Ukimya wa Tanzania na JWTZ Kule Congo DRC si wa Kawaida – Kuna Kitu Kinachezwa?

Kwa anayefuatilia kinachoendelea DRC, hasa katika mkoa wa Goma, atakuwa anajiuliza: Liko wapi lile jeshi jasiri la JWTZ ambalo mwaka 2012-2013 liliwafurusha waasi wa M23 na kuwafanya wasambaratike kabisa?

Kwa mshangao mkubwa, baada ya uchaguzi wa DRC na kuingia madarakani kwa Félix Tshisekedi, waasi wale wale wa M23 wameibuka tena kwa nguvu mpya, wakiwa na uwezo wa kuteka Goma na sasa wakielekea Bukavu. Inaonekana lengo lao ni kuimega DRC, lakini kosa ni la nani?

  • Je, ni Tshisekedi mwenyewe, ambaye kwa sera zake ameshindwa kuimarisha ulinzi wa nchi yake?
  • Au ni MONUSCO, ambalo lilifuta vikosi vya kulinda amani kuwa chini ya Chapter 6 badala ya Chapter 7, hivyo kulifanya JWTZ na walinda amani wengine kuwa wasio na mamlaka ya kupambana na waasi moja kwa moja?

Kwa Nini Tanzania Inaonekana Inampiga Tshisekedi Darubini?

Ukiangalia historia, Tanzania imekuwa mshirika wa karibu wa marais wawili wa DRC:

  • Laurent-Désiré Kabila, ambaye alikombolewa kwa msaada wa Tanzania.
  • Joseph Kabila, ambaye pia alifaidika na uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na DRC.

Lakini kwa Tshisekedi, hali inaonekana tofauti. Serikali ya Tanzania inaonekana kumsaidia kwa "machale machale"—yaani, si kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Kabila na Kabila. Kwa nini?

  • Je, ni kwa sababu hakuwa sehemu ya mfumo wa ushawishi wa Tanzania?
  • Au ni kwa sababu alipotwaa madaraka, alikimbilia kushirikiana zaidi na Kenya badala ya Tanzania?
  • Au alidhani waasi wa M23 wangebakia kule kule Goma, bila kujua kuwa nguvu zao zinatoka Kigali na Kampala?

Tanzania inajua kinachoendelea. Watu wetu wa intelligentsia wamekusanya taarifa zote. Lakini inaonekana Tanzania imeamua kuwapotezea kwa sasa—kwa sababu nzuri tu.

Je, JWTZ Itaendelea Kukaushia au Itaingilia Kati?

Historia inaonesha kuwa Tanzania si nchi inayopenda kuona mataifa jirani yanameguka vipande vipande. Tuliwaunga mkono sana Wacongo bila masharti, tukiwapa muda wa kujijenga. Lakini wao wakaleta dharau.

Sasa swali kubwa ni: Tshisekedi atajinasua vipi?

  • Atapiga magoti kwa Tanzania na kuomba msaada?
  • Atazidi kung’ang’ania kwa Kenya na wengine, huku waasi wakiendelea kuikata DRC vipande vipande?

Muda utaamua. Lakini kwa sasa, JWTZ linaendelea na "hamsini zake", likiwa linajua vizuri kwanini halijarudi vitani kama ilivyofanya mwaka 2012-2013. Sababu tunayo, tena inajitosheleza!
Good
 
JWTZ ikachukue kandarasi Hilo ipige Pesa
Hizo ndizo Kazi zenyewe.

Ndani ya JWTZ kiundwe kikosi kingine cha kushughulikia mambo ya Nje ya mipaka ya Nchi.

