Ukiitegemea biashara yako mpya ikulishe, ikulipie kodi ya nyumba na kadhalika, jiandae kuanguka

Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1,frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota! Mzigo (gharama)1.5m, leseni+bills (bado sijapigia hesabu). Halafu utashangaa TRA sijui manispaa na ving'ora.
Duh hii mbona ni hatari sasa
 
Vilevile usisain mkataba ukiwa na njaa
 
Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1,frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota! Mzigo (gharama)1.5m, leseni+bills (bado sijapigia hesabu). Halafu utashangaa TRA sijui manispaa na ving'ora.
Vya mtumba au special??
Nina biashara ndogo tofauti tofauti kote kuna changamoto lakini angalau biashara ya viatu inalipa, mimi nachanganya mtumba na special ila mtumba ndio unaenda sana, nazungumizia mtumba grade 1, weekend hii liyopita nimechukua mzigo dar nikachanganya na pull meck maana ni maeneo yenye baridi hasa, mzigo ukafunguliwa pale dukani jumanne, ndani ya siku tatu(mpk alhamis) namuuliza muuzaji kaachia pea 70, na pull neck zikawa tayari zimeisha mpk nikajuta kuchukua chache..

Najua moja ya sababu za kuuza kwa haraka ni kua kuna watu wengi walishaweka oda hivyo walikua wanasubiri tuu, ila si kwamba kila siku mambo yanaenda hivyo, inaweza pita hata siku mbili sijauza chochote au uuze pea moja kwa siku, kwa ufupi ni mauzo ambayo kipindi kingine inanichukua mwezi na zaidi kuyafikia, kwahio kushuka au kupanda kwa mauzo ni ka upepo tuu, kikubwa jipe mda pale kabla hujaanza kuhukumu biashara, nakushauri usiwaze kufunga hio biashara mapema, hata mimi nilipitia hapo, na bado kuna siku haziendi vizuri ila najipa mda.

Hili la kutegemea hio biashara ndio ikupe kila kitu ndio kulinifanya nirudishe mpira kwa kipa kwanza, nikamwambia mfanyakazi afunge kwanza sitaweza kumlipa, Kwa kweli kitu ambacho sikuamini Mwenyewe kwa Hiari yake Akasema hapana atauza bila malipo maana anaona kweli ndani hamna kitu ila tukifunga kabisa ndio tutapoteza wateja na pia fursa itaenda na mwingine, aliuza 2 months bila mshahara, mimi ndio nikawa najiongeza kwa uungwana alioonesha, mpk nikaleta mzigo.
 
Mkuu uliza uambiwe. Unafikiri tunapenda? Biashara enzi za jiwe ilikua Kama ugaidi. Madhara Ni mpaka Sasa labda biashara ya kondomu ndo Ina uhakika
Mkuu biashara ya kutoka kirahisi kwa mtu usiekuwa mtaalamu saaaana wa biashara Ni chakula.

Fanya research kwa eneo zuri la kuweka kijiofisi chako ( breakfast , lunch na chakula cha jion kwa mabachelor). Utanishukuru hapa.

Milion 2 kwa kuanzisha kijieneo Cha chakula inatosha.

Huwez kukosa 30,000 mpaka 50,000 kwa siku Kama faida Kama unauza kuanzia asubuhi Hadi usiku.
 
Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1,frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota! Mzigo (gharama)1.5m, leseni+bills (bado sijapigia hesabu). Halafu utashangaa TRA sijui manispaa na ving'ora.
Halafu biashara za hivyo zimehamia mitandaoni , nunua account ya Facebook na Instagram uwe unaweka bidhaa zako huko.
 
Ivi wale ninaowaonaga kwa mzee wa upako wakisema, " miezi mitatu uliyopita nilikuja hapa sina kitu, ila sasa nini nyumba 3, na harrier nimepaki nje" wanawezaje?
Make hakunaga hata mmoja anayetuambia kapataje,kama alidanga, kaiba au kapiga dili sehemu.
 
Biashara ya aina hii haifai mkuu!Maana ukifukuzwa kazi au ukistahafu itakuwa ndiyo mwisho wa biashara.
 
Katika vitu ulivyovitaja hapo, umetaja na bia, kwani lazima unywe bia? Hapo ndipo tunapokosea wengi; kwenye biashara, usitumie sehemu ya mtaji kwenye mambo ya starehe, piga hesabu za maingizo yako kwa kila siku, kama unaona hakuna faida iliyoingia, achana na bia na starehe zingine.
 
Nlitaka kumwambia hivi hivi ajitose mnadani, biashara za frem siku hizi ni changamoto, inabid uwe sehemu yenye watu sana lacvo utamtafuta mchawi.
Ni mwendo wa kuuza bidhaa zako barabarani tu fremu tuwaachie wahindi
 
Wewe ndo uko ubongoni mwangu... hili ndo wazo linanitafuna kichwa now[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…