Ukijiita "MNYONGE" utakuwa mnyonge mpaka kufa kwako,maneno yanaumba. Soma hapa uzinduke leo

Hayo tunaita mawazo ya kujifaliji,ukweli wa mambo % kubwa tujua hii nchi inamatabaka 3au4 ambayo kuna hawa (maisha bora+), kudi lingine ni hawa (maisha Bora) pia kuna hili kudi linaishi (maisha ya kawaida) kudi la mwisho ni kudi ambalo ni dhumuni la maada hii ni kudi fukala,balbaru hili ni kudi lisilojiweza kabisa kudi tegemezi kwa kila kitu na hili ndio tunaita kundi la wanyonge,wanyonge
 
Mkuu binafsi NIMEKUELEWA SANA,
Kuna mtu aliniita mnyonge aliambulia makofi,MANENO HUUMBA,kuitwa wanyonge na kushangilia ni kuruhusu kuendelea kutawaliwa "Mnyonge hutawaliwa na mwenye nguvu"

Ni kipimo gani CCM walikitumia kutupima na kugundua tu wanyonge???

MIMI SI MNYONGE,MUNGU ALINIUMBA MWENYE NGUVU.
 
Yeah! But you still have to fight in order to reach your goals or intended destination. Ukiamua kusurrender na kunyoosha mikono juu then its over for you.
Still nature will keep and drag you where you belong ✌️
Since nobody can outrun his/her destiny
 

Eti jamani mie naona anayejiita mnyonge kama mwanga
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, watumishi mpooooo...
 
Huku uswahilii kuwa mnyonge ni sifa kabisa nawatu wanadeka kwelikweli wakiitwa wanyonge
 
Kwa hiyo ukijiita chuma utakua chuma?
Ukijiita rais utaingia ikulu?
Mnyonge ni neno linatumika na watu wengi. Hii ni nchi huru na kila ana uhuru wa kujiita anavyojiona. Kama wewe mwamba au tajiri au mwenye akili au IQ kubwa hukatazwi kujiita hivyo. Acha wenye kujishusha wajishushe na wenye kujimwambafy (kujikuza) wajimwambafy. Ukweli ni kuwa ukijiita billionaire na wewe siyo huwezi kuwa billionaire, na ukiwa billionaire ukajiita maskini huwezi kuwa maskini. Those are hard facts and not political rhetorics.
 
Kama unakubali kuna watu wanaonewa na hawana njia kujisaidia basi hao ndiyo wanyonge. Je, ulimuona yule bibi kizee alienyang'anywa ardhi, ilichukuwa kuingilia raisi ili kupata haki. Basi hao ndiyo wanyonge. Ni kweli wewe una kauwezo fulani, na si mnyonge kwa sasa. Kama itatokea mtu tajiri akatumia pesa yake kukunyang'anya haki yako, juwa siku hiyo umekuwa mnyonge. Najuwa utasema mahakama zipo, lakini hapo itategemea dau ulilo nalo la kulipia mawakili. Juwa mwenye pesa anapata mawakili "crème de la crème", na wewe unapata wanaosinzia mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…