Ukiona ndugu na watu wanamdharau Mkeo ujue wewe mwenyewe Wanakudharau

Ukiona ndugu na watu wanamdharau Mkeo ujue wewe mwenyewe Wanakudharau

Ndo hivyo kwa ajili ya convince ya watoto unaamua tu kulisukuma, utakuta mwanamke hapendi kuona ndugu wa mume au anawagombanisha! Hapo umekuja kujua her true colours baada ya kuoa? Utafanya nini na vitoto viwili au vitatu ndo hata primary hawajaanza?

Hata wangekuwa watoto sita mwanamke akikosa sifa ya kuwa mke unastahili kumuacha mara moja
 
Hoja yako ni ipi. Hilo tuu ndio watu watalihitaji kabla hujaondoka.


Mahusiano sio Kazi ili mtu ahitaji uzoefu.

Ndio maana mwanaume mwenye miaka ishirini ndoani Muda wowote ndoa inaweza kumshinda licha ya kukaa Muda mrefu na huyo mwanamke na akamshindwa huyo mwanamke lakini akaja kijana mdogo akamtuliza huyo mwanamke aliyeshindikana kwa huyo mbaba(mwanaume) mwenye umri Mkubwa.
Baada ya kumtuliza na yeye akakaa na miaka 20 eti??
 
EXactly, kuna time unajikuta unaishi tena saa zingine unabembeleza kuishi na mtu ambaye unajua kabisa hakupend wala hakuhitaji but just kwakua umeshafika hatua ambayo hutaki tena kurud nyumba kuanza upya usije ukasababisha madhara zaidi.. like huo mfano hapo, umeshazaa watoto na hupend kuona watoto wanapata shida kwa kuoa mwanamke mwingine

Upendo wa kweli na HAKI Havimruhusu mtu kulazimisha(kubembeleza sana) mapenzi na mahusiano.

Hivi unajua kuwa kuna madhara makubwa kimalezi kuishi na mwanamke aliyepoteza sifa ya kuwa Mke?
 
Upendo wa kweli na HAKI Havimruhusu mtu kulazimisha(kubembeleza sana) mapenzi na mahusiano.

Hivi unajua kuwa kuna madhara makubwa kimalezi kuishi na mwanamke aliyepoteza sifa ya kuwa Mke?
Ni kwel nakubali, japo inategemeana..mwanamke anaweza akapoteza upendo juu yako na asikutake tena ila hawez kuwachukia watoto wake. So atawalea tu
 
EXactly, kuna time unajikuta unaishi tena saa zingine unabembeleza kuishi na mtu ambaye unajua kabisa hakupend wala hakuhitaji but just kwakua umeshafika hatua ambayo hutaki tena kurud nyumba kuanza upya usije ukasababisha madhara zaidi.. like huo mfano hapo, umeshazaa watoto na hupend kuona watoto wanapata shida kwa kuoa mwanamke mwingine
Kabisa no one is perfect.
 
Kuna viwango vya kuvumilia, ikiwemo chuki kwa ndugu! Na kikawaida wanawake wengi hawapendi ndugu wa mume, ni asili yao, hivyo tunaishi hivyo hivyo!

Kisaikolojia, mwanamke asiyependa ndugu zako huyo hakupendi.
Vivyohivyo hivyo mwanaume asiyependa ndugu za mkewe huyo hampendi mkewe.

Kuna misconceptions nyingi katika suala la upendo, mahusiano na ndoa.
 
Ni kwel nakubali, japo inategemeana..mwanamke anaweza akapoteza upendo juu yako na asikutake tena ila hawez kuwachukia watoto wake. So atawalea tu

Atawalea vipi watoto ikiwa hakupendi wewe?
Au unazungumzia malezi Mabaya?

Hivi mke kama hakupendi na Hana hisia na wewe, mtahusiana vipi ndani ya nyumba ili watoto wenu wakue wakiona na kujifunza mambo Mema?

Au ndio Ile Baba unadharaulika na watoto wanashuhudia au mama anateswa na watoto wanashuhudia alafu utegemee watoto watakuwa na maadili kisa mnaishi pamoja?

Hizo ni akili za wapi? Au malezi ya wapi?
 
Pure intention yako nimeipima kwenye swali nililokuuliza, ungetakiwa udhihirishe hiyo dhamiri Safi kwa kunijibu lakini bado umeniwekea mtego ili upige ramli yako.

Mbinu unayoitumia wanatumia waganga wa kienyeji na matapeli. Ni mbinu rahisi Sana.

Swali lako lipo nje ya mada, linahusu mambo yangu binafsi.
Ungeuliza yanayohusu Mada ningejibu pasipo kukusumbua



Topic ngumu ni hiyo ya Kutaka taarifa zangu binafsi ambazo sijaziandika hapa.



😃😃

Sasa kama unatumia ID bandia si unaweza kuwa Mkubwa kwa kila kitu. Yawezakuwa wewe ni Bakhresa au Samia. Hapa wewe nakuchukulia kwa namna yoyote nitakayoitaka kama wewe unavyoweza jichukulia kwa namna yoyote kwa sababu upo nyuma ya barakoa
Kwanini swali linalouliza miaka uliyonayo kwenye ndoa unalikwepa kama ukoma ?
 
