Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Nimekuja mkoani kumtembelea bradha Kuna mzigo aliniagiza nimletee.
Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee hiki kitoto Ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi babaake na mama yake wanamlea Kama yai,full kudeka deka hovyo.
Sasa ni heri wangekuwa wanamlea hovyo akawa anawasumbua wenyewe ingekuwa hakuna shida,ila akiwa na wenzie ni kakorofi kanawapiga wenzie.
Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei,ameshaitanua shingo kwa kunivuta vuta,imekuwa Kama nanyonyesha Sasa. Mara aninyang'anye simu,mara aniparamie usoni Kama mbwa,alafu ana vikucha vikali.
Basi naishia kujichekesha chekesha tu mbele ya mama yake,maisha ya ugenini yana unafiki Sana. Wazazi wake Wala hawastuki,wanaona poa tu mtoto wao anavyoact Kama kingedere. Mamaake ananiambia "shemeji Kama junia anakusumbua mchape" Namchapaje mtoto wa watu ugenini? Kwa nini asimkataze kusumbua wageni na kukachapa kakiendelea kuleta ubishi.
Sasa mamaake akaenda dukani akaniacha na junia tunavutana vutana. Happy ndiyo nikambadikilia nikamwonyesha sura ya ukauzu na kumtoa shingoni maana ilikuwa Kama ananidai kwa jinsi alivyokuwa ananikaba. Nikakashika mikono na kukaminya tuvidole vyake Kama naminya karanga,huku namwambi acha utundu kwa wageni mtoto. Kakaanza kulia kanaelekea dukani kwa mamaake.
Maisha ya ugenini magumu Sana. Nilipanga kukaa siku mbili ila moja tu inatosha kwa kweli.
Wazazi wengine hivi mnaleaje watoto kipuuzi Kama hivi?
Katoto ni ka-attention seeker mpo katika maongezi sebuleni, kenyewe kanapita pita na kuvuta watu nguo ili mradi tu kaonekane kapo live. Mkikapotezea kataangusha hata glass!!
Katoto ka Bro wako ni katoto kako pia, kwahiyo wewe na Bro wako hapo mnaanza kupata hasara.
Halafu wewe naye ni jinga kubwa badala ya kuchukua mamlaka ya kumuonya ulipopewa mamlaka na mama yake (shemeji yako) badala yake ukawa unajichekesha kama zuzu!!🤤-- wewe si ndiye baba mdogo hapo!!
Inaonekana huyo shem wako angekutunuku mzig• pia ungejichekesha ?!!🤣🤣.
Siku zingine usituletee habari za kitoto humu.