Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Unaendeshwa na hisia sana.. mkuu


Kuna mambo ajabu sana kwenye mahusiano ya kijinsia ungekuwa Shekhe au Padri yamkini ungeelewa au wale jamaa wa dawati la kijinsia.

Hususa maeneo ya mijini.

Na hayafanani.
 
I can imagine watoto wa kiume wanaolelewa na wababa wa aina hii na kulishwa huu "unyama" in the name of mfume dume. Sijui kama kutakuwa na stable families huko mbeleni, ni single families tu. Baba hakosei wala kuomba msamaha; our little men .....
Mkuu wewe ulilelewa kwenye mfumo wa aina gani? Mshua alikuwa hapindui kwa bimkubwa? Ful bebi kam beki tu mii?
 
Zamani ndio kulikuwa na stable famili Kwa sababu ya mfumo dume ninaouzungumzia lakini sasa hivi wanaume kugeuka madume jike ndio kunafanya



😂😂😂😂

So wamekosa vigezo vya kuitwa waume za watu
Hakukuwa na stable family, sema wanawake walivumilia ubabe Kwa kuwa hawakuwa na option, hawakuwa na PA kwenda.
Siku hizi wanawake Wana nguvu ya kiuchumi, wanaweza kujiendesha bila mwanaume, wanachohitaji ni kujaliwa tu.
Wanaume mjifunze kuishi na wanawake waliowezeshwa....mngepata jando la kisasa mkanolewe....mwanamke wa 1900s sio wa 2000s
 
Hakukuwa na stable family, sema wanawake walivumilia ubabe Kwa kuwa hawakuwa na option, hawakuwa na PA kwenda.
Siku hizi wanawake Wana nguvu ya kiuchumi, wanaweza kujiendesha bila mwanaume, wanachohitaji ni kujaliwa tu.
Wanaume mjifunze kuishi na wanawake waliowezeshwa....mngepata jando la kisasa mkanolewe....mwanamke wa 1900s sio wa 2000s


Hata zamani wapo wanawake waliokuwa na nguvu za kiuchumi. Tena wengi tuu.

Sema wanawake WA Zama hizo waliuelewa mfumo dume Kama ndio msingi Mkuu wa usalama wa maadili na utamaduni wa jamii zao.

Sasa hivi wanawake wanazidi kudhalilika na kunyanyaswa kuliko zamani.
 
Hakukuwa na stable family, sema wanawake walivumilia ubabe Kwa kuwa hawakuwa na option, hawakuwa na PA kwenda.
Siku hizi wanawake Wana nguvu ya kiuchumi, wanaweza kujiendesha bila mwanaume, wanachohitaji ni kujaliwa tu.
Wanaume mjifunze kuishi na wanawake waliowezeshwa....mngepata jando la kisasa mkanolewe....mwanamke wa 1900s sio wa 2000s
Huo ni uongo kusema jamii ya zamani wanawake hawakuwezeshwa mfano mzuri ni mimi katika jamii yanu wanawake walikuwa wanamiliki mashamba na mifugo ambayo hupata pale wanapotolewa mahari

na hiyo yakusema kunyanyaswa na kunyimwa kuwezeshwa ilikuwa inatagemea fikra za wazazi pia haikubezi kwa wanawake tu hata wanaume mfano baadhi jamii za visiwa komoro,lindi,mtwara na huko hindia kwenye familia walikuwa wanawekeza kwa watoto wa kike katika umilikishwaji wa mali hivyo ilipelekea watoto wa kiume kushindwa kuwa na uchumi imara na hata kwenye kuoa jamii hizo mtoto wa kike ndio huoa na kutoa mahari na mwanaume huenda kuishi kwenye familia ya mkewe pia watoto watao zaliwa hufata ukoo wa mama

Shida sio kuo wanawume wengi wanaubabe pia nyie wanawake wa sasa mlio wezeshwa kiuchumi ukiachana na ubabe wa wanaume pia mnadharau,majivuno na kiburi

