Ukimuondoa Rais Samia, kama ni lazima awe mwanamke, then mwanamke huyo ni Dkt. Tulia, ameonesha uwezo, anaweza! Tumchagize au tuache tu bora liende?

Ukimuondoa Rais Samia, kama ni lazima awe mwanamke, then mwanamke huyo ni Dkt. Tulia, ameonesha uwezo, anaweza! Tumchagize au tuache tu bora liende?

Huyuhuyu aliepo alipata urais kwa kudura za mwenyezi Mungu, Tulia naye atulie kama jina lake labda kudura za mwenyezi Mungu zinaweza zikampitia,kwa uhalisia wenyewe wote hawafai kushika na fasi ya urais,kwa kuwa hata dini zenyewe zinakataa mwanamke kuwa kichwa.
Hizo ni kudra zetu hao wandewa , mungu haouni kitu kabisa, laiti ungeyajua ya mwenge?
 
Siwezi kubishana na wewe nafahamu unanizidi kila kitu umri mpaka kipato ila nina babu yangu anaye mzaa mama uwa ananiambia jitaidi kueshimu unacho kiamiani. Ata kama itakupunguzia sifa leo ila kesho itakujengea heshima. Sasa kama wewe ni law school graduates alafu unatupumbaza sisi wajukuu wako mzee unazeeka vibaya.
 
Uwezo wa watanzania kufikiri ni mdogo sana aisee!
Kule kulalamika IPU na kuongea kiingerrza fasaha ndo kigezo cha uongozi??Kiingerrza?Kiingerrza kweli?
basitena mwanaume anakuja na bandiko la kushadidia mtu kutoa boko dah Mungu tusamehe, hv Paschal hujui rais wa taznania anapatikanaje hujui utamaduni wa ccm kumpata rais au huna la kufanya ukaona uchezee simu
 
Dr tulia kutoka kuwa mwalimu wako wa Sheria pale mlimani mpaka kuwa dada yako au ndio mabandiko ya wakubwa.

Nje ya mada mkuu.kule Kwa majirani hawawezi wakatupa yule waliyemtengua na sisi tukawapa dada yako mkubwa?tukajaribu maisha mengine

Kwani toka lini tuna zoezi la kubadilishana wafungwa? 😂 😂 😂 😂 . Mambo hayo yapo Israel and Palestina.
 
Lakini alisema mwenyewe kuwa amepata urais kwa kudra za mwenyeji Mungu hakusema ni kudra zenu.
Sio tuu ni amesema mwenyewe bali ukweli ni Mungu ndie huweka serikali za mataifa,na Rais Samia alipoulizwa na Kikeke, kuhusu 2025,Rais alijibu “Kwanza kazi ifanyike ya 2025 aachiwe Mungu”

Hivyo rais wa Tanzania 2025 amepangwa Mungu na sio lazima awe ni Dada Mkubwa, anaweza kuwa mwingine yeyote hata Dada Mdogo kama nilivyo eleza hapa kuhusu 2025 Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
P
 
Wanabodi,

Kwanza anza na hii video
View: https://youtu.be/kg56zhQjTOg?si=WL_ZQz4gr8fX1VV1
angalieni nchi za wenzetu, linganisha na kwetu, Dr Tulia wa IPU na Dr Tulia wa pale mjengoni kwetu, unaweza kudhani ni watu wawili tofauti.

Hili ni bandiko la swali la kuzungumzia uwezo wa wanawake kwenye lile "jambo letu lile", (naomba nisiliseme), ukimuondoa Rais Samia, kama ni lazima awe ni mwanamke, then mwanamke mwingine ni Dr. Tulia Akson Mwansasu, ameonyesha uwezo, analiweza lile "jambo letu" hivyo kwenye bandiko hili nauliza, je tumchagize kwenye lile "jambo letu", kwasababu ambazo ziko obviously au tuache tuu mambo yaende hivyo hivyo yanavyopaswa kwenda, kama maji kufuata mkondo, kwa kuachia ule utaratibu wa kawaida wa mserereko hata kama ni bora liende, liende tuu?.

Angalizo: JF ni ukumbi wa wote, watoto, vijana, wakubwa na wazee, mimi ni mwandishi wa habari wa wote, nawaandikia watoto, vijana, wakubwa na wazee, ila pia kuna baadhi ya hoja ni za kikubwa, kwanza huwa zinapanda muda watoto wamelala hivyo huwa nawaandikia , wakubwa tuu na sio watoto, hivyo hili sio bandiko la watoto.

Namna ya kujipima kama wewe ni.mkubwa ama mtoto, ni ukijiona umesoma pale nilipoandika "jambo letu" ukijiona wewe unajiuliza hilo "jambo letu" ni jambo gani, basi ujijue tuu hili bandiko sio zaizi yako, okoa tuu muda wako, jiendee mabandiko mengine ya saizi yako.

Hapa ninauzungumzia huo uwezo mkubwa wa Dr. Tulia alionao na aliouonyesha hapo juzi kati, ni upi, kauonyeshea wapi na ana fiti vipi kwa lile "jambo letu lile"?.

Kwanini Dr. Tulia auonyeshee uwezo wake huo kule badala ya hapa nyumbani wakati ni jukumu la mhimili wake kuisimamia serikali yetu!, Je tumshinikize kwa Bunge letu kwanza li do the right thing, kuitekeleza ile hukumu ya Mahakama ya Rufaa, kuhusu ubatili wa katiba yetu na ubatili wa sheria zetu?, kwanini Bunge letu liendelee kututungia sheria batili zinazokwenda kinyume na katiba?.

