Ukibahatika kukutana na Rais Samia utamuuliza swali gani la msingi?

Atoe nafasi ya kuandikwa kwa katiba hiyo itakuwa legacy yake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Badala ya kutegemea utashi, matamko, mtazamo wa Rais aliyepo bora kuweka katiba nzuri itakayopelekea kujengwa kwa taasisi imara ambayo kila ajaye hatakuwa na budi kuifuata.
 
Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?
 
Kabisa Mkuu ndiyo matatizo ya kutoangalia the big picture and thinking outside the box. Anachokiona hapa yeye kama waliomtangulia ni maccm kushindwa uchaguzi lakini anasahau kwamba wapiga kura tutakuwa na choice ya kuamua chama kipi kituongeze kutokana na kufanya vizuri wakiwa madarakani au kubofoa.
Siku ikipita bila kuwataja CCM haujisikii raha?
 
Kwenye siasa sina cha kumuuliza kwa sababu ameshajibu mengi kwa kauli zake.

Labda nitamuuliza kwenye maisha binafsi.

Anajisikiaje kuwa mke wa tatu nyumbani, katika ndoa iliyo na wake wawili wakubwa kwake, wakati huo huo yeye ni Head of State?

Je, hatua hii ni ya kushangiliwa kwamba Tanzania mwanamke anaweza kuwa mke wa tatu lakini bado akawa rais? Au ni ya kuhuzunisha kwamba mpaka leo ndoa za mitala zipo na mtu anaweza kuwa rais wa Tanzania lakini nyumbani kwake ni mke wa tatu?

Anawezaje ku reconcile maisha ya ndoa hiyo ya mitala na uongozi wa nchi bila kuleta matatizo kwenye ndoa au uongozi wa nchi?

Mengine yote ya kitaalam kuna wataalam wa serikalini wataweza kujibu kwa utaalamu kuliko yeye.
 
1620820171056.jpeg

Sawa mkuu
 
2025 tutawashawishi wananchi wampe Samia ushindi wa 90% Ushindi huu ni wa asante kwa kazi kubwa aliyoifanya.
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamiiforums

Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

View attachment 1754058

Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu ni mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Makunduchi visiwani Zanzibar kuanzia 2010 hadi 2015, na alikuwa waziri wa nchi anaeshughulikia muungano katika muda huo.

Samia Suluhu Hassan ndiye makamu wa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania. Kabla ya kuwa Rais kutokana na kifo cha Rais John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa Rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.

SWALI: Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Nampongeza kwa hatua kadhaa anazoendelea kuchukua, kurudisha imani ya sisi watanzania wengi kwa serikali...kwa vile anadumisha amani, upendo na muhimu zaidi kuondoa chuki, udhalimu, unyanyasaji na siasa za makundi.
Kama mtu ambaye amefanya kazi kama community mobilizer, na activist anajua wananchi ktk level ya chini wana issues gani za msingi.
Ndiyo maana kila mara tangu ameanza u Rais unaona anaangalia sana tangible benefits za wananchi na sio siasa za chuki au makundi na kubaguana !
Najua bado anajipanga ili safu ikikamilika ktk ngazi zote kazi ziendelee kwa ufanisi zaidi.
Nitaendelea kumpongeza kwa sera nzuri za kurudisha mahusiano na majirani, na taasisi na hata kumuita za kimataifa.
You can't rule or foster development in isolation hasa ukizingatia sisi ni party wa treaties mbalimbali na kwa kuwa signatories tuna obligations pia.
Nina uhakika sana kwa style yake ni mtu wa kupokea constructive criticism...
Mwisho nitamshauri aziangalie sana bodi za mashirika mbalimbali...
Akiweza pia anaweza kuanzisha mfumo wa kukubali volunteers kwani upo utaalam mwingi sana mtaani, watu ambao wapo tayari kujitolea hata mara mbili kwa week....
Nchi zilizoendelea wanatumia sana wazalendo kwa mtindo huo. Hawa ni watu ambao sio wanasiasa au watu wa kujikombakomba...lkn wana utaalam flani bado wanao.
Wanaweza kuwa diaspora wakija likizo au wastaafu !
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamiiforums

Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

View attachment 1754058

Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu ni mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Makunduchi visiwani Zanzibar kuanzia 2010 hadi 2015, na alikuwa waziri wa nchi anaeshughulikia muungano katika muda huo.

Samia Suluhu Hassan ndiye makamu wa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania. Kabla ya kuwa Rais kutokana na kifo cha Rais John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa Rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.

SWALI: Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Swali la msingi ni lini serikali itaimarisha upatikanaji wa fursa za ajira kwa watoto wa wakulima?

(A) Mashirika na taasisi za umma yana mikakati gani ya kuongeza ubunifu ili kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana?

(B)Mikopo wezeshi kwa vijana kupitia halmashauri inawezaje kuwapatia watoto wakulima mitaji yenye tija ili waweze kujiajiri na kuimarisha uchumi wao ili kupunguza dhana ya kusubiria ajira chache za serikali, tofauti na sasa vijana 10 kupatiwa milioni tatu ambayo haijitoshelezi kutekeleza miradi yenye tija?

(C) Serikali ina mkakati gani kuweka unafuu wa kampuni na taasisi binafsi ili yaweze kutoa ajira kwa vijana kuwapunguzia makali ya maisha?

Kilio chetu ni ajira kwa vijana. Naumia sana kuona vijana wenzangu wanawekewa mazingira magumu ya kuajiriwa au kujiajiri.
 
Sawa mkuu. Yatamfikia mama kwa maana wasaidizi wake wapo humu humu.
 
Back
Top Bottom