Ukikuta Mwanao wa kike Darasa la 6 anaangalia Ngono, unapaswa kufanyaje kumsaidia?

Ukikuta Mwanao wa kike Darasa la 6 anaangalia Ngono, unapaswa kufanyaje kumsaidia?

Mimi kama Millenial huyo mtoto angekuwa binti yangu ningemuita ..namuagiza soda mbili tunakaa nje kwenye bustani ya nyumbani kisha namwambia ulichofanya ni hali ya kibinadamu na lazima kila binadamu aipitie ,hata mimi na mama ako tumefanya ndio mana ukazaliwa wewe ila wewe bado utakiwa usome umalize shule utaleta mwanaume wako tutawapa baraka zenu ili nanyi mkafanye hivyo sawa mwanangu? ...pia usitazame hizo video zitakuletea mazoea hutafurahi ukiwa na mwenza wako muda ukifika unanielewa binti yangu kipenzi? Aya maliza soda yako kanunue viazi na nyama leo nina hamu tule chips mwanangu.FULL STOP

Kuna kitu nawaambia ambao tumezaliwa na wazazi wa 1950s- 1960 hiki ni kizazi cha kipuuzi sana ndio mana hata nchi yetu kuna baadhi ya mambo hayaendi kwa ujinga wao najua mama yangu yupo hili kundi na baba pia ukoloni wa kipuuzi kila muda na ndio mana mimi siwezi omba ushauri kwa mzee bora kijana mwenzangu.
Umeongea vizuri
 
Sisi Waafrika tuna utamaduni mmoja mbaya sana, huwa tunaona mambo ya ngono au afya ya uzazi ni laana kuyazungumza nyumbani.

Huwa tunasubiri mtoto aharibikiwe ndio tuanze kufoka. Lakini ukweli ni kwamba, mtoto wa darasa la 6 wa sasa anajua mambo mengi sana kuliko sisi tulivyokuwa darasa la 6. Dunia imebadilika, habari ziko kila mahali. Usipomweka binti yako chini ukamwambia kwa upendo, 'Mwanangu, mwili wako ukianza kubadilika utahisi hivi na hivi, na ukiangalia vitu fulani vitakuharibu akili, basi mtandao utamfundisha kwa lugha chafu. Ukimya wa mzazi ndio unaosukuma watoto kwenda kutafuta vitu kama maflash na kujaza mambo ya hovyo mtaani huko.
 
Ushauri wangu kama Mzazi.

Ukimkuta Mtoto awe wa Kiume ama wa Kike amekosea, ama amekosea, iwe Kosa Dogo ama kubwa, Malizana naye siku hiyo hiyo, muda huo huo, kama ni kosa linalohitaji kuadhibiwa Mwadhibu hapo hapo, kama ni kosa linalohitaji kumuonya, Muonye hapo hapo, na ukimaliza kumuonya ama kumuadhibu, mwambie yameisha, mwambie yameisha na awe amesikia, ukimwambia Sasa anatakiwa kubadirika.

Hizi mambo za kumwambia Mtoto ngoja nirudi utanitambua Zina madhara.

Cha mwisho Watu wengi hawajui kuwa Dunia hii inaendeshwa na Ulimwengu wa Roho, iwe Negative ama Positive, kama Kuna kitu Shetani anà pambana nacho ni Ndoa, Kwa sababu Ndoa Bora zitazarisha Watoto Bora, Ndoa za ovyo huzarisha Watoto wa ovyo, Watoto wa Mtaani na kadharika, Shetani anapambana kujaribu Ndoa, akifanikiwa anaharibu Matunda ya Ndoa Kwa maana Watoto, na Watoto ambao SHETANI anawalenga, ni wale wenye Hatma kubwa....! Tuwasaidie Watoto wetu kumjua Mungu wakiwa Bado wadogo.
 
Inatisha sana, malezi ni mtihani mgumu sana.

Nafikiri sisi tulikulia nyakati nzuri, miaka 13 tulikuwa tunacheza rede hata blauzi tunavua. There was nothing sexual.
Sure, ilanwa siku hizi wanalelewa na I pad mkononi wanakua wakijua vitu kuanzia mapema
 
Mambo mengne ni kuomba tu yasikukute

Labda umuamishe mimi babu yangu yuko buturi rolya uko my be naweza mpeleka uko akaishi kijijini na wazee na shule kusoma uko

Ila sasa unaweza jikuta unaongeza tatizo au unapunguza tatizo cha msingi ni kuomba tu yasinikute bas
 
Wazazi wengi wanaukoloni wa kizamani ilitakiwa akingemuona anacheki hio video angekauka kimya angemfuta mama yake na kuanza kumueleza kistaarqbu namna ya kuanza kumhoji mtoto sio kufokafoka hovyo kama mbwa watoto wa sikuizi sio wale wa kufokewa hovyo
 
Ujue kuna vitu vingne ni rahisi sana kuviwaza ila ni ngumu sana kuviongelea

Iv saiv ww ukae na mwanao sjui wa kike sjui wakiume uanze kuongelea mambo ya **** na mbolo

Mi nazan tuwatengenezee mazingira wanetu ya kutuogopa maana mtoto akimuogopa mzazi wake hawezi enda kinyume na vle mzazi anataka
Kwa sisi millennials wengi tulitengenezewa mazingira ya kumuogopa baba na hii ilitujenga sana maana ukitaka kufanya au kuwaza mabaya swali linakuja kichwani je baba akijua? Na hii iisababisha millennia wengi tuna mafanikio na tuna tabia nzuru na njema sabu tulimuogopa sana baba
 
Back
Top Bottom