Vijana waajiriwe wakapige Kazi. Hela iletwe nchini.
Hayo Mengine ya sifa za kijinga tuachane nayo
Kweli kabisa, enzi za sifa za kijinga zimeisha.
Sasa hivi ni nipe nikupe.
Twende vitani kwa maslahi ya nchi kiuchumi na siyo vinginevyo
 
Si kweli

Jidanganye kaa mkao mzuri kuanzia kesho sikiliza habari vizuri.
inaudwa kikosi ya upepo wa kisurisuri kutoka south africa zimbabwe botswana zambia malawi na waongozaji Tanzania with full military equipments SADC imetoa fungu hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa(Congo)na wanachama wenzake kumuangalia tu.
Dharau za PK kwa Ramaphosa zimewakera marais wote wa SADC sasa mission ni moja tu PK aondolewe madarakani au lah basi achakazwe hadi awe na adabu..
Poleni wanyarwanda mnaenda kuumia sababu ya majivuno ya PK wenu.
Akuna wa kitu kama icho mkuu.
 
CONGO INATIA HURUMA MNO.

TUSIACHE KUWAOMBE NDUGU ZETU HAWANA HATIA.

RASLIMALI ZINAWATESA WAKONGOMANI KIASI HIKI.
WAZUNGU NI WATU WABAYA SANA.
 
Kwa anayefuatilia kinachoendelea DRC, hasa katika mkoa wa Goma, atakuwa anajiuliza: Liko wapi lile jeshi jasiri la JWTZ ambalo mwaka 2012-2013 liliwafurusha waasi wa M23 na kuwafanya wasambaratike kabisa?

Kwa mshangao mkubwa, baada ya uchaguzi wa DRC na kuingia madarakani kwa Félix Tshisekedi, waasi wale wale wa M23 wameibuka tena kwa nguvu mpya, wakiwa na uwezo wa kuteka Goma na sasa wakielekea Bukavu. Inaonekana lengo lao ni kuimega DRC, lakini kosa ni la nani?

  • Je, ni Tshisekedi mwenyewe, ambaye kwa sera zake ameshindwa kuimarisha ulinzi wa nchi yake?
  • Au ni MONUSCO, ambalo lilifuta vikosi vya kulinda amani kuwa chini ya Chapter 6 badala ya Chapter 7, hivyo kulifanya JWTZ na walinda amani wengine kuwa wasio na mamlaka ya kupambana na waasi moja kwa moja?

Kwa Nini Tanzania Inaonekana Inampiga Tshisekedi Darubini?

Ukiangalia historia, Tanzania imekuwa mshirika wa karibu wa marais wawili wa DRC:

  • Laurent-Désiré Kabila, ambaye alikombolewa kwa msaada wa Tanzania.
  • Joseph Kabila, ambaye pia alifaidika na uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na DRC.

Lakini kwa Tshisekedi, hali inaonekana tofauti. Serikali ya Tanzania inaonekana kumsaidia kwa "machale machale"—yaani, si kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Kabila na Kabila. Kwa nini?

  • Je, ni kwa sababu hakuwa sehemu ya mfumo wa ushawishi wa Tanzania?
  • Au ni kwa sababu alipotwaa madaraka, alikimbilia kushirikiana zaidi na Kenya badala ya Tanzania?
  • Au alidhani waasi wa M23 wangebakia kule kule Goma, bila kujua kuwa nguvu zao zinatoka Kigali na Kampala?

Tanzania inajua kinachoendelea. Watu wetu wa intelligentsia wamekusanya taarifa zote. Lakini inaonekana Tanzania imeamua kuwapotezea kwa sasa—kwa sababu nzuri tu.

Je, JWTZ Itaendelea Kukaushia au Itaingilia Kati?

Historia inaonesha kuwa Tanzania si nchi inayopenda kuona mataifa jirani yanameguka vipande vipande. Tuliwaunga mkono sana Wacongo bila masharti, tukiwapa muda wa kujijenga. Lakini wao wakaleta dharau.

Sasa swali kubwa ni: Tshisekedi atajinasua vipi?

  • Atapiga magoti kwa Tanzania na kuomba msaada?
  • Atazidi kung’ang’ania kwa Kenya na wengine, huku waasi wakiendelea kuikata DRC vipande vipande?

