Ukiona mfanyakazi anamiliki vitu havilingani na mshahara wake hiyo ni Red flag

Masanja yupo efm lakini naendesha mav8 nae Huyu vipi? Ya gharama kuliko boss wake majizo
 
Kabla yakumuwekea reg flag mfanyakazi wako kwanza jiulize ofisi yako inaweza kuibiwa hiyo million 60 ukute thamani ya ofcn yote ni 30 million tu.
 
Kama na biashara au kilimo ila kazi anapata ujuzi na ni kwa sababu zingine huyo nae utasemaje?
 
Nyie wachangiaji kwa kweli mmenitia moyo sana nilikuwa nawaza jinsi ya kwenda na hili gari langu kazini ...sasa majibu ya kumpa boss akileta maneno ninayo.
Mmenifariji sana .
Kazi iendelee
 
Mshahara laki3 , Gari ya milioni60...!!🙄🙄

Kumbe ukikljitahidi sana unaweza ukaubeba mlima Kilimanjaro 😂!
 
SIO KWELI Mkuu.
Nilikuwa na mshahara wa Tsh 35,000/= miakq 20 iliyopita na ulitosha kufanya maendeleo. Hata tukipokea lak 3 sasa hivi mimi na wewe. Mimi utatosha na nitafanya la kufanya kupitia hiyo laki 3 mkuu.
Sio kila mwenye mshahara mdogo ni mwizi hapana. Unapokea laki 3 umepanga,una mke na watoto ,una mchepuko, una watoto kibao unadaiwa matumizi hiyo haita kutosha.!
 
Hili ni tatizio la kurithi jina la ukoo pekee, wengine wanatoka familia zinazojiweza, hivyo wanarithi na mali pia. Ila kusudi uweze kufaulu darasani nadharia yako ni sahihi kwani ndivyo ulivyofundishwa.
 
Mbona mke wangu namuachia afu tatu na kila siku tunakula wali kuku? Acha unoko.
 
Hizo ni redflag lakini hazimaanishi kwamba ni upigaji 100% na inategemeana na mtu husika , mimi nilianza ajira huku napiga mishe mishe zingine , so nilikuwa naweza tumia zaidi ya my salary sometimes.

Ofisi niliopo kuna watu mishahara yao ni ya kawaida ila wanamagari ya mil 80, 90, 120 na nikawaida kabisa maana wanabackup za issue zingine sio salary tu mzee.

labda uzungumzie ofisi za umma ambapo ndio kunakuwa na fraud sanasana.
 
Kuna jamaa alizindua nyumba yake ya gorofa moja akaalika marafiki wa kazini mwezi uliofata akafanyia bonge la audit na kuachishwa kazi
Labda walimuonea wivu tu wenzake ,maana kama angekuwa mwizi asingealika wafanyakazi wenzake. Ghorofa moja sasa ndugu si hata mil 150 mtu ananyanyua? kama karithi?,kauza kiwanja? kakopa ?

Kaka alikuwa mwizi basi ni mjinga kabisa
 
Yaani una ukwasi wa mabilioni halafu unaishi kama digidigi kisa ajira ambayo haikupi hata kipato cha kujenga nyumba ya maana bila kuonekana mwizi?
Jamani mnapotunga hizi stori muwe mnapima uhalisia.
 
Yaani una ukwasi wa mabilioni halafu unaishi kama digidigi kisa ajira ambayo haikupi hata kipato cha kujenga nyumba ya maana bila kuonekana mwizi?
Jamani mnapotunga hizi stori muwe mnapima uhalisia.
Mwamba umechanganua umeshtuka story ni ya kupangwa
 
Yaani una ukwasi wa mabilioni halafu unaishi kama digidigi kisa ajira ambayo haikupi hata kipato cha kujenga nyumba ya maana bila kuonekana mwizi?
Jamani mnapotunga hizi stori muwe mnapima uhalisia.
Ukwasi wa mabilioni? hao wanaokuja kukuona lazima watakuwa kwao nyumba sio issue ,so jamaa anatupiga fix
 
😄😄😄Yaani wewe ukiwa ni boss sehemu fulani utateseka sana Kwa mentality yako ya namna hii.
Fungua ubongo vizuri mzee.
 
Hii philosophy ni kufikiri kimaskini. Hili nilikuja kulitambua baada ya jamaa mmoja tuliye ajiriwa naye, alikuwa na maisha ya kawaida kabisa ya kupanda Daladala na wakati mwingine alikuwa anaweza kukupiga kibomu cha fifty au zaidi. Ila hakuwa mzulumati. Akikopa anarudisha mwisho wa Mwezi.

Baadae akawa amefiwa na mzazi. Issue za Mirathi hazikukawia, watoto wakagawana Mali na mkwanja. Yeye akabahatika kupata 280m. Halafu bado akaendelea kubakia Low Key.

Sasa mtu kama huyo akija kuomba kazi kwako, leo na kesho ukamuona ana drive Anaconda au Subaru X-Brake, utaanza kumfuatilia !?

Binafsi nashauri tuache kufikiri kizamani.
 
Na ukiona mtu ana frame kubwa pale sinza alafu ndani ya hiyo fremu kaning'iniza vinguo viwili tu, huku nje kapaki V8 kali/Sport car hiyo ni redflag.
 
Duh kila mtu na mbinu zake za kimaisha
 
Watanzania wengi ni very sadist. Ona huu uzi.
Wabongo wengi ni wapigaji sasa hapa wanapeana sapoti za kijinga. kuna jamaa namfaham alikuwa mshkaji tu tupo naye kijiweni siku zote mara akapata kazi sehem flani. siku iyo ghafla kanicheki anataka kuanzisha kiprojekti chake cha milioni 10 nikajua uku tyr kumekucha. mara naskia kafukuzwa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…