Ukimya wa Tanzania na JWTZ Kule Congo DRC si wa Kawaida – Kuna Kitu Kinachezwa?

Ukimya wa Tanzania na JWTZ Kule Congo DRC si wa Kawaida – Kuna Kitu Kinachezwa?

Bi Tozo hana uelewa wowote na masuala ya geo-politics, waziri wa ulinzi mwenyewe hajui lolote kuhusu masuala ya kivita ma usalama. Siku ile kathibitisha baada ya kubadili darubini mbele nyuma na nyuma mbele halafu yupo busy utasema yupo serious, sasa sijui alikuwa anaona nini, kwa maana darubini ukiigeuza pa kuangalizia unaona taswira ya kitu ipo mbali zaidi...

We imagine mtu darubini hajui kutumia, hivi atakuwa ana uelewa hata na kinachoendelea DRC?

Haya mambo yanahitaji kiongozi mwenye uelewa kwa upana kuhusu migogoro hii na historia zake, tena uelewa kwa undani zaidi, haya masuala yanahitaji intel.

Inahitajika kiongozi mwenye kujua historia za undani kuhusu majirani zake.

Mtu anasikiliza taarabu atajuaje hayo masuala?
Kwamba 🤣🤣
downloadfile.jpg
 
JW wapo goma na wameishapiga kazi ya kutosha na wanaendelea kupiga kazi na video za operation ya kuigomboa radio ni gumu kuzitizama kilichofanywa pale so far wamefanya kazi nzuri ni vile sisi tunawadharau ile huko nje wanaheshimika sana Tena Sana
 
Kagame na jeshi lake la m23 wako vizuri kwenye medani na zana za kisasa za kivita kuliko nchi zote za maziwa makuu.

Habari za sijiu nduli Amini alishikishwa adabu hizo ni zilipendwa.
Si kweli
Hakuna kitu. Pumba tupu. JW zamani sio sasa.... Na Kwa Namna Tunavyomuogopa Kagame Kimbaumbau trust me JW hata pua hawezi kusogeza😁😁
Jidanganye kaa mkao mzuri kuanzia kesho sikiliza habari vizuri.
inaudwa kikosi ya upepo wa kisurisuri kutoka south africa zimbabwe botswana zambia malawi na waongozaji Tanzania with full military equipments SADC imetoa fungu hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa(Congo)na wanachama wenzake kumuangalia tu.
Dharau za PK kwa Ramaphosa zimewakera marais wote wa SADC sasa mission ni moja tu PK aondolewe madarakani au lah basi achakazwe hadi awe na adabu..
Poleni wanyarwanda mnaenda kuumia sababu ya majivuno ya PK wenu.
 
JWTZ ikachukue kandarasi Hilo ipige Pesa
Hizo ndizo Kazi zenyewe.

Ndani ya JWTZ kiundwe kikosi kingine cha kushughulikia mambo ya Nje ya mipaka ya Nchi.

Vijana waajiriwe wakapige Kazi. Hela iletwe nchini.
Hayo Mengine ya sifa za kijinga tuachane nayo
Good!
Ila viongozi wetu hawa wengi hua wapo pale tu hawana revolutionary idea wanachojua wao wakiamka wanaingia ofisini wanasign jioni wanaondoka wapo kimazoea tu ndo maaana hata lile tukio lililotokea 2021 wahuni walitaka kwenda kinyume na Katiba wakati huo boss mkubwa yupo zake Ihumwa hata hajui kama anapaswa kulinda katiba...mwisho wa siku wenye Nia njema wakamsanua ndo yy kushtuka
 
Si kweli

Jidanganye kaa mkao mzuri kuanzia kesho sikiliza habari vizuri.
inaudwa kikosi ya upepo wa kisurisuri kutoka south africa zimbabwe botswana zambia malawi na waongozaji Tanzania with full military equipments SADC imetoa fungu hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa(Congo)na wanachama wenzake kumuangalia tu.
Dharau za PK kwa Ramaphosa zimewakera marais wote wa SADC sasa mission ni moja tu PK aondolewe madarakani au lah basi achakazwe hadi awe na adabu..
Poleni wanyarwanda mnaenda kuumia sababu ya majivuno ya PK wenu.
Amka utakojoa Mkuu..
 
