Ukiona mfanyakazi anamiliki vitu havilingani na mshahara wake hiyo ni Red flag

Ukiona mfanyakazi anamiliki vitu havilingani na mshahara wake hiyo ni Red flag

Ukiona kiongozi ananeemeka halafu watu wake wa chini hawana hili wala lile, huyo hapaswi kuwa kiongozi.

Kiongozi mzuri ni yule anayefurahia mafanikio na furaha ya watu wake.
Atafanya kila aliwezalo ili kila aliye chini yake anyenyuke kiuchumi.

Kuna watu wana roho mbaya, mfanyakazi wake akipendeza tu ni tatizo, achana na kumiliki gari zuri.
 
Kuna jamaa alizindua nyumba yake ya gorofa moja akaalika marafiki wa kazini mwezi uliofata akafanyia bonge la audit na kuachishwa kazi
 
Kuna jamaa alizindua nyumba yake ya gorofa moja akaalika marafiki wa kazini mwezi uliofata akafanyia bonge la audit na kuachishwa kazi
Watu hawaelewi ila watu unaofanya nao kazi hawapaswi kujua mambo yako. Kutaneni kazini au baa achaneni huko huko. Mimi ni Nina kijumba Cha kuzugia kabisa siku kama naumwa au Nina tatizo wanakuja kuniona hapo na wanajua ndio kwangu.

Nilikajenga maalum Kwa ajili ya kazi hiyo. Kilichofuata jamaa wananidharau na kunipuuzia wakati wangejua namiliki ukwasi wa mabillion
 
Kwahiyo wewe unataka mfanyakazi wako aishi kwa kutegemea mshahara wako peke yake? Maboss wengine akili hamnaga kabisa
 
Kama kazi anatimiza na hupati hasara ubaya uko wapi hapo?
 
Ukiona mfanyakazi wako anamiliki vitu havilingani na mshahara unaomlipa lazima upate wac wac , mfano haiingii akilini kwa mtu anayelipwa laki 3 halafu ananunua Gari la milioni 60 , au anaishi maisha yanayozidi mshahara wake . Waajiri kuweni makini hizo ni Red flag za kupigwa
mhn! naogopa nikikambia kuwa unaishi kizamani utachukia! lakini ndio hivyo.
wakati huo mshahara ndio ulikuwa chanzo pekee kwa mfanyakazi kuishi na kiukweli kulingana na mahitaji ya wakati huo alikuwa anaweza kumudu maisha yake ya kawaida.
lakini kwa sasa mambo ni tofauti mshahara ni moja ya chanzo cha mapato. mfano mtu akiwa na mshahara anaweza kumudu kujiunga na VICOBA na kuweza kukopa zaidi ya 3,000,000 akawekeza kwenye biashara nyingine inayoweza kumwakikishia pato la shilingi 20,000 kwa siku sawa na laki sita kwa mwezi bado hajauza supu na chakula ambayo tufanye kwa siku inaleta 10,000 sawa na 300,000
chanzo kingine inawezekana familia imeuza mali ya urithi kama nyumba akapata mgao wa 150m sasa kwanini asinunue gari?
viko vyanzo vingi zaidi ya kipato zaidi ya wizi
 
Ushakariri kila mtu anaishi kwa kutegemea mshahara tu.

Kuna watu pamoja na ajira wana side hustles zao zinazolipa vizuri, kuna wanaotokea familia bora ambao pamoja na ajira zao bado wanpewa ziada.

Ikiwa huna losses zozote kwenye kampuni yako, hupaswi kujali nini anamiliki mfanyakazi wako. kutoweza kwako kuishi/kumiliki vizuri kusiwe sababu ya kuweka ghilba kwa wengine.
Kuna mfanyakazi mmoja wa mshahara kama aliyosema huyo mnoko mwaka jana alinunua used horse+ tela (kichanga) kwa zaidi ya 100m; asee alichunguzwa balaa; ikafahanika alipata mgao kwenyeurithi.
Jamaa mwingine mwaka juzi aliwekewa 50m kwa anaunti, asee NMB (kupitia FIU) walimsakama, wanajua kuwa ameuza ardhi, TRA wakaliunga wakitaka Kodi ya Ongezeko la Thamani; baadaye wakamwacha.
Ukiwa raia mwema, wakapona unakaribia kutoboa unasakamwa; Ila wezi + mafisadi wanavyonza mvinyo kwenye casino.
 
Wazee wangu wanasimulia kuwa miaka ya 80 waliweza kununua land rover 2 kutokana na biashara halali, ila hata kununua baiskeli hawakuthubutu kwa kuwa wangeishia korokoroni.
Hicho ni kipindi chini ya miaka 50 iliyopita. Umaskini na kiduwaa kwa Watanzania una mizizi ya muda mrefu
 
Watumishi wengi wa umma ni wezi,hela wanapata kimagumashi

Anyway nchi hii ukipata upenyo we piga tu nasema we pigaaa tuu

Ila cheza kwa step tu

Ova
 
Watumishi wengi wa umma ni wezi,hela wanapata kimagumashi

Anyway nchi hii ukipata upenyo we piga tu nasema we pigaaa tuu

Ila cheza kwa step tu

Ova
Usiwafundishe watu tabia mbaya , kuwa mzalendo
 
Watu wanakopa Jamani,au wana ndugu zao wanawasaidia, nafanya kazi ya Pesa ndogo lakini wazazi wananipa Gari na pesa. Nakataaje?
Vipi gari yako Leo umewekea mafuta kweli mamy? Ebu njoo inbox nkutumie hela ya mafuta
 
Back
Top Bottom