Wanaume oeni wanawake wenye akili kupata watoto wenye akili. Kusema ukweli mama yangu anamzidi mzee akili hilo naliona waziwazi. I mean uwezo wa kukariri, kuelewa haraka, kutafsiri yaani ukimuelekeza kitu na ukamsimamia kinafanyika.
Ukiweza oa mwanamke anakuzidi akili, wewe uwe na maamuzi, busara, maarifa na ujuzi baadae utaongezea na uzoefu. Watoto wazaliwe na akili za mama yao, wewe mengine utafundisha na kulipia ada. Ila wakiwa matutusa tuition fee utatoa sana, mafunzo utawapa, shule nzuri utapeleka na mitaji utawapa ila wapi vyote bure. Ukifa tu mali wanalewea pombe.
Kuna mzee mmoja marehemu baba wa rafiki yangu alikuwana mke ana akili sana ila hajasoma hivyo mume alikuwa anamtumia kwenye ushauri wanajadili ila mke akisema kitu yule mzee akigundua ni option sahihi anaipinga alafu anamaliza mjadala kiaina. Baadae anaitafakari anamwambia mke wake "Mama Mwisa, lile wazo lako naona kama linakujakuja hivi hebu tutajaribu" hapo ameishakubali ila hataki kumpa credit mke wake asije mpanda kichwani.
Sijasema elimu, nimesema akili.