Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Wakuu,
Kichwa cha thread chahusika.
Yaani ukijifanya kuwa mfuatiliaji sana wa kinachojiri huko kwa wenzetu unaweza pata wasiwasi na kuhisi dunia itafikia mwisho usiku wa leo. Kumbe maisha yapo tu na yataendelea kuwepo sana.
Mwanzoni wakati nasikia Russia ikiwapiga beat Ukraine pamoja na NATO nilidhani Ulaya yote itaangamia, lakini wapi. Mpaka sasa jioni hii watu pande za Ulaya wanakula tu mvinyo kama kawa.
Sasa dawa ya kukomesha hofu tunayolazimishwa na media ni nini?
Ni kupuuzia kila kitu kinachoendelea na kuendelea kupambana na maisha yako tu. Usiache kabisa kufuatilia kinachojiri ila ukishasoma hizo habari we achana nazo na uendelee na maisha yako.
Nilitumia njia hii wakati wa COVID ikanisaidia. Mwanzoni nilikuwa nafuatilia sana habari za COVID kisha nikawa napata hofu, ila tangu nilipoanza kupuuza habari zake COVID ilipita na maisha mpaka sasa yanaendelea kama kawa hapa Duniani.
Mwisho wa thread.