Good!
Ila viongozi wetu hawa wengi hua wapo pale tu hawana revolutionary idea wanachojua wao wakiamka wanaingia ofisini wanasign jioni wanaondoka wapo kimazoea tu ndo maaana hata lile tukio lililotokea 2021 wahuni walitaka kwenda kinyume na Katiba wakati huo boss mkubwa yupo zake Ihumwa hata hajui kama anapaswa kulinda katiba...mwisho wa siku wenye Nia njema wakamsanua ndo yy kushtuka

Maana unaweza ukashangaa wanaopelekwa huko wengine sio kwa kupenda bali kushinikizwa.

Sasa kiundwe Kitengo kwaajili ya vitu vya namna hiyo watu wajiunge Kwa ajili hiyo
 
JW wapo goma na wameishapiga kazi ya kutosha na wanaendelea kupiga kazi na video za operation ya kuigomboa radio ni gumu kuzitizama kilichofanywa pale so far wamefanya kazi nzuri ni vile sisi tunawadharau ile huko nje wanaheshimika sana Tena Sana
Tutaaminije au ndo poropaganda zimeanza
 
Sio kila Jambo tuwaige wazungu.
Mengine tunaweza kujiongeza wenyewe.

Kwa nchi yetu ulinzi na Usalama ni huduma ambayo wananchi lazima wapewe lakini ulinzi na Usalama ni biashara inayolipa kama tukiiuza kwa nchi zingine.

Serikali na vyombo vya kijeshi vinaweza kuundw Kitengo kingine cha kijeshi ambacho kitapewa mafunzo ya kijeshi na kitahusika zaidi na mission za Nje ya Nchi.
Hapa wachukuliwe wale watu ambao wanapenda Michezo Hatari, Dili Hatari na wapiganaji wa Kulipwa lakini Kwa maslahi yao na maslahi ya Nchi.

Kisha Kazi ianze.
Kuliko vijana wawe Panya road au mateja huko mtaani na barabarani na Wana hobby ya mambo kama hayo ni Bora wapelekwe huko

Lakini lazima wapewe mafunzo ya kimedani wawe na uwezo.
Sio waende kuuza roho Zao huko
We jamaa unaakili sana lkn unakuwaga mjinga mjinga sana😨
 
Kwa anayefuatilia kinachoendelea DRC, hasa katika mkoa wa Goma, atakuwa anajiuliza: Liko wapi lile jeshi jasiri la JWTZ ambalo mwaka 2012-2013 liliwafurusha waasi wa M23 na kuwafanya wasambaratike kabisa?


Kwa mshangao mkubwa, baada ya uchaguzi wa DRC na kuingia madarakani kwa Félix Tshisekedi, waasi wale wale wa M23 wameibuka tena kwa nguvu mpya, wakiwa na uwezo wa kuteka Goma na sasa wakielekea Bukavu. Inaonekana lengo lao ni kuimega DRC, lakini kosa ni la nani?


  • Je, ni Tshisekedi mwenyewe, ambaye kwa sera zake ameshindwa kuimarisha ulinzi wa nchi yake?
  • Au ni MONUSCO, ambalo lilifuta vikosi vya kulinda amani kuwa chini ya Chapter 6 badala ya Chapter 7, hivyo kulifanya JWTZ na walinda amani wengine kuwa wasio na mamlaka ya kupambana na waasi moja kwa moja?

Kwa Nini Tanzania Inaonekana Inampiga Tshisekedi Darubini?


Ukiangalia historia, Tanzania imekuwa mshirika wa karibu wa marais wawili wa DRC:


  • Laurent-Désiré Kabila, ambaye alikombolewa kwa msaada wa Tanzania.
  • Joseph Kabila, ambaye pia alifaidika na uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na DRC.

Lakini kwa Tshisekedi, hali inaonekana tofauti. Serikali ya Tanzania inaonekana kumsaidia kwa "machale machale"—yaani, si kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Kabila na Kabila. Kwa nini?


