Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Leo umenifanya nijisikie vibaya kweli,yaan unatetea tunavyodhalilika mbele ya watoto et ni ukatili..kuna mahali unapotoka mkuu
Mtoto anakudhalilishaje bwana Maweed hebu acha kunichekesha, lakini hapo bado hatupaswi kulaumu mtoto bali ni wazazi wa mtoto
 
Fanya hivi wakati unakabeba beba kamata tako moja halafu ufanye kama unaliviringa kwenda kulia....
Kakifanya ng`a na wewe unafanya ng'a,watajua mnacheza ila lazma wakakape panado maana katalalamika siku nzima..
Ushike mtoto wa wato makalio mkuu uko serious Kweli ,mshike wako
 
Hahaha aise nmecheka mpaka watu wamenishangaa hapa bar.
Kilichonifurahisha ni hiyo Ntakuvunja,Tone utakayotumia na utakavyoishupaza sura dah.
Hawa watoto ukiwachekea chekea utakuza vitu vya ajabu sana! Mimi ni rafiki mzuri sana wa watoto na naelewana nao sana… ila mode zangu wanazijua.. huyo junia mpaka naondoka angekua kapunguza au ameacha kabisa hizo tabia😊
 
Lea wa kwako uwezavyo Mimi wa kwangu nidhamu ni lazima halafu tusipangiane namna ya kulea watoto
Alokupangia malezi ya mtoto wako nani mbona kama umechanganyikiwa? Sisi tunachangia mada iliyopo mezani wewe unaleta fangasi zako
 
Mtoto anakudhalilishaje bwana Maweed hebu acha kunichekesha, lakini hapo bado hatupaswi kulaumu mtoto bali ni wazazi wa mtoto
Mtoto akiingiza mikono mfukoni mwangu si amenifedhehesha...halafu ukumbuke ni mgeni kwanza ndo nafika
 
kuna mwenzako kaanzisha uzi hashibi ugenini naona wewe mtoto wa wenyewe anaharibu shati la vunja bei….all in all pole sana mkuu..fanya hima uondoke mapema kuepuka kero
 
Nimekuja mkoani kumtembelea bradha Kuna mzigo aliniagiza nimletee.

Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee hiki kitoto Ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi babaake na mama yake wanamlea Kama yai,full kudeka deka hovyo.

Sasa ni heri wangekuwa wanamlea hovyo akawa anawasumbua wenyewe ingekuwa hakuna shida,ila akiwa na wenzie ni kakorofi kanawapiga wenzie.

Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei,ameshaitanua shingo kwa kunivuta vuta,imekuwa Kama nanyonyesha Sasa. Mara aninyang'anye simu,mara aniparamie usoni Kama mbwa,alafu ana vikucha vikali.

Basi naishia kujichekesha chekesha tu mbele ya mama yake,maisha ya ugenini yana unafiki Sana. Wazazi wake Wala hawastuki,wanaona poa tu mtoto wao anavyoact Kama kingedere. Mamaake ananiambia "shemeji Kama junia anakusumbua mchape" Namchapaje mtoto wa watu ugenini? Kwa nini asimkataze kusumbua wageni na kukachapa kakiendelea kuleta ubishi.

Sasa mamaake akaenda dukani akaniacha na junia tunavutana vutana. Happy ndiyo nikambadikilia nikamwonyesha sura ya ukauzu na kumtoa shingoni maana ilikuwa Kama ananidai kwa jinsi alivyokuwa ananikaba. Nikakashika mikono na kukaminya tuvidole vyake Kama naminya karanga,huku namwambi acha utundu kwa wageni mtoto. Kakaanza kulia kanaelekea dukani kwa mamaake.

Maisha ya ugenini magumu Sana. Nilipanga kukaa siku mbili ila moja tu inatosha kwa kweli.

Wazazi wengine hivi mnaleaje watoto kipuuzi Kama hivi?
Katoto ni ka-attention seeker mpo katika maongezi sebuleni, kenyewe kanapita pita na kuvuta watu nguo ili mradi tu kaonekane kapo live. Mkikapotezea kataangusha hata glass!!
Hayo matoto siku hizi mengi yana zaliwa na autism,yaani usonjo yanakuwa na utundu hatarishi kabisa na wazazi wengi hawajui
 
Back
Top Bottom