Ukinunua simu online (Mfano Ebay au AliExpress) kuipata ni bahati nasibu

Ukinunua simu online (Mfano Ebay au AliExpress) kuipata ni bahati nasibu

Bora ebay mkuu usijekujaribu kikuu, utapigwa na kitu kizito. Nilishaagiza iphone na beg la laptop bikafika ndani ya week tatu na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuagiza kupitia kikuu.

Kuna mtu flani akaniomba nimuagizie iphone kama yangu, daah! Nilijihis ataniona tapeli. Walinitumia meseji eti mizigo umekamatwa Adis Ababa kwaajili ya clearance. Wakaniomba nivumilie lakini mwisho wakanirudishia hela. Nikaagiza tena ikachukua mwez na week mbili ikafika.

Mwaka jana tena nikaagiza iphone ya ndugu yangu, hii ni hadi niliwatukana huduma kwa wateja. Simu ilipotea mara tatu. Mara ya kwanza ilitumia mwez na week nikawa refunded, sababu ni mzigo umepotea. Nikaagiza tena mwezi na week 1 nikawa refunded tena, duuh. Nikaagiza mara ya tatu, ilitumia mwezi na week tatu nikapewa ujumbe mzigo umepotea. Niliwatukana huduma kwa wateja nikawaomba waitoe hela, wakaniomba namba ya tigo pesa nikawapa. Sijawahi rudia tena


Aieone ERoni
 
Ushauri: agizeni mizigo yenu kupitia Fedex, DHL, Aramex....achaneni na posta...
Hizi kampuni zipo miji mikubwa pekee.watu wanafata urahisi posta.Vitu vidogo vya thamani bora utumie kampuni hizi.vile vikubwa thamani unaijua wewe pekee unatumia posta.
 
Haiwezekani Kufuatilia Wezi hao?
Wanalindana. Utakuta gharama za kufuatilia ni kubwa kuliko walichoiba. Mfano mtu upo mkoani umeagiza simu ya laki1 inapotelea posta makao makuu Dar. Utapanda bus kuja Dar kuhangaika nao?
 
Njia nyingine nikupitia mawakala km dhl wapo juu. .kuna agents wavitu toka nje ya nchi. .UK. .us na hasa China. ..ww unalipia kwa agent moja kwa moja na si through posta
 
Back
Top Bottom