#COVID19 Ukimya wa Serikali dhidi ya chokochoko za Askofu Gwajima, Je imempuuza? Inamuogopa? Anainamlia timing?

Great thinker [emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr mshana ,,hapa u pool off,,the government imefeli kujibu hoja za asikofu gwajima ,,kama umemsikia anasema wandae mdaharo aitwe Yuko Tayari ,alafu asikofu gwajima ni mtu Mungu anafundisha kondoo wake watende mema
 
Hawana majibu ,,
 


 
Hawatakaa abadani walete majibu mkuu kwa hoja za gwajiboy! Wamefunua makabrasha yote kabatini ili wapate pa kudesa kitu kinasoma not reachable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hii ndio chanjo ya kwanza Tanzania? Kwa nafasi yake kama mbunge je hiyo ndio ilikuwa njia sahihi ya kuwasilisha hoja yake?
Hii sio chanjo ya kwanza, lakini hii ni ya majaribio, kwa sababu madhara yake ya muda mfupi, muda wa kati na ya muda mrefu hayafahamiki. Pia aliwasilisha hoja zake bungeni kama mbunge na sasa anawasilisha hoja zake kaniasani kwake kama askofu.Yupo sahihi kabisa100%.
 
👏👏👏
 
Serikali sio ya kipuuzi kiasi Hi ho mpaka imjibu mpayukaji...! Kuna namna ya kuwasiliana kuna namna ya kuwasilisha hoja
Gwajima kaenda kuropoka kwenye kanisa lake halafu mnataka serikali imjibu? Are serious?
Kama kuna kitu serikali itafanya basi ni kuchukua hatua kulingana na,maadili ya uma.. Ufafanuzi umeshatolewa elimu imeshatolewa... Wengi wenu mmebaki na kutaka ajibiwe badala ya kuangalia serikali imesema nini
 
Mr mshana ,,hapa u pool off,,the government imefeli kujibu hoja za asikofu gwajima ,,kama umemsikia anasema wandae mdaharo aitwe Yuko Tayari ,alafu asikofu gwajima ni mtu Mungu anafundisha kondoo wake watende mema
Unadhani huo ndio utendaji wa serikali? My foot[emoji1787][emoji23][emoji23] eti iandae mdahalo na gwajima...hii kali
 
Siku moja pale Magomeni Kanisani Mama mmoja aliibiwa simu na kibaka, akapiga mayowe, wanachi wakaanza kumkimbiza yule mwizi. Kumbe wale hawakua wananchi pale vibaka wenzake wakimkinga jamaa asidhuriwe. Walikua wanajifanya kumpiga huku wakimwelekeza pa kukimbilia...kibaka akatokomea hakukamatwa.....

Moral: Kibaka hawezi kumkamata kibaka mwenzie ila sijataja mtu
 
Ila kaka Mshana Jr, Gwaji boy kuna hoja alizozijenga na kusema tangu mwanzoni akiwa Bungeni kuwa haipijgi Chanjo na akakiri uwepo wa ugonjwa. Alichotaka ni kujibiwa kwa Hoja kitaalamu kwa Mgagasiko wa maswali aliyokuwa nayo lakini hakuna mtaalamu hata mmoja ambaye amejitokeza hadharani kumjibu.

Ukisema mpaka sasa tumechanjwa chanjo ngapi na hakuna anayehoji uhalali wazo, nami nikuulize, Je chanjo ya Polio ilichukua miaka mingapi mpaka kuja kufanikiwa!? Chanjo ya Surua ilichukua miaka mingapi mpaka kufanikiwa!? Uangalie uhalali wa dawa za Mseto, ukikaa na daktari mliyeshibana, hatakushauri utumie Mseto(take it from me).

Kaka Mshana Jr hebu mjibuni Gwajima Chidi kwa hoja na sio Mkono wa baunsa, au habari za kufufua. Tunataka mumjibu kwa hoja sisi mambo yao ya kifamilia hayatuhusu!
 
Dada yetu D.Gwajima viatu vya Wizara ya Afya havimtoshi kabisa avivue tu yeye na timu yake yote.
Tumuombe mtoa mada atusaidie kutuambia staha na "HAIBA" ya mtumishi wa Umma inatapswa kuwa vile? Uongeaji wa mtumishi wa Umma mwenye renki kubwa ya Wizara anapaswa kujibehave vile? Hapo mtoa mada haoni na hawez ongelea sababu ameamua kutolea hasira zake kwa mtu mmoja.

Kujiuzulu ni sehemu ya kutunza legacy na imani kwa umma.....

Walichofanya hawa mawaziri miezi michache nyuma na hivi sasa ni kuiaminisha umma kwamba serikali inaweza kudanganya na kujikanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hili kosa la Gwaji-mwanaume liko wapi? Dorothy na serikali ya awamu ya tano waliziruka kimanga chanjo na kupigia debe nyungu, wakuwashangaa ni wapigia debe nyungu ambao gafla misimamo yao imebadilika akiwemo Gwaji-ke na Rais mwenyewe. Gwaji-Mwanaume msimamo wake umebaki palepale.

Nguvu kubwa ilitumika kuzipinga chanjo awamu iliyopita, watumie nguvu hiyo hiyo kuwashawishi wananchi wakachanje, sio kutisha wasiotaka chanjo. Yaani watu tuliowakabidhi dhamana ya uongozi jana walisema chanjo hazifai, leo wanasema zinafaa, sisi wananchi wa kawaida tusiokuwa na uelewa wowote tufuate lipi? Makosa yao yaliyopita wasitake kumtwisha Gwajiboy.

Tunataka katiba mpya ambayo itaweka miongozo ya sheria, sera na taratibu zitazotumika kuongoza serikali kwa miongo na miongo na kubainisha sera katika mambo yanayohitaji dharura, Kama sio Katiba mpya basi wapinga katiba mpya watuambie ni kwa namna gani tutapata hii miongozo "written" itakayofuatwa na serikali za awamu zote ili tuondokane na hizi drama za kila serikali kuja na lake, tuandikeni maandishi yoyote yale ambayo yatatumika kama sheria, hata tusipoyaita katiba tuyape jina lingine (sababu kuna watu wakisikia katiba mpya wanapandwa na jazba na kuanza kufunga watu magerezani) nauliza tena kama si katiba mpya ninini basi tufanye, tunahitaji majibu!

Hata hivyo, MIMI NIMEISHA CHANJA, Sio kwa ushawishi wa serikali wala wa gwajinani sijui. Serikali isiwe kichwa cha mwendawazimu, kuna watu wanategemea sana msimamo wa serikali katika kufanya maamuzi yao, wanawatesa sana wananchi!
 
Moral: Kibaka hawezi kumkamata kibaka mwenzie ila sijataja mtu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uhamasisha huu, umekosa uungwaji mkono kwa sababu nyingi ikiwemo: Kutumika kwa watu walewale waliokuwa hawaamini katika sayansi. Makosa hayo yanachagizwa pia na Mama kutumia watu wa Aliyetangulia ambao hawataki kubadili mitazamo yao.
Kundi Hilo ndilo limpalo nguvu Mchungaji.
Yajayo yanafurahisha. Naomba kwa Allah ampe nguvu mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…