#COVID19 Ukimya wa Serikali dhidi ya chokochoko za Askofu Gwajima, Je imempuuza? Inamuogopa? Anainamlia timing?

#COVID19 Ukimya wa Serikali dhidi ya chokochoko za Askofu Gwajima, Je imempuuza? Inamuogopa? Anainamlia timing?

Serikali inamwogopa Gwajiboy... simple.

Angekuwa Mwananchi wa kawaida akichochea watu wasichanjwe muda huu angekuwa ndani ya shimo la tewa.
 
Ngoja nikueleze kitu bwana mkubwa, hakuna mwanadamu asiye na haya...halafu hivi vitu vinafanyika public sio mafichoni ushawishi wa gwajima ni mkubwa isitoshe sio mtu wa hovyo ( Ameelimka) na anajua kuitumia elimu yake ipasavyo, anajua kujenga hoja...naweza kusema wanajipanga namna nzuri ya kumwingia bila kuharibu image ya kisiasa isitoshe gwajima yupo upande wao (CCM) kwa hiyo kama watachanga karata zao vibaya watajikuta wanapoteze imani kubwa kwa wananchi ogopa sana binadanu aina ya gwajima anaweza kukusumbua kuliko gaidi. Wako wachache sana, kiufupi jamaa kawazidi maarifa, BBB serikali wakitumia nguvu tu...wameumia[emoji4]
 
Kwani hii ndio chanjo ya kwanza Tanzania? Kwa nafasi yake kama mbunge je hiyo ndio ilikuwa njia sahihi ya kuwasilisha hoja yake?
Tatizo sio chanjo ya ngapi, chanjo zinataratibu zake na zinafahamika hii inatutia wasiwasi kwanza ipo kwenye majaribio, mosi imechukua muda mfupi mno km uitengeneza...lanazima kuwepo na taharuki
 
Mliokuwa mnamsifia kipindi cha Makonda,leo mnamwita mwongo, so kwa hiyo inawezekana hata kipindi cha Makonda alikuwa anasema uongo.

Manake mlimsifia na kumpamba kipindi cha Makonda, leo mnamponda wakati ametumia style ile ile aliyo itumia kwa Makonda. Ila si shangai baadhi ya wabongo, wanapenda kusikiliza na kusifia ujinga na Gwaji anapita mule mule, japokuwa ikitoa hizo personal attacks kwa waziri, still kwenye chanjo bado ana hoja.
 
Anayepotosha NI Waziri na Naibu wake, Ukijaribu kutizama msimamo wa waziri huyu huyu na naibu wake miezi mitano iliyopita ndio kile kile anachokiongea Gwajima kwa sasa (Na aliongea hivyo tangu awali), Kilichotakiwa ni waziri ama naibu waziri wajibu hoja ama maswali yanayokinzana na msimamo wao wa sasa. Wao ndio walituambia mambo ya Chanjo na Dna & rna. Walichokosea ni ku attack personality badala ya kujibu hoja na kutoa elimu.

Naibu waziri alisema chanjo hizi zinaenda kugusa Sijui DNA & RNA pasipo kujua madhara yake, atuambie sasa ni kipi kimebadilika hadi tuziamini tena.
 
Mshana jr kule bungeni nani anayeweza kuwatetea watu wasiotaka kuchanjwa?
Kama ni Spika Tuambie
Kwani msimamo wa Gwajima ulikuwa upi kabla na baada ya kupata Ubunge.
Tumia uganga wako kutubashiria Madhara ya Chanjo kwa miaka ijayo. Wewe unaweza kujuwa tatizo la mtu kabla hata hajafika kwako.
Jibu hoja za Gwajima. JJ wametengeneza busta hakuna majaribio yeyote yaliyofanyika heti inasaidia kupambana na kirusi cha Delt.

Naona kama una support upande wa Serikali .
America wameshndwa Corona na Taliban ni bora Mchina aliyefanikiwa kudhibiti Corona
 
Kila jambo lina uwili...Hata kulia kuna uwili wake. .huwezi kulia milele kuna siku utacheka na huwezi kucheka milele kuna siku Italia
Sakata la usalama wa chanjo ya korona linaingia wiki ya tatu sasa kama si nne! Ni kinara wa hili sakata ni mchungaji Josephat Gwajima.

Ambaye ameshiriki kikamilifu kukwamisha, kuyumbisha na kupotosha dhana nzima ya chanjo husika! Gwajima ni kiongozi wa kiimani mwenye wafuasi wengi.. Hivyo kampeni take imeleta madhara makubaa nchi nzima

Upotoshaji wake ambao naweza kuupa vipengele vya seasons ni kama wiki hii unaingia season four sasa.. Seasons hizi huwa zinaanza siku ya ibada Jumapili kwenye kanisa lake na huwaandaa watu kuanzia Jumatano yake!

