and series mambo ya arithmetic progression, geometric progression na realistic limits za peogression hizo ina person's natural lifetime.

Kwa sisi tunaopenda historia, uzi huu unatukumbusha ombi la mtu mmoja aliyemuomba mfalme amuwekee nchele kwenye set ya chess yenye byumba 64 (kama ya drafti) punje moja chumba cha kwanza, punje ya pili vhumba cha pili, punje nne chumba cha tatu, akiendelea ku double mpaka chumba cha 64.

Mfalme hakuelewa hesabu akaona kazi ndogo, kumbe dunia nzima hakuna mchele wa kutosha kuweka hivyo.

Mwishowe jamaa akauawa na mfalme kwa sababu mfalme aliona huyu ntu kamdhalilisha kaonesha mfalme hajui hesabu.

Uzi una mambo mengi makubwa kifaksafa na kimahesabu, lakini kama hujui utaishia kuudharau.
Imebidi nikaitafute hiyo historia. Nimecheka sana.
 
Ongezeko la mara mbili maana yake ni asilimia 100. Ni kitu kigumu kutokea. Lakini inafikirisha.

Nimekaa nafanya hesabu ya ongezeko la asilimia moja tu kwa siku. Baada ya siku 30 kuna nyongeza ya asilimia 34. Hii si haba.
 
Back
Top Bottom