Muda utaamua. Lakini kwa sasa, JWTZ linaendelea na "hamsini zake", likiwa linajua vizuri kwanini halijarudi vitani kama ilivyofanya mwaka 2012-2013. Sababu tunayo, tena inajitosheleza!

Nimemsikiliza Kagame kile alichokizungumza kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Nimemsikiliza pia alichoongea na waandishi wa Habari. Sasa nimemuelewa Kagame na I am with him.

Halafu kama hii issue itakuwa inaongelewa kwenye mikutano miwili basi badala ya kuisuluhisha ndiyo waitaiongeza. Hii issue inatakiwa EAC waibebe na SADC ikae pembeni.
 
Bi Tozo hana uelewa wowote na masuala ya geo-politics, waziri wa ulinzi mwenyewe hajui lolote kuhusu masuala ya kivita ma usalama. Siku ile kathibitisha baada ya kubadili darubini mbele nyuma na nyuma mbele halafu yupo busy utasema yupo serious, sasa sijui alikuwa anaona nini, kwa maana darubini ukiigeuza pa kuangalizia unaona taswira ya kitu ipo mbali zaidi...

We imagine mtu darubini hajui kutumia, hivi atakuwa ana uelewa hata na kinachoendelea DRC?

Haya mambo yanahitaji kiongozi mwenye uelewa kwa upana kuhusu migogoro hii na historia zake, tena uelewa kwa undani zaidi, haya masuala yanahitaji intel.

Inahitajika kiongozi mwenye kujua historia za undani kuhusu majirani zake.

Mtu anasikiliza taarabu atajuaje hayo masuala?
Pole kwa kuwa na UONI MFUPI MNO.....
 
Ndhani bwana GEORGE MKUCHIKA atakuwa anajua kila kitu
 
Si kweli

Jidanganye kaa mkao mzuri kuanzia kesho sikiliza habari vizuri.
inaudwa kikosi ya upepo wa kisurisuri kutoka south africa zimbabwe botswana zambia malawi na waongozaji Tanzania with full military equipments SADC imetoa fungu hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa(Congo)na wanachama wenzake kumuangalia tu.
Dharau za PK kwa Ramaphosa zimewakera marais wote wa SADC sasa mission ni moja tu PK aondolewe madarakani au lah basi achakazwe hadi awe na adabu..
Poleni wanyarwanda mnaenda kuumia sababu ya majivuno ya PK wenu.
Niliwaambia kaane mkao mnzuri kuanzia leo jioni mambo yanaanza kuchangamka..
Maazimio ni kwamba hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa na wanachama wenzake wakae kimya lazima majibu yarudishwe kwa nguvu ta 5G na kutoa onyo kali..
Dharau za PK kwa Ramaphosa zitamgharimu sana.
 
Si kweli

Jidanganye kaa mkao mzuri kuanzia kesho sikiliza habari vizuri.
inaudwa kikosi ya upepo wa kisurisuri kutoka south africa zimbabwe botswana zambia malawi na waongozaji Tanzania with full military equipments SADC imetoa fungu hakuna mwanachama wa SADC atavamiwa(Congo)na wanachama wenzake kumuangalia tu.
Dharau za PK kwa Ramaphosa zimewakera marais wote wa SADC sasa mission ni moja tu PK aondolewe madarakani au lah basi achakazwe hadi awe na adabu..
Poleni wanyarwanda mnaenda kuumia sababu ya majivuno ya PK wenu.
Itakuwa jambo jema huyu Kagame ameleta dharau sana Sasa APIGWE
 
Kwa jinsi mambo yanavyoenda huu mgogoro unaweza kujitengenezea sura mpya ambayo inaweza kuwa ngumu zaidi kuliko sasa.

