Wewe mwenyewe mwanzoni umesema ni syndrome ( AIDS) acquired immunodeficiency syndrome na pia umetaja baadhi ya organs mfano, liver, kidneys nk tafsiri yake ni kwamba hivyo virus vinaenda kushambulia hizo organs na dalili anazokuwa nazo ni za hizo organs ulizo zitaja. Anyway hiyo kitu siyo ya kuombea sana wala kufutahia sana. Nina ndugu yangu wa karibu alipata shida kama hiyo akawa kichaa, akavua nguo kabisa tukazungusha hospital lakini ikaja kubainika ana hicho kitu alipewa dawa akawa vizuri. Alipewa dawa za ukichaa ( chlorpromazine) pamoja na ART/ ARV, akarudi kwenye hali yake ya kawaida hii ilikuwa mwaka 2015, hadi sasa yuko salama anatumia dawa maisha yanasonga. NB: Kabla ya hapo mdugu na jamaa walisema amerogwa na tayari akawa amesha pelekwa kwa waganga wa kienyeji