Huko ibada zake maranyingi si za kiroho bali za kupambana na wale wote wanaoenda naye kinyume.. Huko atakuchamba, kukusiliba na kukusema atakavyo na waumini wake watashangilia sana halafu watatoa sadaka

Je Gwajima anaijua vema miiko ya kuwa mtumishi wa kiimani? Je Gwajima anaijua vema miiko ya kuwa mtumishi wa kisiasa? Weledi? Heshima? Hekima? Tafakuri!? Utu? Katika nafasi zote mbili?

Ni wazi Gwajima kashindwa kuyatambua mambo muhimu makubwa matatu yanayomfanya awe na uono kimo cha mbilikimo

Kashindwa kabisa kujitambua yeye ni nani Kashindwa kabisa kujjijua yuko wapi, Kashindwa kabisa kujijua anafanya nini...!

Kama kiongozi wa kiimani na kisiasa kuna code of conduct inamuongoza kwenye kila nafasi! Alikuwa na nafasi nzuri kabisa ya kuwakilisha hoja Zane kupitia channel sahihi kama mbunge na pia kama kiongozi wa kiimani

Cha ajabu kashindwa kufanya hivyo na kuamua kutumia mimbari anayoita ya kimungu kupayuka na kuropoka, yaliyokosa, weledi, yaliyokosa uhalisia, yaliyokosa ithibati, yaliyokosa heshima na hekima na yaliyojaa upotoshaji mkubwa.

Hao waumini anaowatetea wasichanjwe ukiwaona wanatia huruma..wana shida. Wana dhiki kama zote! Wamepigika kimaisha na wengi wao ni wagonjwa wa magonjwa mengine mbalimbali
Wanatumia dawa nyingine za mzungu
Wamepata chanjo nyinginezo
Wameshawahi kupata chanjo na dawa nyinginezo na zikawaletea side effects
Wanatumia vitu vingi sub standards vyenye madhara kiafya kuanzia vyakula mpaka vinywaji na vingine vipo hapo nje tu ya kanisa lake

Sijawahi kusikia akitoa elimu ya afya kuhusiasa na vyakula vya kusindika viwandani, mbolea zenye kemikali, wanyama wa kukuzwa kwa madawa, carbonated juices, vidonge vya uzazi wa mpango na njia za kuzuia mimba zenye madhara mengi kiafya...lakini la chanjo yeye ndio kawa daktari na mshauri bingwa..

Chokochoko zake zimeingia hatua mbaya ya sasa, kutoka kisiasa mpaka mambo binafsi, mambo ya kifamilia, siri za familia ...hapa kavuka mipaka.. Ni wazi kabisa kashindwa kujitambua yeye ni nani yuko wapi na anafanya nini...!

Kama ni kukosea walikosea wanasiasa na mawaziri wote enzi za kayafa... Ule utawala ulikuwa wa one man show huwezi kupingana naye kama unajipenda.. Waliokengeuka kauli sio Dorothy pekee ni karibia mawaziri wote kama sio wote!

Kwa ubovu wa katiba tuliyonayo waziri wa afya yuleyule wa Magufuli inabidi sasa aende na biti ya Samia.. Ni ngumu lakini hakuna namna labda ujiuzulu..wanasisa wetu wengi ni vinyonga na hatuna katiba nzuri ya kuwaongoza!

Gwajima anaumizwa na kuukosa uwaziri..Gwajima kwa kificho yuko nyuma ya kundi kubwa faidika enzi za kayafa ambalo halina furaha na mama Samia.. Ukiachana na tofauti zao kifamilia..Gwajima hampingi waziri wa afya anampinga rais kupitia msaidizi wake!

Serikali iko kimya sana kwenye hili.. Ni uamuzi mzuri na wa busara japo una madhara yake.. Kutokurupuka kwenye ishu hii ya Gwajima kungefanyika kwa wengine na kwenye mengine ingepata mileage kubwa sana!
Gwajima anachokonoa sana ili ajibiwe..lakini hajibiwi.. Dorothy alijaribu lakini haraka sana akagundua kosa lake na kaamua kukaa kimya! Ukimya wa serikali dhidi ya upotoshaji na chokochoko za Gwajima ni kama kumpuuza lakini Gwajima amakinike kwakuwa ngoma ikivuma sana HUPASUKA!View attachment 1904222
Huyu ni Mshana kweli au kuna mtu ame-hack ID yake?
 