Mimi mama yangu alizaliwa 1961 alipo olewa na baba alikuwa ameshafiwa na baba yake hivyo alikuwa anamiliki mashamba na mifugo ya urithi
ukiachana na vyote hivyo alikuwa nurse wa hospitali ya mkoa ila kitu cha kushangaza sijawai muona akimgombeza wala kumfokea baba yangu japo baba yangu hakuwa na kazi yenye mshahara mkubwa sana na baba yangu alikuwa na kiukoloni fulani hivi lakini haikuwa sababu ya mama yangu hakubehave kama wanawake wengi wa sasa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Na wengi wapo kundi hili
Mimi nipo kundi hili,akipokea mshahara robo nzima ya mshahara anahamishia kwenye akaunti yangu kila mwezi,ntapinduaje hapa? Afanye atakavyo tu,simuachii ng'oo...
 
MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE

Anaandika Robert Heriel.

Leo sina mengi ya kusema ndugu yenu. Nimefanya uchunguzi Kama mnavyonifahamu. Nikisemacho ni kweli tupu. Wala sisemi haya Kwa maslahi yangu, au ya mtu yeyote Yule. Nazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa.

Na ujumbe huu usomwe na wangu wote. Mnisikie na kuyafuata ninayoyasema, Kwa maana maneno yangu yamepimwa na kuthibitika kuwa hayana madhara kwenu.

Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).

Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.

Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.

Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.

Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.

Tuna Baba wawili, Baba WA kweli, ndiye MUNGU muumba wa mbingu na Nchi. Na yupo Baba wa uongo ndiye Ibilisi.
Ibilisi Kama Baba mpaka Leo anaamini yupo sahihi, licha ya wengi kuona alikosea. Ubaba ndio upo hivyo. Unapaswa uwe na msimamo. Ikiwa Baba unapaswa kuwa na msimamo basi yakubidi kabla yakufanya maamuzi yoyote lazima utumie akili ili ufanye uchaguzi uliosahihi kwako.

Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.

Utamhesabia siku saba za mwanzo, ikiwa hajakutafuta, utamhesabia siku Saba zingine, ikiwa hatajishusha, mhesabie siku saba zingine mpaka zifike siku 28, asipokuja achana naye kabisa wala usihesabu tena siku.


Ikiwa atarudi kabla hata ya mwezi Kuisha utampokea, kisha utampa barua awapelekee wazazi wake, waandikie na Fidia kadiri utakavyoona kulingana na siku alizokaa, na utoe onyo kuwa kama tabia hii itajitokeza wakati mwingine, barua hiyo itahesabika Kama sehemu ya onyo la mwisho, hivyo akirudi basi mtoto wao utampa talaka.
Ikiwa watashindwa kulipa fidia waambie asirudi wakae naye, au wanaweza kumuozesha na barua hiyo itahesabika Kama talaka kwani sababu utakuwa umeziorodhesha.

Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.

Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe mama Mtawala hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.

Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.

Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.

Ikiwa utakiuka na kukaidi maneno haya basi utajikuta katika taabu ambayo hukupaswa uipitie.

Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.

Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.

Mwanamke akienda kwao Kama hamna hata mtoto mmoja mwambie akae huko huko asirudi. Kama mtakuwa na walau mtoto mmoja kuendelea unaweza mfanyia subra Kama nilivyoeleza hapo juu ya siku 28 yaani kabla mwezi mwingine haujaandama awe karudi, Kama hajarudi fukuza. Wala usimsikilize yeyote.

Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.

Usiponisikiliza;
Kila siku utaenda kujidhalilisha ukweni kuomba omba misamaha Kama Juha,
Kujiliza Liza Kama Paka ukweni ati kisa mwanamke asiyejielewa.
Mwanamke akijua kuwa akikimbia kwao utamfuta atakuwa hata kitu kidogo kakimbia kwao, sijui nini kwao,

Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.

Nafahamu kuna watu watanipinga, Hilo sitalijali na ninalitarajia.
Kuna watu watasema kuwa ninadada au nitazaa watoto wakike, Ndio ni kweli; mashemeji zangu na wakwe zangu WA baadaye utaratibu ni huo nilioutoa.

Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.

Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.

Be a Man not like a man.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Maninazako(sijatukana) nakusifia!
hii na print naweka nyuma ya kabati la nguo
 
Back
Top Bottom