Ukimzidi mshindani wako kwa 90%, kutakuwa na sababu mbili za wewe kushinda...

Ukimzidi mshindani wako kwa 90%, kutakuwa na sababu mbili za wewe kushinda...

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Ukimzidi mshindani wako kwa asilimia 90% kutakua na sababu kubwa mbili za wewe kuupata ushindi huo.

1. Uwezo wa mshindani wako katika mnachoshindania ulikua duni sana. Hili hata walimu huwa wanajitahidi kutunga mitihani yao kutokana na uwezo wa wengi darasani. Nusu ya darasa wakipata 90% basi inamaana mtihani ulikua rahisi sana. Sasa ukimzidi mshindani wako kwa 90% angalia mchakato mzima wa kumpata mshindi ulikuwaje?

2. Mshindani wako ulimminya kiasi cha kukosa nguvu kabisa katika shindano. Ni sawa na kuwa ulishindana na maiti isiyo na uwezo wa kujitetea. Katika hali hii kulikuwa na haja ya kuwa na shindano?
 
Na wapinzani wajiandae kiakili ni kesi juu ya kesi uzuri bwana yule anajua kulipiza kisasi.

Ila naomba ifike hatua wananchi tukaanza baguana kivyama kauli kama si ulichagua fulani
 
Teh teh, tulianza na TWENDE NA MEMBE, upepo ukamgeuka ikaja NI YEYE! The thing is, upinzani na watu wake huwa hamjitambui, hamuangalii nyakati tulizo nazo. Without a free NEC and other institutions, bila kumpunguzia madaraka raisi, kizazi chetu kitapita bila kuona upinzani kuongoza dola.
 
Wenzako washaanza kujipanga kwa ajili ya 2025 🤣.

Hawa watu akili zao wanazijua wenyewe.

And let me guess, Shangazi 2025 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom