Ukifa leo nani atatoa taarifa zako hapa JF?

Ukifa leo nani atatoa taarifa zako hapa JF?

Ila ukifa umekufa tu, hata wadau JF wakipata taarifa hakuna litalobadilika...

Funzo kwenye kifo, ni kwamba unapoona mtu kaondoka ni kiashiria kuwa nawe uliye hai utaondoka hivyo tengeneza maisha yako na Muumba...
 
Mi nadhani hamna haja ya kufahamiana tukifa rambirambi zenyewe hamtoi mtaishia tu kusema mungu kampenda zaidi
 
Mimi naona mnaumiza kichwa tu kwa mambo hata yasiyo ya msingi.
You think people should know about your death , what for??
Mbona wengine taarifa zao zinaletwa..
Simple, violate ur anonymas policy, make urslf public
 
Wengine hapa JF tuko kwa siri kuu. Na inatokea tupo wote ofisi moja lakini hakuna anayemjua mwezie kwa ID Feki 😀 😀 kuna siku nilibahatia kuona boss wangu akichati JF na kulijua jina lake, tena huwa anacomment msg zangu bila kujua!!!...... mambo ya siri huishia sirini hata nikifa itakuwa siri tu.....
 
Kama mtu amekua JF miaka yote bila kujulikana basi hata mauti yake yaheshimiwe kwa kubaki hivyo hivyo.

Ikitokea member mwingine amejua na kuleta taarifa huku JF basi atoe taarifa tu na si location ya msiba, picha ya mwendazake, michango na mbwembwe zingine.

Mtu asitiriwe vile alivyoishi.
 
Ila ukifa umekufa tu, hata wadau JF wakipata taarifa hakuna litalobadilika...

Funzo kwenye kifo, ni kwamba unapoona mtu kaondoka ni kiashiria kuwa nawe uliye hai utaondoka hivyo tengeneza maisha yako na Muumba...
Hajauliza kuhusu mafunzo.
 
Salamu baadae.

Sku hizi RIP zimekuwa nyingi mtaani hata huku. jf wanautaratibu wa kuweka hio status kwenye profile yako pale unapofariki na taarifa wanazipata kutoka kwa watu wa karibu. Sasa swali ni nani mtu wako wa karibu anayeweza kutufahamisha?

Naamini wapo wengi walishatutangulia lkn hatufahamu tunaishia kusema "sku hizi wamepotea".
Zikishatolewa unafufuka ?
 
Back
Top Bottom