Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020

Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020

TCRA wanataka kuua Telecom companies , na wakishaua serikali itakosa kodi

Issue sio mimi kua na line zaidi ya moja issue hapa ni wao waweke controls jinsi ya kudhibiti watakaoenda kinyume
 
Serikali ya CCM imejaa washauri wasiojua umuhimu wa pato la Taifa wanakosa pesa nyingi kwenye ununuzi wa line, kwani line nyingi huongeza mapato na pia wenye photocopy hupata pesa wenye viwanda vya karatasi huuza zaidi na Serikali kujipatia kodi
Mshauri mkuu wa mtukufu ni Náibu Rais ndugu Daud Bashite asiye na vyeti anzia hapo ndipo uendelee
Hivi hawa TCRA hawajaona changamoto za kutatua katika sekta ya mawasiliano mpaka wanakuja sheria zisizo na mantiki,sehemu kubwa ya nchi mawasiliano ya simu bado ni dhaifu Sana au hakuna kabisa.
Hayo Ndio mambo ya kushughulikia.

Hii sheria ni ya kisoshalist na kiimla zaidi,ni sawa na kuniambia nisimiliki magari mawili aina ya Toyota.
Tupeni laini ,hizi mbwembwe hazitawasaidia,hongera kwa serikali ya awamu ya tano

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli. Me naina kilicho muhimu zaidi ni kusajili line zote kama inavyotakiwa.
Nchi hii ina upumbavu mwingi sana, hata nikiwa na laini 5 za voda tatizo lao nini? Mimi si ndo najua matumizi yake?
Mpaka sasa nina line hizi

Voda-3
Airtel - 2
Tigo-2
Ttcl-1
Halotel-2
 
Wakuu heshima kwenu, kuna wakati nlisikia kuna sheria TCRA inatulazimu kuwa na ulazima wa kumiliki line moja kwa kila mtandao na mwisho ni tareh 30 Juni, 2020, hii imekaaje? Tutafungiwa laini leo?


Nina simu ya nyumbani hiyo huwa haitoki kabisa ni kwa ajili ya kuwasiliana na watoto! Ngoja nikabadilishe line kabla ya sijafungwa!
 
Tatizo ni wao wenyewe, kama kumiliki zaidi ya lini moja kwa mtandao mmoja ni kosa, inakuwaje kitambulisho cha nida kikubali kusajili lini zaidi ya moja kwa mtandao? Si wangezuia kwenye kitambulisho chenyewe kisikubali kusajili line zaidi ya moja kwa kila mtandao?.
 
REASONS FOR ADDITIONAL NUMBERS

SABABU ZA UHITAJI WA NAMBA NYENGINE ZA ZIADA AMBAZO NI ZAIDI YA NAMBA YA SIMU YA MWANZO

SELECT A REASON
CHAGUA SABABU

1. For additional devices

KWAAJILI YA MATUMIZI YA KUONGEZA SIMU NYENGINE.

2. To separate office and private usage.

KUTOFAUTISHA LAINI YA MATUMIZI YA KIOFISI NA MATUMIZI BINAFSI.

3. To separate business and personal usage.

KUTOFAUTISHA LAINI YA MATUMIZI YA KIBIASHARA NA MATUMIZI YANGU BINAFSI.

4. For Mobile Financial Services

KWAAJILI YA MATUMIZI YA HUDUMA ZA KIFEDHA KUPITIA SIMU.

5. Mobile Number Porting – with reasons

KWAAJILI YA MATUMIZI YA KUBAKI NA NAMBA UNAPO BADILI MTANDANO WA SIMU.

6. Increase Branches/Shops/Business

KWAAJILI YA MATUMIZI YA KUONGEZA MATAWI/MADUKA au BIASHARA NYENGINE.

7. Increase staff/employee

KWAAJILI YA MATUMIZI YA KUONGEZA WAFANYAKAZI.

8. Test Numbers for compliance purposes

KWAAJILI YA MATUMIZI YA MAJARIBIO YA MADHUMUNI YA UFUATAJI WA UTARATIBU.

9. Test Numbers for roaming partners

KWAAJILI YA MATUMIZI YA MAJARIBIO YA HUDUMA ZA KIMATAIFA NA WASHIRIKI.

10.Kupata promition za vifurushi....
 
Ana line nyingi za kila mtandao, wewe ndiyo umekurupuka,

Sent using Jamii Forums mobile app
Akiwa na laini nyingi wewe inakukera? What if kila laini ina matumizi separate? Hao TCRA ni mbwa; mwanzo tuliambiwa unaruhusiwa kusajili laini mwisho 5 kwa kila mtandao, sasa wanakuja na mengine. Taasisi za kitanzania ni za kipuuzi sana.
 
Hebu Wakuu watumie common sense, mimi nina laini mbili za airtel, Voda na tigo...laini moja natumia kwenye simu na moja ya kutumia kwenye modem...itawezekana vipi nikitaka kutumia modem nitoe laini kwenye simu na isababishe nisiwepo hewani siku nzima?.

