Ukimya wa vyombo vya habari juu ya unyama wa wanajeshi dhidi ya raia huko Kawe

Ukimya wa vyombo vya habari juu ya unyama wa wanajeshi dhidi ya raia huko Kawe

Tanzania hakuna vyombo vya habari! Media ndio sector iliyooza na kutia aibu mno. Bora hata enzi za mwalimu ...
 
Bado elimu inahitajika sana kwenye jeshi letu. Jeshi lenye hadhi ya kimataifa halileti picha nzuri kwa upuuzi kama huu.
Na huyu askari wa cheo hicho anawezaje kuzozana na raia hadi kupigana. Mimi nilifikili konstebo kumbe mtu wa rank kubwa halafu anakua mjinga.
Waafrika tunamatatizo sana.
 
Kufuatia tukio lq mauqji ya Luteni Kanali aambaye inasadikiwa alizozana na mwendesha bajaji na kupelekea ugomvi uliogharimu maisha. Imesemwa kuwa mruhumiwa ameshatiwa nguvuni akisubiri sheris kuchukua mkondo wake

kuna vurugu zinaendelea Kawe ambapo baada ya shughuli za kuaga marehemu pale Lugalo, imesemwa vurugu hizo zinafanywa na wanajeshi hususan MP ambapo wwnatembeza kichapo kwa kila raia wanayemkuta. Hawwjali jinsia wala hali.

Je, jeshi ni DPP na Mahakama wakati huo huo? Wananchi wanaopigwa wana mchango upi kwenye tukio ambalo inasemwa marehemu alilianzisha dhidi ya dereva wa bajaji?

Ni lini wananchi watqthibitishiwa amani ndani ya nchi yao?

View attachment 2795689

View attachment 2795690

picha hizi zinapatikana mtandao wa X kwa mtumiaji aitwaye Fortunatus Buyobe

Vyombo vyetu vya habari kama havipo ila wanaendekeza sana habari za udaku na ujinga wa kila namna. Hata kama imetokea hayo wengine hawahusiki na hayo wanayotendewa,hii nchi inaendeshwa kwa mjibu wa Katiba na sheria,watu waishi kwaku heshimiana ili Amani idumu.

Media House za Tanzania kwa kiwango kikubwa imekuwa ikifumbia macho matukio hasi yanayofanywa na serikali na vyombo vyake dhidi ya raia. Tumeona waandishi wengi wakipata teuzi ambazo ni kama rushwa za kisiasa.


RAI
Naliomba Jeshi (JWTZ) kutoa tamko la kurekebisha huu mtanziko unaoendelea. Jeshi linalopendwa na raia haliwezi hata mara moja likawadhuru raia.


inawezekaba likaona kuomba radhi ni kujishusha, basi likemee ama lizuie askari wake kushiriki matendo yanayoumiza ama kuwaletea raia tafran

Tunashukuru JamiiForums kutupatia jukwaa la kuzungumza kwa uwazi

Tuamke
Tuzinduke
Tuiponye Tanzania
Polisi Tanzania Wana wajibu pia kuchukua hatua Kwa wote wavunja sheria maana hakuna aliye juu ya sheria.
 
Kama ni kawe wacha wapigwe tuuuu

Wamewahi kuua Binti wa Askari kwa mapanga hawakufanywa kitu

Wacha kiwarambe This time
 
Haiwezekani Luteni wa Jeshi auawe mambo yapite hivi hivi..usalama wenu ni kuwataja wote waliohusika mara moja .kichapo kipo pale pale.
 
Back
Top Bottom