  • Je, ni kwa sababu hakuwa sehemu ya mfumo wa ushawishi wa Tanzania?
  • Au ni kwa sababu alipotwaa madaraka, alikimbilia kushirikiana zaidi na Kenya badala ya Tanzania?
  • Au alidhani waasi wa M23 wangebakia kule kule Goma, bila kujua kuwa nguvu zao zinatoka Kigali na Kampala?

Tanzania inajua kinachoendelea. Watu wetu wa intelligentsia wamekusanya taarifa zote. Lakini inaonekana Tanzania imeamua kuwapotezea kwa sasa—kwa sababu nzuri tu.


Je, JWTZ Itaendelea Kukaushia au Itaingilia Kati?


Historia inaonesha kuwa Tanzania si nchi inayopenda kuona mataifa jirani yanameguka vipande vipande. Tuliwaunga mkono sana Wacongo bila masharti, tukiwapa muda wa kujijenga. Lakini wao wakaleta dharau.


Sasa swali kubwa ni: Tshisekedi atajinasua vipi?


  • Atapiga magoti kwa Tanzania na kuomba msaada?
  • Atazidi kung’ang’ania kwa Kenya na wengine, huku waasi wakiendelea kuikata DRC vipande vipande?

Muda utaamua. Lakini kwa sasa, JWTZ linaendelea na "hamsini zake", likiwa linajua vizuri kwanini halijarudi vitani kama ilivyofanya mwaka 2012-2013. Sababu tunayo, tena inajitosheleza!
Kwa jinsi mambo yanavyoenda huu mgogoro unaweza kujitengenezea sura mpya ambayo inaweza kuwa ngumu zaidi kuliko sasa.

Kwa maana kama watu wameanza kunyoosheana vidole waziwazi basi kuna siku haitakua kunyoosheana vidole tena bali yatakua ni mapigano ya wazi kwasababu mgogoro utakua umehama kutoka kwenye sura ya kisiasa na kwenda kwenye sura ya kiuchumi waziwazi.

Na kutokana na hiyo basi Kila taifa ambalo litakua linaenda kutoa msaada pale Congo litaenda kwa makubalino yanayo lenga maslahi zaidi ya utu (na hiki ndicho ambacho nakiona kimepelekea haya mabadiliko) .

Na kama Kila taifa litaamua kuisaidia Congo kwa mikataba ya maslahi, huenda mgogoro ukaendelea kuwa chanzo cha utata kiasi cha kuvuka mipaka ya kwamba wewe unaingilia himaya yangu utaona, nitakuoneshaaa (hii itakua mbaya zaidi).

Kwahiyo Kila nchi ambayo itashiriki kwenye huu mzozo lazima ihakikishe imechanga karata zake vizuri kwa maana once ukiingia hakutakua na turning back, kwa maana hadi sasa tayari vita imeanza kuwa ya wazi kwa maana kwamba si vita ya Congo na waasi ila ni vita ya Congo na PK.

Kuna uadui unaenda kutengenezwa baina ya mataifa kadhaa ya Africa, na kama ni kweli hii vita ni kwaajiri ya maslahi ya watu fulani basi wenye maslahi sidhani kama wataweza kukubali kirahisi.
 
Vita za misituni si mchezo, Inahitaji watu wa maana sana. Ni muda wa Kila taifa liangalie maslahi yake, muda huu ni muda wa wanafiki wa kupindukia, tuombe kozi Kwa USA au UK watufundishe unafiki wa kiwango cha juu kwasababu drc na Rwanda si marafiki wetu wa kudumu.
 
Si ulisema ulikuwa jeshini wewe au ulikuwa unatupanga??

Au ulikimbia mgambo halafu mnakuja humu kujimwambafai?? Sasa mjeshi gani anaogopa vurugu??!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaa sanaaa. Uwiiiih
 
Hakuna kitu. Pumba tupu. JW zamani sio sasa.... Na Kwa Namna Tunavyomuogopa Kagame Kimbaumbau trust me JW hata pua hawezi kusogeza[emoji16][emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom