Ukinunua simu online (Mfano Ebay au AliExpress) kuipata ni bahati nasibu

Hapo kwanza tupeleke malalamiko yetu posta moja kwa moja ikiwezekana kwa wizara husika bila kusahau kamati za ulinzi na usalama

Pia kwa kuwa mitandao ina nguvu sana watu wooote tukipaza sauti zetu humu jf, facebook, tweeter, instagram nk wahusika watasikia na wataona kweli Watu wamechachamaa katika hilo.
 
Shirika limejaa wazee unatarajia nini???
Nilishakutana na mchezo huo ambapo niliagiza 1 Teller GB External H Drive moja nilitumia elfu 28
Kwenye system ikaonyesha mzigo umefika kwenye country of destination.
Nikaenda posta dsm nikapanda juu first floor ofisini posta hq dsm nikaeleza shida yangu nikaambiwa ninuone mama mmoja mtu mzima kidogo , nikafika nikamweleza ishu yangu nikampatia reference code zangu .
Kwanza alikuwa busy akaniambia nisubiri nikakaa sana kwenye viti vyao vile vya kusubiria vya kama aluminium hivi vilivyounganishwa .
Baadae akaniita akanieleza kwamba mzigo wangu haujafika.
Nikamwambia naomba niprintie hiyo document inayoonyesha kwamba mzigo haujafika ili niwatumie Alibaba wanirefund fedha yangu.
Yule mama alinijibu printa haina wino nikashangaa sana, nikamuomba nitumie kwenye email yangu basi ili nikaprint mwenyewe akanijibu taratibu haziruhusu yeye kutuma email nje nikamwambia nije lini printer itakuwa na wino akanijibu hajui watu wa stoo watampatia lini wino kwani ni muda printer yake haina wino mwisho nikamuomba anionyeshe basi niangalie hiyo taarifa inayoonyesha mzigo wangu haujafika akaniambia taratibu haziruhusu eti naweza ona siri nyingine za ofisi.
Dah nilikasirika halaafu nilikuwa na mtu ananisubiri nje tukafanye ishu nyingine bank na muda ulikuwa umekwenda
Ikabidi niondoke zangu.
Nikaingia alilibaba kudai wanirefund wakanidai document ya kuonyesha mzigo haujafika ndani ya siku 14 niwatumie wanirefund.
nikaja kusafiri nikarudi baada ya mwezi ila kwa kweli posta jirekebisheni kwa huduma zenu.
sio kwa huduma zenu mbovu mlizonionyesha.
 
hata watumishi wake ni waajabu sana nakumbuka nilishasoma story yao moja ya ajabu sana kwamba junior officer (security officer) alipandikiza kiasi cha bangi kwenye parcel ya CEO wa hilo shirika sijui alifanya usiku, kesho yake watu wengine wa security walipokagua hiyo parcel wakagundua kuna kiasi cha gramu kadhaa za bangi so ikabidi huyo boss awe aswerable ilikuwa mshikemshike kwenye taasisi ikabidi bosi akapimwe mkojo kama anatumia bangi ikaonekana hatumii,ukafanyika uchunguzi mkali ndipo ikabainika kwamba hiyo bangi ilifanywa kuchomekwa kwenye mzigo wa bosi hapohapo ofisini kwao huyo jamaa alipogundua amegundulika akakimbia akafukuzwa kazi on absentee.
Just imagine mtu anafungua parcel ya bosi wake na kuweka bangi mtu huyoatashindwaje kuiba parcel za wateja
 
Hii inanikumbusha rafiki yangu alikuaa kwenye taasisi moja inayosomesha watoto inayodhaminiwa na wamarekani, ilitumwa cheque kufika posta walichana wakaenda nayo bank wakafeli kuiba hela maana pamoja na uwepo wa sahihi ya mdhamini ilikua inahitaji sahihi ya rafiki yangu pamoja na muhuri anaokaa nao rafiki yangu, POSTA HQ WEZI SANA
 
Posta wazembe sana ...wangepata viongozi na wafanyakazi makini wangepiga hela sana kwenye shipping ya online. Watanzania wengi sana wanatamani kununua vitu online ila wanasita kwa sababu ya posta.
 
