Ukilewa sana kisha ukalala unaweza kuota ndoto ndani ya ndoto na ukiwa kwenye hiyo ndoto ukaota tena ndoto ila process ya kuamka inaweza kukuchizisha

Hii huwezi kusema ndoto ndani ya ndoto ...
Mimi kwangu ni kawaida kuota ndoto ndani ya ndoto

Naweza nikaota jambo fulani alafu nikashtuka lakini hata hiyo kushtuka ni kuwa nimeota nimeshtuka kutoka kwenye ndoto angali bado nimelala.
Ninapokuja kushtuka in reality ndo huwa natambua kuwa niliposhtuka mara ya kwanza nilikuwa naota ndoto nikiwa nashtuka kutoka kwenye ndoto ya ndoto
 
Umeshawahi kuota ndoto za kutisha halafu ndani ya hizo ndoto unajipa moyo ukijiambia lakini hii ni ndoto tu?
Ukija kustuka moyo unadunda mapigo ambayo hujawahi kuyashudia ukiwa haupo ndotoni na jasho jingi sana,

Hivi huwa inakuaje mtu utoke jasho namna ile na wakati umelala na hufanyi kazi yoyote?
 
Mie ndo maana nadhan unakua somewhere unaishi hayo unayoyaota, hizo hofu, kuchoka, maumivu etc.. kwa nn viendelee kuwepo kama haukufanya kweli hayo mambo?
 
Ota uotavyo, ila ukiona choo ndotoni usikitumue.
 
Wasi wasi.

Na wasi wasi ukuzidi katika kuona matukio ya ndotoni, moyo huelemewa na kukufanya ushituke kutoka usingizini.

Moyo kwenda mbio ni impact ya maono hayo ya kutisha ama kufadhaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…