Ukimya wa Philip Mpango na Mwigulu kwenye ishu ya DP World unashangaza

Hela za Mwarabu wachukue wengine,mzigo abebe Mpango !.
 
ΩˆΩŽΩ„ΩŽΨ§ ΨͺΩŽΨ±Ω’ΩƒΩŽΩ†ΩΩˆΨ§ Ψ₯ΩΩ„ΩŽΩ‰ Ψ§Ω„Ω‘ΩŽΨ°ΩΩŠΩ†ΩŽ ΨΈΩŽΩ„ΩŽΩ…ΩΩˆΨ§ فَΨͺΩŽΩ…ΩŽΨ³Ω‘ΩŽΩƒΩΩ…Ω Ψ§Ω„Ω†Ω‘ΩŽΨ§Ψ±Ω ΩˆΩŽΩ…ΩŽΨ§ Ω„ΩŽΩƒΩΩ… مِّن Ψ―ΩΩˆΩ†Ω Ψ§Ω„Ω„Ω‘ΩŽΩ‡Ω مِنْ Ψ£ΩŽΩˆΩ’Ω„ΩΩŠΩŽΨ§Ψ‘ΩŽ Ψ«ΩΩ…Ω‘ΩŽ Ω„ΩŽΨ§ ΨͺΩΩ†Ψ΅ΩŽΨ±ΩΩˆΩ†ΩŽ

(HUD - 113)
Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.

Sent from my vivo Y67 using JamiiForums mobile app
 
PhD ya Mpango ni kusomea darasani na kufanya utafiti.
Sawa sawa na PhD za Maaskofu.

Kikubwa ni kuwa tulijikwaa kumpa cheo mtu asiyestahili kwa hisani za Huruma.

Matokeo yake ndio haya.
Na Bila kumshtua kwa kelele angeuza kila kitu pamoja na yeye mwenyewe.
 
Bosi wao SSH aliposema kule Moshi kwamba ameamua kukaa kimya ule ni msimamo wa serikali, kufanya kazi kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi na kuweka siasa za malalamiko pembeni.

Pia kuna tangazo la TPA la kutaka mwekezaji mpya, litakuwa limesomwa na kueleweka. Kusema serikali inataka kuuza nchi ni upungufu wa uelewa wa kijamii.
 
Wakati mwingine mkataba kuonekana ni mbovu ni uelewa wetu kuwa duni. Haiwezekani ukaiacha biashara pana ya mizigo ya Rwanda, Congo kisa eti msafirishaji, huo ni upuuzi wa kiwango cha juu sana.
 
kuna ugonjwa aliugua Pilato alipo mhukumu yesu bila kosa unaitwa " KAMA WEWE UKIM,WACHIA HUYU BASI SIO RAFIKI WA CAISARI" huuu ugonjwa unawasumbua sana wanasiasa wengi barani africa.
 
Lisemwalo ......
Ila mama kaharibu sana maswala ya bandari, ngorongoro, umeme, madini, mafuta. Labda ni kweli, VIATU NI VIKUBWA SANA KWAKE, labda alitakiwa awe anakata utepe, mazingira, haki za watoto na kina mama tu...πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Uzuri na Samia naye kakaa kimya
 
Kwa jinsi hali ya kisiasa iliyvokuwa hapa nchini hivi sasa, CCM imeshaanza kukigwaya na kukiogopa kivuli chake chenyewe. Baada ya kifo cha Mwl. Nyerere, wakati wa utawala BWM nidhamu na mshikamano wa viongozi Ilianza kupotea ndani yake, na viongozi wakaanza kuangaliana kwa jicho la "elites" vs non-elites". Wakati wa utawala wa JK waliangaliana kwa jicho la kimtandao, Kisha wakati wa utawala wa JPM waliangaliana kwa jicho la ukanda na ukabila.

Kwa sasa wanaangaliana kwa jicho la Uzanzibar, Utanganyika na udini. Muasasi wa chama aliwapa angalizo kuwa ukisha kula nyama za watu huwezi kuacha tena. Dhambi hii sasa inawatafuna, kwa kuwa CCM ya sasa ni chama mseto ambacho kimepoteza asili yake.

Chama kimewaweka kwa pamoja makada wenye mitazamo na itikadi tofauti kabisa. Mseto huu huwajumuisha makada asili, wale wakuja, makinikia, wahafidhina, machawa, wafia chama, wenye maslahi binafsi japokuwa hawakipendi chama, n.k.

Kila kada anahangaika na ligi yake mwenyewe. Sera za chama zimebakia kuwa zimeandikwa katika makaratasi, hakuna anayezisoma wala kuziishi, ni kama bwawa la tope tu lililojaa kambale wakubwa na wadogo, ila wote wana sharubu, Kila mmoja wao anapigana vita vyake mwenyewe, wanafanana kwa kitu kimoja (sharubu), wote wananuka ufisadi uliotamalaki.
 
Thubutu ngoja tuone na wazee wa chetezo washatoa waraka ivi
Jiandae kisaikolojia Novemba mosi wanaanza kazi pale TPA. Wazee wa chetezo kuna kipindi wanakuwa ni binadamu tu kama mimi na wewe, wanayo maslahi yao pia na miongoni mwao kuna wanasiasa wanaojivika majoho ya uchungaji mfano ni Father Kitima aliyekuwa mwenyekiti wa kamati za kampeni za urais wa Tundu Lissu mwaka 2020.
 
Kama kuanza kazi kwa ule mkataba bila marekebisho yoyote waache waje waanze kazi.
Ila ujue haitapita muda mrefu tutawapindua tena.
Kama walivyo pinduliwa Zanzibar baada ya Mkataba wa Chifu Mangungo.
Kuwaacha waje kuanza kazi kwa ule mkataba ni fedheha kwa viongozi wetu wa Kitaifa.
 
Ukweli ni kwamba nchi imegawiwa bure kwa Waarabu. Serikali iseme huu uwekezaji una thamani gani?
 
Sidhani kama unao uelewa wa masuala ya mikataba mingi inayosainiwa na kuendesha miradi mingi hivi sasa.
 
Ukweli ni kwamba nchi imegawiwa bure kwa Waarabu. Serikali iseme huu uwekezaji una thamani gani?
Ukiwasikiliza sana wanaharakati kina Prof Tibaijuka lazima upotoshwe na kuwa na maoni ya namna hii. Bandari inajiandaa kuwa na waendeshaji watatu wa kigeni mpaka muda huu.

Pia kule Tanga kutakuwa na mwingine, lengo ni kupata kwa asilimia zaidi ya 90 kile kinachotakiwa kipatikane kupitia sekta ya bandari. Paul Kagame alimponda JK kwamba anayo bandari na bado nchi yetu inashindwa kusimama yenyewe.

Mama Samia anaufanyia kazi kwa vitendo ushauri huo. Lengo ni pale TPA paweze kuwa na waendeshaji wawili pamoja na mamlaka yenyewe. Bandari ya Tanga pia inakwenda kupatiwa mwendeshaji mwingine.

Maendeleo ya kweli hayapatikani kwa watu wa nchi hii kuwa na akili zile zile za kizamani zisizotaka kubadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…