SI KWELI Ukimeza kidonge kwa maji ya baridi sana, kidonge hakifanyi kazi

SI KWELI Ukimeza kidonge kwa maji ya baridi sana, kidonge hakifanyi kazi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hivi ni kweli kuwa mtu anapomeza vidonge kwa maji ya baridi sana ya friji, vidonge hivyo haviwezi kufanya kazi?

IMG_6748.jpeg
 
Tunachokijua
Maana ya kifamakolojia inaitaja dawa kama kemikali, au zao la kemikali (isipokuwa chakula) ambayo hutumiwa kuzuia, kutambua, kutibu, au kupunguza dalili za ugonjwa au hali isiyo ya kawaida. Pia, zinaweza kuathiri jinsi ubongo na mwili wote unavyofanya kazi na kusababisha mabadiliko katika hisia, ufahamu, mawazo au tabia.

Mgawanyo wa dawa unaweza kufanyika kwa namna mbalimbali. Tunaweza kuzigawa kwa kuzingatia;
  • Sehemu zinapofanya kazi
  • Mfumo wa dozi zake
  • Namna zinavyofanya kazi
  • Sheria zinazoongoza utolewaji wake kwa wagonjwa
  • Jinsi zinavyotumika (Kupaka, kumeza au sindano)
Mfano, kwa kuzingatia dozi zake, tunaweza kuzigawa kwenye makundi ya Vidonge, sindano, poda na creme. Pia kwa kuzingatia namna zinavyofanya kazi, tunaweza kuzigawa kama dawa za presha, dawa za maumivu, dawa za kansa n.k. Hii ni mifano michache kati ya mingi.

Kuacha kufanya kazi ikiwa kitamezwa kwa kutumia maji ya baridi sana
Vidonge ni aina ya dawa iliyo kwenye hali yabisi (Solid state), ambayo mara nyingi hutengenezwa kwa kutumia unga wenye kemikali hai moja au zaidi pamoja na viambato vingine vya kuongeza ujazo, kushikilia kemikali pamoja na kuzuia isiharibike kirahisi.

Kitaalam, dawa yoyote inayomezwa hupitia mchakato wa hatua nne ambao huandikwa kwa kifupi kama ADME, yaani Absorption (Ufyonzwaji), Distribution (Usambazwaji), Metabolism (Kutumiwa na mwili kuleta athari tarajiwa) pamoja na Elimination (Kutolewa nje).

Hatua ya ya awali inayofuatiwa na ufyonzwaji wa kemikali hai za dawa yaani uyeyushwaji wa dawa huamuriwa na mambo mengi, ikiwemo joto la mwili na aina ya kimiminika kilichotumika.

Utaratibu wa kimafakolojia unatambua maji kama kimiminika cha kidunia, chenye uwezo na sifa kubwa ya kutumika katika kumeza na kuyeyusha dawa.

Maji ya baridi sana huchelewesha uyeyushwaji na ufyonzwaji wa dawa hivyo kuathiri uwezo wa dawa husika katika kuleta matokeo chanya. Huufanya mwili utumie muda mrefu zaidi kwenye kuleta usawa wa mazingira ya ndani yaliyoharibiwa kwa utofauti wa joto lake asilia na joto dogo la maji yaliyotumika katika kumeza dawa.

JamiiForums imebaini kuwa;
  1. Matumizi ya maji ya baridi sana haisababishi kidonge/dawa iache kufanya kazi, bali huathiriwa katika kuyeyuka na kufyonzwa kwake hivyo kupunguza ufanisi wake.
  2. Pia, maji ya moto sana yanaweza kuiharibu dawa na kupunguza ufanisi wake.
Hivyo, wataalam wa afya hushauri kutumia maji ya kawaida ili kutunza ubora wa dawa pamoja na kurahisisha uyeyushwaji na ufyonzwaji wake ili iweze kufanya kazi yake vizuri katika muda sahihi.
Back
Top Bottom