Ukijiita "MNYONGE" utakuwa mnyonge mpaka kufa kwako,maneno yanaumba. Soma hapa uzinduke leo

Ukijiita "MNYONGE" utakuwa mnyonge mpaka kufa kwako,maneno yanaumba. Soma hapa uzinduke leo

Hayo tunaita mawazo ya kujifaliji,ukweli wa mambo % kubwa tujua hii nchi inamatabaka 3au4 ambayo kuna hawa (maisha bora+), kudi lingine ni hawa (maisha Bora) pia kuna hili kudi linaishi (maisha ya kawaida) kudi la mwisho ni kudi ambalo ni dhumuni la maada hii ni kudi fukala,balbaru hili ni kudi lisilojiweza kabisa kudi tegemezi kwa kila kitu na hili ndio tunaita kundi la wanyonge,wanyonge
 
Kwanza kabisa natangulia kusema SIIJUI KESHO YANGU lakini siwezi kuwa mnyonge kila siku.

Watanzania tumejengewa dhana potovu sana. Hivi unajua kujiita mnyonge ni kujidhalilisha?

Kama ulikua hujui usipopata changamoto katika maisha utakuwa mjinga tu,ukiishi ukiamini"mimi ni mnyonge" utakuwa mnyonge mpaka kufa,hata ukipewa dili ya milioni 100 utaona ujinga sababu tayari una dhana ya unyonge moyoni mwako.

Jitoe kwenye unyonge leo acha mawazo ya miaka 1800s, nani asiependa maisha mazuri? Nani anapenda kuwa mnyonge kila siku?

Ikiwa watanzania wengi wataendelea kuamini wao ni wanyonge wasiojiongeza badi tuna safari ndefu sana kufikia hata Kenya tu.

Unyonge unafanya mtu anatawaliwa, anadharauliwa,anateswa na kuonewa.

Dhana ya unyonge inapaswa kufa haraka sana, mama Samia naomba uhakikishe hilo ili nchi isonge mbele haraka. Kama unakubali ni mnyonge nyosha kidole juu na unipe mwisho wa unyonge ni ni lini kwako.
Mkuu binafsi NIMEKUELEWA SANA,
Kuna mtu aliniita mnyonge aliambulia makofi,MANENO HUUMBA,kuitwa wanyonge na kushangilia ni kuruhusu kuendelea kutawaliwa "Mnyonge hutawaliwa na mwenye nguvu"

Ni kipimo gani CCM walikitumia kutupima na kugundua tu wanyonge???

MIMI SI MNYONGE,MUNGU ALINIUMBA MWENYE NGUVU.
 
Yeah! But you still have to fight in order to reach your goals or intended destination. Ukiamua kusurrender na kunyoosha mikono juu then its over for you.
Still nature will keep and drag you where you belong ✌️
Since nobody can outrun his/her destiny
 
Uchagani ukijiita MNYONGE utatumwa mpaka uzee wako...na kila mtu anataka kujitoa kwenye unyonge.

Ili uonekane una akili ni jinsi unavyopqmbana na changamoto za maisha. Ukitesekeka sana akili itakuja kichwani tu.

Nani asiye penda kuendesha gari zuri? Kuwa na nyumba nzuri?

Eti jamani mie naona anayejiita mnyonge kama mwanga
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, watumishi mpooooo...
 
Huku uswahilii kuwa mnyonge ni sifa kabisa nawatu wanadeka kwelikweli wakiitwa wanyonge
 
Kwa hiyo ukijiita chuma utakua chuma?
Ukijiita rais utaingia ikulu?
Mnyonge ni neno linatumika na watu wengi. Hii ni nchi huru na kila ana uhuru wa kujiita anavyojiona. Kama wewe mwamba au tajiri au mwenye akili au IQ kubwa hukatazwi kujiita hivyo. Acha wenye kujishusha wajishushe na wenye kujimwambafy (kujikuza) wajimwambafy. Ukweli ni kuwa ukijiita billionaire na wewe siyo huwezi kuwa billionaire, na ukiwa billionaire ukajiita maskini huwezi kuwa maskini. Those are hard facts and not political rhetorics.
 
Hata mimi ili suala la kujiita mnyonge huwa sikubaliani nalo.Sababu mnyonge siku zote huitaji mwenye nguvu, yaani mbabe amsaidie,hapo ndipo naona pana shida.

Kwanini ukubali kuitwa mnyonge? Ki uhalisia hakuna anaetaka kuonewa na hata akionewa ni kutafuta mbinu ya kujitetea kwa kila hali na si kutafuta mtu akutetee sababu utaonekana ni dhaifu, sasa kwa nini uhalisia huu usitumike ili wote tujione tuna nguvu na sio wanyonge.

Mimi naona ni vizuri kujiita wenye nchi aka wananchi badala ya wanyonge,sababu hii itatoa changamoto kila mtu kubeba majukumu ya kulinda nchi,kulinda rasilmali za nchi,kufichua maovu,kulinda haki na usalama,pia kuchagua watu wanaowataka ili kuwaongoza. Sababu mwenye chake ukitunza.
Kama unakubali kuna watu wanaonewa na hawana njia kujisaidia basi hao ndiyo wanyonge. Je, ulimuona yule bibi kizee alienyang'anywa ardhi, ilichukuwa kuingilia raisi ili kupata haki. Basi hao ndiyo wanyonge. Ni kweli wewe una kauwezo fulani, na si mnyonge kwa sasa. Kama itatokea mtu tajiri akatumia pesa yake kukunyang'anya haki yako, juwa siku hiyo umekuwa mnyonge. Najuwa utasema mahakama zipo, lakini hapo itategemea dau ulilo nalo la kulipia mawakili. Juwa mwenye pesa anapata mawakili "crème de la crème", na wewe unapata wanaosinzia mahakamani.
 
Back
Top Bottom