Ukinunua simu online (Mfano Ebay au AliExpress) kuipata ni bahati nasibu

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kwema wakuu.

Siku hizi ukinunua simu/smartphone online mfano kutoka China AliExpress au Ebay n.k aisee kuipata ni kubet.

Zoezi zima la kununua litaenda vizuri, itatumwa, utaitrack, tatizo itakavyofika Tanzania.

Aisee sijui ni Airport au Posta wanapiga. Tracking inaishia “item has arrived in destination country “ baada ya hapo mazima.

Ilivyonitokea mara mbili nikajua labda muuzaji magumashi ila ilivyojirudia tena mara 4 mwezi wa 12 hadi january nikahisi kitu. Nikawauliza baadhi ya watu wakasema inaibiwa sana izo small packages, ila hawajui ni Airport au posta.

Zinazofika ni zile ambazo nje zimeandikwa “Electronic device” au jina jingine ila ikiandikwa “Smartphone” wajomba wanatambaa nazo. Akipata simu zake 10 kwa mwezi amepata CIF ya Crown.

Watu wanatamaa sana na hii inasababisha wauzaji wengi wasiuze/ship vitu vyao kuja hizi nchi za masikini, maana ni hasara wanavyodaiwa dispute.

Mamlaka husika chunguzeni ilo.
 
Bora ebay mkuu usijekujaribu kikuu, utapigwa na kitu kizito. Nilishaagiza iphone na beg la laptop bikafika ndani ya week tatu na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuagiza kupitia kikuu.

Kuna mtu flani akaniomba nimuagizie iphone kama yangu, daah! Nilijihis ataniona tapeli. Walinitumia meseji eti mizigo umekamatwa Adis Ababa kwaajili ya clearance. Wakaniomba nivumilie lakini mwisho wakanirudishia hela. Nikaagiza tena ikachukua mwez na week mbili ikafika.

Mwaka jana tena nikaagiza iphone ya ndugu yangu, hii ni hadi niliwatukana huduma kwa wateja. Simu ilipotea mara tatu. Mara ya kwanza ilitumia mwez na week nikawa refunded, sababu ni mzigo umepotea. Nikaagiza tena mwezi na week 1 nikawa refunded tena, duuh. Nikaagiza mara ya tatu, ilitumia mwezi na week tatu nikapewa ujumbe mzigo umepotea. Niliwatukana huduma kwa wateja nikawaomba waitoe hela, wakaniomba namba ya tigo pesa nikawapa. Sijawahi rudia tena
 
Mimi kwa uzeofu wangu ebay ndo miyeyusho vitu vichache sana ndonvilifikaga ila Aliexpress wao vitu hua vinachelewa na nikiona miyeyusho naomba refund hela inarudi..yani kama ni utapeli ningewatapeli sana hawa Aliexpress..maana vitu navipata kabisa lakini vinasoma havijafika....🤣🤣🤣
 
Nilishakutana na mchezo huo ambapo niliagiza 1 Teller GB External H Drive moja nilitumia elfu 28
Kwenye system ikaonyesha mzigo umefika kwenye country of destination.
Nikaenda posta dsm nikapanda juu first floor ofisini posta hq dsm nikaeleza shida yangu nikaambiwa ninuone mama mmoja mtu mzima kidogo , nikafika nikamweleza ishu yangu nikampatia reference code zangu .
Kwanza alikuwa busy akaniambia nisubiri nikakaa sana kwenye viti vyao vile vya kusubiria vya kama aluminium hivi vilivyounganishwa .
Baadae akaniita akanieleza kwamba mzigo wangu haujafika.
Nikamwambia naomba niprintie hiyo document inayoonyesha kwamba mzigo haujafika ili niwatumie Alibaba wanirefund fedha yangu.
Yule mama alinijibu printa haina wino nikashangaa sana, nikamuomba nitumie kwenye email yangu basi ili nikaprint mwenyewe akanijibu taratibu haziruhusu yeye kutuma email nje nikamwambia nije lini printer itakuwa na wino akanijibu hajui watu wa stoo watampatia lini wino kwani ni muda printer yake haina wino mwisho nikamuomba anionyeshe basi niangalie hiyo taarifa inayoonyesha mzigo wangu haujafika akaniambia taratibu haziruhusu eti naweza ona siri nyingine za ofisi.
Dah nilikasirika halaafu nilikuwa na mtu ananisubiri nje tukafanye ishu nyingine bank na muda ulikuwa umekwenda
Ikabidi niondoke zangu.
Nikaingia alilibaba kudai wanirefund wakanidai document ya kuonyesha mzigo haujafika ndani ya siku 14 niwatumie wanirefund.
nikaja kusafiri nikarudi baada ya mwezi ila kwa kweli posta jirekebisheni kwa huduma zenu.
sio kwa huduma zenu mbovu mlizonionyesha.
 
