Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Inaonekana malezi yako kwa mtoto ni ya kumdekeza,mtoto alielelewa kimaadili anaonekana kabisa
 


Tatizo linaanzia hapa:

"Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei,ameshaitanua shingo kwa kunivuta vuta,imekuwa Kama nanyonyesha Sasa. Mara aninyang'anye simu,mara aniparamie usoni Kama mbwa,alafu ana vikucha vikali"
 
Mara aninyang'anye simu,mara aniparamie usoni Kama mbwa,alafu ana vikucha vikali. [emoji23]
 
Bora wewe anakukaba shingo mie yule ddogo bwana sii alikuwa ananipiga ngumi za pumbuz😂😂😂😂
 
Halafu huyo mtoto wala sio mtukutu ila yupo excited kumuona Anko wake ndio maana anampandia pandia kwa furaha ila kwa kua watu mmejazwa roho mbaya na ukatili hata furaha ya watoto mnaigeuza chuki,

Hii gender ya Kiume ingeteketea tu [emoji849]
Umeongea upuuzi ujue[emoji23][emoji23][emoji23]sasa gender ya kiume ipotee kwasababu ya watoto na hao watoto kama ni wakiume..

Acha makasiriko mtoto lazima aonywe ajue mipaka yake...kama anafanya tabia mbaya kumbe anaweza kufanya na tabia nzuri ila wazazi wake ndo wamemlea kindezi..

nyie ndo mnalea watoto kama yai akifanya kosa unasingizia bado mdogo...mwisho wa siku kinakuwa kikubwa ndo mnatuletea vipanya road, na viwezi mtaani...muda mzuri wa kumtengeneza mtu aweje baadae ni akiwa mtoto.

samaki mkunje angali mbichi.
 
Kuna dogo aliwahi kunisumbua kinyama nimekaa kwenye kochi ye akaanza kupanda kwenye mabega yangu akashika dirisha akaanza kurukaruka juu ya mabega
Nimeanza kunywa chai wakati nakula mkate akasukuma mkono nikajipaka blueband usoni
Mamaake akaanza kujichekesha na mimi nikajichekesha kiaina ila moyon nilikua nina hasira kinoma

Nimepigiwa simu nikaitoa mfukon wakat naipokea akaipiga ikaruka juu ikaangukia kwenye jagi la maji, mamaake akamgombeza kidogo dogo akaanza kulia hata hajaguswa mama akaanza tena kumbembeleza huku anammwambia mtoto wake nani mbaya? Uncle? Haya tema mate tumpige dogo akatema mate maza akafanya kama vile ananipiga ndo dogo akanyamaza

ilibidi niondoke tu maana ilibaki kidogo nimtandike vibao mama na mtoto wake
 
Haya ndio yalikua malezi mgeni akija akinunuliwa soda mtoto haisogelei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…