Kwa maana kama watu wameanza kunyoosheana vidole waziwazi basi kuna siku haitakua kunyoosheana vidole tena bali yatakua ni mapigano ya wazi kwasababu mgogoro utakua umehama kutoka kwenye sura ya kisiasa na kwenda kwenye sura ya kiuchumi waziwazi.

Na kutokana na hiyo basi Kila taifa ambalo litakua linaenda kutoa msaada pale Congo litaenda kwa makubalino yanayo lenga maslahi zaidi ya utu (na hiki ndicho ambacho nakiona kimepelekea haya mabadiliko) .

Na kama Kila taifa litaamua kuisaidia Congo kwa mikataba ya maslahi, huenda mgogoro ukaendelea kuwa chanzo cha utata kiasi cha kuvuka mipaka ya kwamba wewe unaingilia himaya yangu utaona, nitakuoneshaaa (hii itakua mbaya zaidi).

Kwahiyo Kila nchi ambayo itashiriki kwenye huu mzozo lazima ihakikishe imechanga karata zake vizuri kwa maana once ukiingia hakutakua na turning back, kwa maana hadi sasa tayari vita imeanza kuwa ya wazi kwa maana kwamba si vita ya Congo na waasi ila ni vita ya Congo na PK.

Kuna uadui unaenda kutengenezwa baina ya mataifa kadhaa ya Africa, na kama ni kweli hii vita ni kwaajiri ya maslahi ya watu fulani basi wenye maslahi sidhani kama wataweza kukubali kirahisi.
KWENYE HII DUNIA NI AIDHA UPIGE AU UPIGWE. KUWA NEUTRAL NI UFALA!!!

📌SOMEONES AMEJISAHAU SASA NI MUDA WA KUMKUMBUSHA KUWA NA MIPAKA!!!
 
Speaking of waziri wa Ulinzi na ile Darubini Dah ni Ametuaibisha sana kwa kweli hii nchi inafaa kuingia The Guinness Book of Records kwa kuongozwa na Mazwazwa kwenye sekta tofauti tofauti
 
Kagame na jeshi lake la m23 wako vizuri kwenye medani na zana za kisasa za kivita kuliko nchi zote za maziwa makuu.

Habari za sijiu nduli Amini alishikishwa adabu hizo ni zilipendwa.
Amewahi kuivamia nchi gani zaidi ya jeshi dhaifu la DRC?
 
KWENYE HII DUNIA NI AIDHA UPIGE AU UPIGWE. KUWA NEUTRAL NI UFALA!!!

📌SOMEONES AMEJISAHAU SASA NI MUDA WA KUMKUMBUSHA KUWA NA MIPAKA!!!
Wacha waadabishane huko wenyewe kwa wenyewe sisi tuendelee kuwa wavumilivu ila ikitubidi kufanya hivyo tutafanya, now hatuna sababu yoyote ya msingi.
 
Kagame ana mtandao ,anaweza agiza vichwa vya nuclear NK , kagame bwana nacheka kama mazuri vile
 
Muda utaamua. Lakini kwa sasa, JWTZ linaendelea na "hamsini zake", likiwa linajua vizuri kwanini halijarudi vitani kama ilivyofanya mwaka 2012-2013. Sababu tunayo, tena inajitosheleza!
JWTZ mbona wapo frontline? Ila M23 wana uzoefu wa vita za guerilla so sio rahisi kupambana nao. Mind you enzi za JPM kuna kambi ya JWTZ ilivamiwa wakauwawa wanajeshi zaidi ya 20!! So JWTZ sio invicible kwamba hawawezi pigwa ni tactics tu hata US na ubabe wake alikwama Somalia!!
 
Kinacho shangaza Kagame anamfokea president wa SA anamwacha jirani yake wa Tanzania 😆
huku hawezi kutufokea ndiko alikopikwa akawa shushu hatari wa mambo ya kivita na vita vya Uganda alishiriki kutusaidia upande wa Inteljesia
 
Back
Top Bottom