Wewe mbona unampeleka mtoto wako akachanjwe anapozaliwa zaidi ya chanjo 3.. umewahi uliza side effects za hizo chanjo? Na kwanini hujauliza mpaka leo? Au wewe ni miongoni mwa misukule wa Gwajima!?
Kwa sababu hizo chanjo zilishafanyiwa majaribio za muda mfupi, muda wa kati, na muda mrefu
 
Ni kukosa hoja, serikali haina hoja za kumjibu Askofu Gwajima, ndio maana wapo kimya. Tukiwauliza side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 ni zipi kwa atakaechomwa na kwa watoto atakaowazaa wanabaki kutoa macho kama panya aliyebanwa na mlango.
😀 😀 😀 😀. Jamaa alihoji hata contents tu za hiyo chanjo macho yanawatoka ndio itakuwa madhara yake?. Kwenye hili la chanjo wamekurupuka.
 
Nimefuatilia kwa karibu majibu machafu na ovyo ya huyo Gwajima (siamini kama kweli ni mchungaji au askofu mwenye karama), Kama kweli ni mchungaji kuna ethics zake, ni upumbavu na upuuzi kujitapa kuwa hata kama amelala na mrembo yule kwani kuna shida gani? Hivi ni wewe unayehubiri kanisani neno la Mungu na kumdharau mke wako na familia yako? Huo si ubabe bali ni ujinga uliokomaa kupita kiasi. Kwa hiyo mafundisho yako ya dini yana-based wapi? Kwa watu kusaliti ndoa zao? Sasa una tofauti gani na asie na dini huku ukijidai wewe ni askofu? Kama kweli wewe ni kiongozi wa dini, unapaswa uwe na ile moral behavior na ujali pia ethics za kazi zako. Unachokifanya kinaendelea kukushushia heshima kiasi kwamba huna tofauti na wengine wenye tabia za kishenzi na kipuuzi. Hufai kwa lolote wewe mchungaji au askofu Gwajima, huna adabu, wala hekima na pia hujitambui. Sitaki kuongelea mengi kukuhusu ila bottom line ni kuwa hufai.

Credit kwake field marshall1
Swali....Je nikichanja nitaambukizwa au sitaambukizwa?
Jibu......utaambukizwa

Swali... kwa nini nichanjwe?
Jibu....wewe sio askofu mwenye karama.

Mshana"....you are exposing yourself, stop it. Chanjo ni ya hiyari.
 
Nimefuatilia kwa karibu majibu machafu na ovyo ya huyo Gwajima (siamini kama kweli ni mchungaji au askofu mwenye karama), Kama kweli ni mchungaji kuna ethics zake, ni upumbavu na upuuzi kujitapa kuwa hata kama amelala na mrembo yule kwani kuna shida gani? Hivi ni wewe unayehubiri kanisani neno la Mungu na kumdharau mke wako na familia yako? Huo si ubabe bali ni ujinga uliokomaa kupita kiasi. Kwa hiyo mafundisho yako ya dini yana-based wapi? Kwa watu kusaliti ndoa zao? Sasa una tofauti gani na asie na dini huku ukijidai wewe ni askofu? Kama kweli wewe ni kiongozi wa dini, unapaswa uwe na ile moral behavior na ujali pia ethics za kazi zako. Unachokifanya kinaendelea kukushushia heshima kiasi kwamba huna tofauti na wengine wenye tabia za kishenzi na kipuuzi. Hufai kwa lolote wewe mchungaji au askofu Gwajima, huna adabu, wala hekima na pia hujitambui. Sitaki kuongelea mengi kukuhusu ila bottom line ni kuwa hufai.

Credit kwake field marshall1
Mkuu mshana hata huyo waziri naye anamajibu ya hovyo tu ndiomaana awali bandiko langu nikakwambia unafeli unapo weka sides, kama mtu alikua kwenye cabinet ya kwanza na sasa amebadilika alitakiwa aseme waziwazi aliamini nini na sasa kwanini amebadilika badala yake anahangaika kuatack personalities, nimesema woote hawako sawa na unaposhadadia kuwa the whole cabinen imebadilisha mwelekeo jiulize ni kwanini? na kwanini sasa wana msimamo mwingine? jamani watanzania sio wajinga wana akili zao mjue. Suala la uasikofu sijui nini halina tija hapa ishu ni mambo anayouliza hayana mashiko? mtu leo unatwambia chanjo ni sumu keshokutwa wewe huyohuyo unabadilika kisa umehamia kwenye nyumba ya mmiliki mwingine unasema haina shida, utaeleweka kweli? Reasoning ya watanzania ni kubwa msifikiri hawajui kitu
 
Swali....Je nikichanja nitaambukizwa au sitaambukizwa?
Jibu......utaambukizwa

Swali... kwa nini nichanjwe?
Jibu....wewe sio askofu mwenye karama.

Mshana"....you are exposing yourself, stop it. Chanjo ni ya hiyari.
Chanjo sio hiari chanjo ni lazima..uhiari wake unakuja na vigezo na masharti
 
Back
Top Bottom