Wewe ndio umefeli na chama chako chakavu na katiba chakavu.
Katiba yao Kenya inasema nguvu iko kwa wananchi na wananchi ndio wenye maamuzi kikatiba hivyo kuna ushirikishwaji wa mwananchi.
Umeona jana wananchi walivyokua wanatoa maoni yao Bomas pale , lini Tanzania wananchi waliwahi kujitokeza kujadili kama vile kumtoa ofisini kiongozi mwenye tuhuma?
Mwisho Gachagua hajaondolewa ofisi amepewa nafasi kwenda kufanya utetezi bungeni kuhusu tuhuma hizo baada ya kukusanya signature za wabunge alipojadiliwa akishindwa mjadala utahamia bunge la senate halafu ndio ataondolewa ofisini, lini Tanzania wabunge watakuwa na ujasiri wa kupiga kura za kutokuwa na imani na hata makamu wa rais na ukawepo mjadala wa wazi bungeni na wananchi baadae wakajadili kwa uwazi bila kuhofia usalama wao?
Hapo huoni tu gap , tayari bunge la sasa limejaa CCM kutokana na wizi wa kura 2020 yani wezi wajadili wizi?