Ukibahatika kukutana na Rais Samia utamuuliza swali gani la msingi?

Ukibahatika kukutana na Rais Samia utamuuliza swali gani la msingi?

Nitamuuliza kama anawasikiliza wafuasi wa mtangulizi wake,akijibu ndio nitamwambia hana kura yangu 2025
 
Sitamuuliza swali nitamwambia mama tunakutegemea utuvushe twende mbele kamwe usiturudishe tulikotoka.
 
Kwanini hutembelei uridhi wa Baba?
Kwa nini umeruhusu Baba yetu wamtusi Bungeni na mitandaoni kabla hata ya 40 ?
Hujatenda yakupasayo kama Mwafrika na Mtanzania.
Rudi ukatubu
 
Kwakweli bado mapema kwangu mimi kumuuliza swali

ila...
Ningemuomba aandike vitabu vyaa maadili kwa ajili ya vijana
 
1. Kwanini ameshindwa kuunda serikali yake ambayo itakuwa na watu wanaoendana nae?

2. Kwanini mpaka sasa hivi hajatangaza ajira kwa watoto wetu?

3. Kwanini ripoti ya CAG hafanyiwi kazi mfano jizi Hamis Kigwangwala hajachukuliwa hatua licha ya kufanya ubadhilifu wa mali ya Umma?

4. Kwanini mpaka muda huu ameshindwa kutoa tamko kuhusu katiba mpya ya JMT?
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamiiforums

Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

View attachment 1754058

Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu ni mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Makunduchi visiwani Zanzibar kuanzia 2010 hadi 2015, na alikuwa waziri wa nchi anaeshughulikia muungano katika muda huo.

Samia Suluhu Hassan ndiye makamu wa rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania. Kabla ya kuwa Rais kutokana na kifo cha rais John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.

SWALI: Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wale Covid 19 mama wataondolewa lini???
 
Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?
Yani ukutane na mh Raisi uanze kumuuliza maswali! Kwani we mwandishi wa habari? Hapo ni kumpa PETITION (CV) ili akukumbuke kwenye teuzi.
Kwa kiswahili wanaita kumpeti peti!
 
Nitamuuliza kwanini wizara ya mawasiliano na makampuni ya simu yanamdharau.. amesema washushe bando lakin wamekaidi. Wanamuonyesha dharau za waziwazi kabisa!
 
Back
Top Bottom