Wakumbuke hii mitandao haiko stable kwenye suala la network, kuna wakati unanunua bando la airtel unakuta network iipo slow inabidi ujaribu tigo au voda...kwa maana hiyo ni kwamba Mtu unalazimika kuwa na laini mbili walau kwa kila mtandao ili usikwamishwe shughuli zako kwa kutegemea network ya mtandao mmoja.

Kwa nini TCRA wasianze kuziwajibisha kampuni hizi za huduma iwapo nitanunua kifurushi na sijakitumia basi nirudishiwe pesa zangu...maana nalazimika kununua tena kifurushi kwenye mtandao mwingine.
Kwanza watupe reasoning kuna kosa au madhara gani ya kumiliki line zaidi ya moja ya mtandao mmoja maana wengi sisi ni wafanyabiashara vijiji vingine mitandao ya pesa ni kampuni fulani ndo common,na Hakuna benk vijijini nahitaji kununua mifugo au mazao nalazimika kuwa na laini hata tatu za kuweka pesa.
Wasitujumlishe wote Kama ni wahalifu wa mitandao, wengine tupo bize na maisha hatuna mda wa kufanya uhalifu kupitia simu.N
Ni makosa kutujumlisha site.
 
Tarehe 27 na 29 Juni, 2020, nilitumiwa sms hizi.

MUHIMU
You registered more than 1 SIM card using your NIDA ID. TCRA requires you to verify the numbers you own, dial
*106# to check.
Kuna wengine wanamiliki laini mbili kwenye mtandao mmoja kwa matumizi tofauti kwa mfano moja iko kwa modem kwa ajili ya internet na nyingine kwenye simu kwa matumizi ya kawaida. Watafungwa wengi kwa kuwaonea tu. Lakini tujiulize kuna madhara gani kwa mtu kumiliki zaidi ya laini moja kwenye mtandao mmoja, ikiwa zote amezisajili kisheria?
 
Kuna wengine wanamiliki laini mbili kwenye mtandao mmoja kwa matumizi tofauti kwa mfano moja iko kwa modem kwa ajili ya internet na nyingine kwenye simu kwa matumizi ya kawaida. Watafungwa wengi kwa kuwaonea tu. Lakini tujiulize kuna madhara gani kwa mtu kumiliki zaidi ya laini moja kwenye mtandao mmoja, ikiwa zote amezisajili kisheria?
Ni kweli ukisemacho.. ila kuna wengine wamewasajilia ndugu, watoto, marafiki, wake/waume.. sijui hapo inakuwaje.. Maana mtumiaji si mwenye jina lililosajili laini hiyo
 
Nchi hii ina upumbavu mwingi sana, hata nikiwa na laini 5 za voda tatizo lao nini? Mimi si ndo najua matumizi yake?
Mpaka sasa nina line hizi

Voda-3
Airtel - 2
Tigo-2
Ttcl-1
Halotel-2
Pole!
 
Nifanyeje kwa watoto wangu wawili ambao nimewachukulia laini za voda? Kawaida tunawasiliana nao mara kwa mara kwani nasafiri kikazi mara nyingi na nilisajili laini tatu kwa jina langu
 
Mimi Nina laini zifuatazo,
Voda 4 hapa ninatumia 3 moja anatumia mama angu
2 tigo zipo 5 zote natumia mimi mwebyewe
3. Airtrl moja ambayo natunia pia
4. Halotel 1 kwa sasa siitumii
N.b laini anayotumia mama ni yangu Na sidhani kama ni haki kunizuia kuwasiliana Na mzazi kisa namba ya simu yangu kuiweka kwenye simu yake nchi hii INA mengi ya kufanya Na so huu upuuzi wanaotuletea.
 
Wakuu heshima kwenu, kuna wakati nlisikia kuna sheria TCRA inatulazimu kuwa na ulazima wa kumiliki line moja kwa kila mtandao na mwisho ni tareh 30 Juni, 2020, hii imekaaje? Tutafungiwa laini leo?

TCRA watupe ufafanuzi wa sheria hii.
Na Je?
Ukiwa na SIM card MOJA kil a mtandao inakuwaje?.....

Halotel a Sim card moja
Airtel Sim card moja
Vodacom Sim card moja
TIGO sim card Moja
ZAIN Sim card moja TTCL Sima card moja
ZANTEL Sim card moja

Sheria inasemaje hapa?
 
Nchi hii ina upumbavu mwingi sana, hata nikiwa na laini 5 za voda tatizo lao nini? Mimi si ndo najua matumizi yake?
Mpaka sasa nina line hizi

Voda-3
Airtel - 2
Tigo-2
Ttcl-1
Halotel-2
Ha ha ha.. hapo faini ya m5 kwa Kila line ya ziada, andaa Tsh m25 jumlisha sh 75 ,000 kwa siku kwa Kila line kujihakikishia usalama
 
Back
Top Bottom