Ukifa leo nani atatoa taarifa zako hapa JF?

Ukifa leo nani atatoa taarifa zako hapa JF?

Taarifa ziletwe humu watu waanze kuitafuta sura ya marehemu ili wapate cha kuzungumza wakishakula wali maharage, akuuuu!

Kama wataka ujulikane, verify your ID pia waambie nduguzo waingie kwa akaunti yako watangaze kifo chako.
 
Salamu baadae.

Sku hizi RIP zimekuwa nyingi mtaani hata huku. jf wanautaratibu wa kuweka hio status kwenye profile yako pale unapofariki na taarifa wanazipata kutoka kwa watu wa karibu. Sasa swali ni nani mtu wako wa karibu anayeweza kutufahamisha?

Naamini wapo wengi walishatutangulia lkn hatufahamu tunaishia kusema "sku hizi wamepotea".
Hatujui
 
Siku ya kuacha ID tu bila maudhulio jamii forums hii siku huwa naiogopa sana wapendwa

Vijana wenzangu wa baadae watasoma sana comment zangu nondo

Sijuhi Nani atakuwa mtoaji taarifa

I love jamii forum
 
Kama atakayechukua simu yangu atakuwa member wa Jf basi huyo ndio atatoa taarifa. Maana nimejaribu kufikiria hata watu wa hapa ninaofahamiana nao hawatakuwa na namna ya kupata taarifa
Ah kumbe hujafa. Ngoja nikadelete ule uzi
 
Kama mtu amekua JF miaka yote bila kujulikana basi hata mauti yake yaheshimiwe kwa kubaki hivyo hivyo.

Ikitokea member mwingine amejua na kuleta taarifa huku JF basi atoe taarifa tu na si location ya msiba, picha ya mwendazake, michango na mbwembwe zingine.

Mtu asitiriwe vile alivyoishi.

Kweli kabisa natumain utanisitiri
 
Back
Top Bottom