KERO Ukienda Polisi kuwataka watrack Simu iliyobiwa, bila Pesa hufanikiwi

KERO Ukienda Polisi kuwataka watrack Simu iliyobiwa, bila Pesa hufanikiwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
589
Reaction score
1,897
Tarehe 16.7.2024. Nilliibiwa simu ktk eneo langu la kazi. nikaenda polisi kutoa Taarifa wakanipa RB baada ya hapo nikaambiwa ni subili mpelelezi, kufika kwa mpelelezi, ananiambia kutrack simu kuna gjharama. Gharama ya kutrack simu ni shilingi 100,000/=. Thamani ya simu yangu iliobiwa ni shilingi 260,000/=

Nimeenda kituoni kama mara 4 hivi, sipati msaada wowote zaidi ya polisi kutaka Pesa. Mwanzo nilikua na Imani kubwa sana kwa Polisi, ila niliposikia kuhusu malipo ya kutrack simu,niliwaza kupoteza pia pesa maana polisi sio mtu wa kumuamini,anaweza kula pesa yangu na kazi isifanyike.

Nikaa pata wazo lingine kua niende kituo kingine cha polisi wanisaidie swala langu, uko walitaka 80,000/= ila niwalipe cash, na mi nikawapa ombi langu kazi ifanyike ndo niwape malipo yao. wao nao polisi wanasema kuna Ada ya kutrack simu, bila ada ya kiingilio kazi haiwezi kufanyika.

Kuanzia mda huo nilikata tamaa nikaona hii Huduma ya Kutrack simu inawezekana hawa Askari wetu hawaiwezi ndomana wanakua na longo longo, ni jambo ambalo liko nje ya uwezo wao.
 
Kitengo cha upelelezi kuna ambao wamepewa hiyo access na simu juu kwaajili ya kazi hiyo ya kupambana na uhalifu kwa njia ya mtandao.

Cha ajabu hicho kitengo wamekigeuza dili

Ni mambo ya aibu na ajabu kubwa

Wakikosa wateja wanaanza kuzunguka mtaani na kuuza simu bei chee then kesho tu wanakuja kukushika kuwa una simu ya wizi na ilipoibiwa ziliibiwa million 10 . Hutoki ndani mpaka ulipe pesa hiyo iliyotajwa kisha simu wanaichukua wanakwenda kuuza mtaa mwingine.

Hii nchi hapana
 
Wanasema ukiipata, mwizi wako atalipa fidia zote.
Mi nilikwapuliwa na vibaka wa morogoro wanaotumia pikipiki,nikaenda central, nikaambiwa nitoe hela kuitrack. Simu yenyewe ya laki moja, nikaachana nayo.

Na hapo ujue bado gharama kulipia upate loss report. Ukiibiwa simu, kadi za nida, bank, kazi, afya nk ni gharama kubwa kuzirudisha. Wezi watuache tu kwakweli. Wanatutesa
 
Ngoja nikupe hadithi ya kuchekesha! Au tuseme ya kufurahisha.

Mwaka 2018 nilipoteza simu yangu sumsung kali nilinunua laki 9. Kwa Bahati nilikua na imei. Nilienda TCRA ili ifungwe kumkomoa "aliyeiba" ili tukose wote! Yule mtu wa cyber wa TCRA akanihakikishia simu imefungwa.

La haula! Baada ya kama mwezi niliipata simu imetumbukia ndani ya sofa! Sebuleni kwangu! Kuiwasha simu inawaka na inafanya kazi kama kawaida!

Tanzania kuna usanii mwingi sana!
 
Ngoja nikupe hadithi ya kuchekesha! Au tuseme ya kufurahisha.

Mwaka 2018 nilipoteza simu yangu sumsung kali nilinunua laki 9. Kwa Bahati nilikua na imei. Nilienda tcra ili ifungwe kumkomoa "aliyeiba" ili tukose wote! Yule mtu wa cyber wa TCRA akanihakikishia simu imefungwa.

La haula! Baada ya kama mwezi niipata simu imetumbukia ndani ya sofa! Sebuleni kwangu! Kuiwasha simu inawaka na inafanya kazi kama kawaida!

Tanzania kuna usanii mwingi sana!
Huyo litutumbwe ungemlima vibao kwa uongo huo
 
Ngoja nikupe hadithi ya kuchekesha! Au tuseme ya kufurahisha.

Mwaka 2018 nilipoteza simu yangu sumsung kali nilinunua laki 9. Kwa Bahati nilikua na imei. Nilienda tcra ili ifungwe kumkomoa "aliyeiba" ili tukose wote! Yule mtu wa cyber wa TCRA akanihakikishia simu imefungwa.

La haula! Baada ya kama mwezi niipata simu imetumbukia ndani ya sofa! Sebuleni kwangu! Kuiwasha simu inawaka na inafanya kazi kama kawaida!

Tanzania kuna usanii mwingi sana!
haaaaa. Ndugu unapose,ma Tanzania kuna usanii kweli, mambo mengi ni longo longo,
Magomeni Nida niliwai kutapeliwa shilingi 30,000. na polisi akiwa na uniform
 
Ila duniani hakuna cha buree
Huu msemo una ushetni ndani yake.
Huyu polisi analipwa kwa fedha za kodi za wananchi, na analipwa kwa kazi hiyo. Access kapewa na serikali, kapewa na simu kabisa pamoja na computer afanye kazi hiyo la kushangaza anataka pesa. Pesa ya nini huku mshahara analipwa na posho analipwa?
Je, hii kazi anifanya nje ya wajibu wake wa kila siku?
Kwanini pesa wanayotaka isilipwe kwa control number kama malipo ni halali?
Mnalirudisha taifa nyuma, mnalilani taifa na vizazi vyenu vinalaaniwa .
 
Alikua kwa pikipiki.. alivonikwapua mi sikua na papara mana kwa ile kikiri kakara mwenzake akakosa stamina..

Basi wakaanguka na mwendokasi ukapita nao watu wanashangaa mi naenda nachukua simu yangu huyo bila kuuliza
 
Ku track simu sio rahisi huwa nawaambiaga hata watu mtaani wanaopata temper baada ya kuibiwa simu zao.

Hususan hivi vi simu vya low end. Mtu kaibiwa Infinix badala ya kupotezea eti anaanza kuhangaika na ma loss report ili aanze utaratibu wa kui track.

Ukifanya evaluation hiyo simu unakuta thamani yake haizidi 200K na pengine ni ya mkopo kabisa.

Kumbuka zoezi gumu kwa mwizi ni kuiba hiyo simu, mwizi akishaiba hiyo simu basi kuitegua hizo sehemu za kui track simu ni jambo jepesi sana.

Hao polisi wataendelea kula hela zako mpaka utakapokata tamaa.
 
Ngoja nikupe hadithi ya kuchekesha! Au tuseme ya kufurahisha.

Mwaka 2018 nilipoteza simu yangu sumsung kali nilinunua laki 9. Kwa Bahati nilikua na imei. Nilienda TCRA ili ifungwe kumkomoa "aliyeiba" ili tukose wote! Yule mtu wa cyber wa TCRA akanihakikishia simu imefungwa.

La haula! Baada ya kama mwezi niliipata simu imetumbukia ndani ya sofa! Sebuleni kwangu! Kuiwasha simu inawaka na inafanya kazi kama kawaida!

Tanzania kuna usanii mwingi sana!
Hahaaa jamaa alikuchezesha sana
 
Back
Top Bottom