Ukibahatika kukutana na Rais Samia utamuuliza swali gani la msingi?

Nitamuuliza kama anawasikiliza wafuasi wa mtangulizi wake,akijibu ndio nitamwambia hana kura yangu 2025
 
Sitamuuliza swali nitamwambia mama tunakutegemea utuvushe twende mbele kamwe usiturudishe tulikotoka.
 
Kwanini hutembelei uridhi wa Baba?
Kwa nini umeruhusu Baba yetu wamtusi Bungeni na mitandaoni kabla hata ya 40 ?
Hujatenda yakupasayo kama Mwafrika na Mtanzania.
Rudi ukatubu
 
Kwakweli bado mapema kwangu mimi kumuuliza swali

ila...
Ningemuomba aandike vitabu vyaa maadili kwa ajili ya vijana
 
1. Kwanini ameshindwa kuunda serikali yake ambayo itakuwa na watu wanaoendana nae?

2. Kwanini mpaka sasa hivi hajatangaza ajira kwa watoto wetu?

3. Kwanini ripoti ya CAG hafanyiwi kazi mfano jizi Hamis Kigwangwala hajachukuliwa hatua licha ya kufanya ubadhilifu wa mali ya Umma?

4. Kwanini mpaka muda huu ameshindwa kutoa tamko kuhusu katiba mpya ya JMT?
 
Wale Covid 19 mama wataondolewa lini???
 
Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?
Yani ukutane na mh Raisi uanze kumuuliza maswali! Kwani we mwandishi wa habari? Hapo ni kumpa PETITION (CV) ili akukumbuke kwenye teuzi.
Kwa kiswahili wanaita kumpeti peti!
 
Nitamuuliza kwanini wizara ya mawasiliano na makampuni ya simu yanamdharau.. amesema washushe bando lakin wamekaidi. Wanamuonyesha dharau za waziwazi kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…