Washaurini alibaba wafungue ofisi zao Tza wawe na delivery center yao Tza. Wawe na magodown tza, mwenye link yao anipe niwape wazo hilo. Wachina wapo speed Sana kurespond
Sidhani kama wanabiashara kubwa kihivyo hadi wafungue na ofisi
 
Hapa ndipo wanatanzania tunafanya makosa kwa kulea upuzi na wajinga....ulipaswa kwenda kwa mabosi wao, ikiwezekana mpaka kwa Waziri na mahakamani kabisa..... mkifanya hizi watu 10 watakuwa na adabu kidogo
 
Washaurini alibaba wafungue ofisi zao Tza wawe na delivery center yao Tza. Wawe na magodown tza, mwenye link yao anipe niwape wazo hilo. Wachina wapo speed Sana kurespond

Ni idea nzuri, unaweza kuomba kuwa agent wao kwa delivery zote kuzifanyia kwako...
 
hata watumishi wake ni waajabu sana nakumbuka nilishasoma story yao moja ya ajabu sana kwamba junior officer (security officer) alipandikiza kiasi cha bangi kwenye parcel ya CEO wa hilo shirika sijui alifanya usiku, kesho yake watu wengine wa security walipokagua hiyo parcel wakagundua kuna kiasi cha gramu kadhaa za bangi so ikabidi huyo boss awe aswerable ilikuwa mshikemshike kwenye taasisi ikabidi bosi akapimwe mkojo kama anatumia bangi ikaonekana hatumii,ukafanyika uchunguzi mkali ndipo ikabainika kwamba hiyo bangi ilifanywa kuchomekwa kwenye mzigo wa bosi hapohapo ofisini kwao huyo jamaa alipogundua amegundulika akakimbia akafukuzwa kazi on absentee.
Just imagine mtu anafungua parcel ya bosi wake na kuweka bangi mtu huyoatashindwaje kuiba parcel za wateja
Khaaaa

Wanahitaji wapitiwe upya kwa kweli!!!!
 
Hii inanikumbusha rafiki yangu alikuaa kwenye taasisi moja inayosomesha watoto inayodhaminiwa na wamarekani, ilitumwa cheque kufika posta walichana wakaenda nayo bank wakafeli kuiba hela maana pamoja na uwepo wa sahihi ya mdhamini ilikua inahitaji sahihi ya rafiki yangu pamoja na muhuri anaokaa nao rafiki yangu, POSTA HQ WEZI SANA
Duh!!!
 
Kwema wakuu.

Siku hizi ukinunua simu/smartphone online mfano kutoka China AliExpress au Ebay n.k aisee kuipata ni kubet.

Zoezi zima la kununua litaenda vizuri, itatumwa, utaitrack, tatizo itakavyofika Tanzania.

Aisee sijui ni Airport au Posta wanapiga. Tracking inaishia “item has arrived in destination country “ baada ya hapo mazima.

Ilivyonitokea mara mbili nikajua labda muuzaji magumashi ila ilivyojirudia tena mara 4 mwezi wa 12 hadi january nikahisi kitu. Nikawauliza baadhi ya watu wakasema inaibiwa sana izo small packages, ila hawajui ni Airport au posta.

Zinazofika ni zile ambazo nje zimeandikwa “Electronic device” au jina jingine ila ikiandikwa “Smartphone” wajomba wanatambaa nazo. Akipata simu zake 10 kwa mwezi amepata CIF ya Crown.

Watu wanatamaa sana na hii inasababisha wauzaji wengi wasiuze/ship vitu vyao kuja hizi nchi za masikini, maana ni hasara wanavyodaiwa dispute.

Mamlaka husika chunguzeni ilo.
Ndiyo maana hata zoezi la anuani za makazi ni bure tu! Ni kuimarisha polisi's surveillance on citizens, in a 'police state'.
 
Kila aliebiwa mzogo wake na posta aufungulie uzi wake, malalamiko yakiwa mengi humu jukwaani ni lazima tu watashughulikiwa, haiwezekani serikali itoe pesa nyingi kulifufua hili shirika halafu viongozi wa hilo shirika ndio wawe wa kwanza kulihujumu.
 
Si Wana office Dar nadhani wanajua changamoto au kwenda kuwaripotia office kwao

Screenshot_20220210_220350.jpg

Screenshot_20220210_220408.jpg
 
Posta wazembe sana ...wangepata viongozi na wafanyakazi makini wangepiga hela sana kwenye shipping ya online. Watanzania wengi sana wanatamani kununua vitu online ila wanasita kwa sababu ya posta.
Ila nchi yetu imejaa uozo sana na wafanyakazi mambumbumbu

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom