mhn! naogopa nikikambia kuwa unaishi kizamani utachukia! lakini ndio hivyo.
wakati huo mshahara ndio ulikuwa chanzo pekee kwa mfanyakazi kuishi na kiukweli kulingana na mahitaji ya wakati huo alikuwa anaweza kumudu maisha yake ya kawaida.
lakini kwa sasa mambo ni tofauti mshahara ni moja ya chanzo cha mapato. mfano mtu akiwa na mshahara anaweza kumudu kujiunga na VICOBA na kuweza kukopa zaidi ya 3,000,000 akawekeza kwenye biashara nyingine inayoweza kumwakikishia pato la shilingi 20,000 kwa siku sawa na laki sita kwa mwezi bado hajauza supu na chakula ambayo tufanye kwa siku inaleta 10,000 sawa na 300,000
chanzo kingine inawezekana familia imeuza mali ya urithi kama nyumba akapata mgao wa 150m sasa kwanini asinunue gari?
viko vyanzo vingi zaidi ya kipato zaidi ya wizi