Kitendo cha kumpa Rais wetu kuzisaini sheria batili kinyume cha katiba, kutakuja kutokea wabunge makini ambao watahitaji Ibara ya 46A ya katiba yetu itekelezwe, kwanini huu mhimili wetu wa Bunge utufanyie hivi wakati mhimili huu uko chini ya Mwanasheria nguli, mbobezi na mbobevu?.

Endelea kufuatana nami mdogo mdogo. ambapo Rais Samia japo anaitwa Mama, kwa umri wangu mimi ni Dada (mimi ni wa 60s) na Dr. Tulia, ni mdogo kwangu, hivyo mimi nawaita ni madada wawili, mtu na dada mtu, au mtu na dada yake, mmoja ni Dada Mkubwa , mwingine ni Dada Mdogo.

Mhimili Mkuu kabisa ni Serikali unaongozwa na Dada Mkubwa, mhimili wa pili kwa ukubwa ni Bunge, unaongozwa na Dada mdogo, tena almanusa na ule mhimili wa tatu, kama tusingepindisha katiba, CJ aendelee kinyume cha katiba, kwenye hierarchy ya mhimili ile, the most senior ilikuwa aingie Mwanamke!,ikabidi katiba ipindishwe kidogo hivyo tungekuwa chini ya madada watatu, "Three Sisters". Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.

Kuhusu jambo letu, kwa vile mada ni kumhusu Dada Mdogo na uwezo wake kwenye lile jambo letu, sio vibaya nikiendelea kusisitiza kuwa hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Dada Mkubwa, tena wengi walimjua baada ya kukabidhiwa lile jambo baada ya lile tukio, lakini angalia akina sisi, tulianza nae wapi, au tulianza nae lini.

Kili kitu kumhusu Dada Mkubwa na Dada Mdogo na Jambo letu zama deep hapa...
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kwa wale wa short and clear unaweza kumruka Dada Mkubwa, uka jump kwa Dada Mdogo

Tuje kwa Dada Mdogo ambaye ndiye mwenye Bandiko lake.
Naomba kuanza na declaration of Interest,
Dada Mdogo ni mwalimu wangu wa sheria, mwaka wa kwanza UDSM, somo letu la kwanza, hivyo naomba usijekuonekana hapa ni mwanafunzi anampigia promo mwalimu wake ili ndio awe yeye kwenye lile jambo letu!. No!, hapa ni meritis, facts na hoja.

Kujifagilia rukhsa!, mimi ndie mtu wa kwanza kutangaza humu jf kuwa Dada Mdogo atakuwa Spika wetu Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... humo nilisema

Hivyo, ilipojitokeza fursa ya U Spika, nilisema Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa? na Dr. Tulia alipoukwaa Uspika, hatukumkopesha nilisema Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

Alipoingia akaanza moto wake Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi
Akaendelea kuwasha
Pamoja na mazuri yake yote, Dr. Tulia pia ni binadamu, anaweza kukosoea, hivyo alipokosea kwenye madudu ya IGA ya DPW na bandari zetu, tulimpaka "IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Mazuri yake, yameendelea na Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria? na alipoukwaa urais wa IPU ndio funga kazi, juzi kati ndio kafunga kazi.

Hitimisho.
Kwa vile Dada Mdogo ameonyesha uwezo kuwa anaweza na kiukweli anaweza, kwa vile kwenye lile jambo letu, tumeamua twende na mwanamke, na , japo katiba yetu, imeweka umri wa mwanzo wa lile jambo letu lakini hakuna umri wa ukomo, lakini kwa public service umri wa ukomo wa utumishi wa umma ni miaka 65, ambayo Dada Mkubwa atakuwa ameitimiza kabla ya jambo letu,kwa vile lile jambo letu waliowengi ni generation Z,ambao ni wasumbufu sana, na Dada Mkubwa atakuwa 70 kusumbuana na hawa vijana ni kumchosha bure Dada Mkubwa mnaonaje tukimshauri Dada Mkubwa aamue kumpisha kwa kumuachia Dada Mdogo aimalizie ulemserereko wa lile jambo letu, na yeye ajipumzikie mapema?, maana nilimsikia hapa Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Jumamosi Njema
Paskali

Huyo Tulia anafaa kuwa mke wako mdogo nyumbani kwako. Ndiyo Kazi atakayoiweza. Kukupunguzia machungu ya mke mkubwa.
 
Si ajabu nchi yetu tunapimwa IQ yetu ipo chini sana across jamii nzima! Yani mtu akiunda slogan tu au akifanya comedy moja tu basi anateka nchi nzima kustahili kuwa rais!! National embecility. Bwana Mtilikila alisema ule unyani haujatuisha yani (Apodomia) yani mtu akija na mkungu wa ndizi nyani tunaukimbilia kama mazuzu tu! Mungu atusaidie kama yupo angalau tupate akili kijiko kimoja tu!

Wasomi wa nchi hii wameshindwa kusaidia kabisa kuna haja ya kutafuta mfumo mpya kabisa wa kuwezesha watu wetu kupata ufahamu wa kupambana na maisha yao, elimu ya kimagharibi imetufundisha kuandika na kusoma tu ila maarifa waliondoka nayo wakoloni!
 
Huyo Tulia anafaa kuwa mke wako mdogo nyumbani kwako. Ndiyo Kazi atakayoiweza. Kukupunguzia machungu ya mke mkubwa.
We dogo JAYJAY ,heshima kitu cha bure, ishike ikushike!Spika Dr Tulia ni mke wa mtu na mama wa familia,muheshimu, kila mtu anastahili heshima。
P
 
Back
Top Bottom