Kwema wakuu.

Siku hizi ukinunua simu/smartphone online mfano kutoka China AliExpress au Ebay n.k aisee kuipata ni kubet.

Zoezi zima la kununua litaenda vizuri, itatumwa, utaitrack, tatizo itakavyofika Tanzania.

Aisee sijui ni Airport au Posta wanapiga. Tracking inaishia “item has arrived in destination country “ baada ya hapo mazima.

Ilivyonitokea mara mbili nikajua labda muuzaji magumashi ila ilivyojirudia tena mara 4 mwezi wa 12 hadi january nikahisi kitu. Nikawauliza baadhi ya watu wakasema inaibiwa sana izo small packages, ila hawajui ni Airport au posta.

Zinazofika ni zile ambazo nje zimeandikwa “Electronic device” au jina jingine ila ikiandikwa “Smartphone” wajomba wanatambaa nazo. Akipata simu zake 10 kwa mwezi amepata CIF ya Crown.

Watu wanatamaa sana na hii inasababisha wauzaji wengi wasiuze/ship vitu vyao kuja hizi nchi za masikini, maana ni hasara wanavyodaiwa dispute.

Mamlaka husika chunguzeni ilo.
Aisee izo small package kweli posta zina potea sanaa, mm ni mhanga

Nahisi kuna kamchezo tuna fanyiwa ili ku discourage uagizaji wa bidhaa kupitia hii mitandao, coz posta siku izi na wao wana duka lao online, embu tujaribu ku shop kwao tuone kama vita potea pia
 
Nilishakutana na mchezo huo ambapo niliagiza 1 Teller GB External H Drive moja nilitumia elfu 28
Kwenye system ikaonyesha mzigo umefika kwenye country of destination.
Nikaenda posta dsm nikapanda juu first floor ofisini posta hq dsm nikaeleza shida yangu nikaambiwa ninuone mama mmoja mtu mzima kidogo , nikafika nikamweleza ishu yangu nikampatia reference code zangu .
Kwanza alikuwa busy akaniambia nisubiri nikakaa sana kwenye viti vyao vile vya kusubiria vya kama aluminium hivi vilivyounganishwa .
Baadae akaniita akanieleza kwamba mzigo wangu haujafika.
Nikamwambia naomba niprintie hiyo document inayoonyesha kwamba mzigo haujafika ili niwatumie Alibaba wanirefund fedha yangu.
Yule mama alinijibu printa haina wino nikashangaa sana, nikamuomba nitumie kwenye email yangu basi ili nikaprint mwenyewe akanijibu taratibu haziruhusu yeye kutuma email nje nikamwambia nije lini printer itakuwa na wino akanijibu hajui watu wa stoo watampatia lini wino kwani ni muda printer yake haina wino mwisho nikamuomba anionyeshe basi niangalie hiyo taarifa inayoonyesha mzigo wangu haujafika akaniambia taratibu haziruhusu eti naweza ona siri nyingine za ofisi.
Dah nilikasirika halaafu nilikuwa na mtu ananisubiri nje tukafanye ishu nyingine bank na muda ulikuwa umekwenda
Ikabidi niondoke zangu.
Nikaingia alilibaba kudai wanirefund wakanidai document ya kuonyesha mzigo haujafika ndani ya siku 14 niwatumie wanirefund.
nikaja kusafiri nikarudi baada ya mwezi ila kwa kweli posta jirekebisheni kwa huduma zenu.
sio kwa huduma zenu mbovu mlizonionyesha.
Vipi kampuni zingine je mfano DHL,UPS,TNT yaani wasio link na posta
 
Back
Top Bottom