Do you think ,what does i

Umeongea hisia sana. Anyway, si kila mtu anachukua chukua tu kila kitu bila ku verify source au author. Sasa wewe uko tofauti na mimi na let us not judge this anymore. Unaonaje??
Let us not judge what?

Mwanzoni mwa kitabu 'IF GOD WERE A SPACE ALIEN'. cha Hamilton amesema, I know you may ask who i am, and which credentials i have, to write what i have written, i am your neighbour next door or a man across the bar!.

Alikuwa anamaanisha, muda mwingine unatakiwa kuangalia content bila kujali sana alieandika ni nani.

Kinachoonekana kwako, unajali sana mleta maudhui bila kuzingatia maudhui, and that is a logical fallacy, nyie ndio mnaomeza kila kila kitu kisa Mange kasema.

Unaweza kuniambia ni wapi na kwa mantiki ipi, unasema nimeandika kwa hisia sana?
 
Let us not judge what?

Mwanzoni mwa kitabu 'IF GOD WERE A SPACE ALIEN'. cha Hamilton amesema, I know you may ask who i am, and which credentials i have, to write what i have written, i am your neighbour next door or a man across the bar!.

Alikuwa anamaanisha, muda mwingine unatakiwa kuangalia content bila kujali sana alieandika ni nani.

Kinachoonekana kwako, unajali sana mleta maudhui bila kuzingatia maudhui, and that is a logical fallacy, nyie ndio mnaomeza kila kila kitu kisa Mange kasema.

Unaweza kuniambia ni wapi na kwa mantiki ipi, unasema nimeandika kwa hisia sana?
Am done with you man. Fanya mengine
 
UKIONA NDUGU NA WATU WANAMDHARAU MKEO UJUE WEWE MWENYEWE WANAKUDHARAU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Huwezi kuwa Mwanaume mwenye heshima kama Mkeo anadharaulika, na kudharauliwa na watu wengine. Iwe ni wazazi au ndugu zako ukiona Wanamdharau Mkeo ujue hata wewe wamekudharau, wanakuchukulia oyaoya! Kwa kifupi wewe huna lolote.

Chain inaendelea, ukiona Mkeo Wanamdharau ujue hata watoto wako wanadharaulika, wanadharauliwa.

Haiishii hapo, sasa Mkeo anadharauliwa na watu, watoto nao vivyohivyo, kinachofuata ni watoto na Mkeo kukudharau.

Mtoto hawezi kumheshimu Baba yake ikiwa Mama yake anadharauliwa na watu wengine wakati Baba yupo. Never ever!

Heshima ya Mwanaume kama Baba inajengwa na Mambo Makuu yafuatayo;
1. Upendo wa Baba kwa Familia yake.
Ili Baba aheshimike katika familia yake lazima, narudia ni lazima aipende familia yake kuliko kitu chochote kile.
Baba anayeipenda familia yake kuliko kitu chochote kile huheshimiwa na mke na watoto wake kuliko yeyote Yule.
Hii ni kusema, upendo wa Baba ni proportional na heshima atakayopewa.

Kadiri unavyoipenda familia yako ndivyo watu wengine watakavyoiheshimu familia yako yaani Mkeo na watoto.

2. HAKI.
Ili mwanaume kama Baba ajenge Legacy katika familia na ukoo atakaouanzisha, watoto na Mkewe wampende lazima ajue kutenda HAKI kwa familia yake.
Sheria, kanuni na taratibu ambazo Baba au mwanaume utaziunda ndani ya familia yako lazima zizingatie HAKI.
Haki za kiumri
Haki za kijinsia.
Haki za kimaumbile.
Haki za kiwakati.
Haki za kijumla yaani za watu wote.
Mamlaka, majukumu na wajibu ya members wa familia lazima yazingatia HAKI na yawe na mantiki.

Kama Baba lazima Ujitahidi kuwa role model katika kufuata Sheria, kanani, na taratibu mlizojiwekea ndani ya familia ili kuonyesha kuwa Sheria hizo zinatekelezeka, na wote mpo sawa ndani ya familia lakini hamlingani.

Ukiweza kutenda HAKI kwa Mkeo na watoto wako, automatically ndugu na watu wengine hawawezi kumdharau Mkeo na watoto.

3. MAENDELEO KUPITIA KUFANYA KAZI.
Kama Baba na mwanaume lazima uhakikishe Mkeo na watoto wanatija ndani ya hiyo familia.
Kupitia vipawa, karama, ujuzi na elimu wa kila Mmoja wa Memba wa familia lazima azalishe au aingize chochote ndani ya familia.

Mkeo kama sio mzalishaji ni rahisi ndugu zako na watu wengine kumdharau kwa sababu mtu yeyote asiyezalisha ni kama maiti tuu.

Kuzaa hata panya wanazaa. Kulea hata mbwa wanalea.

Iwepo mipango ya kifamilia, iundwe miradi ya kifamilia na kila Mmoja apewe mradi wa kusimamia kulingana n uwezo, ujuzi, umahiri na elimu ya Memba katika mradi husika.
Ziwepo Sheria za mapato na matumizi kwa kila memba mzalishaji katika mradi husika.
Mfano,
Kila memba kupitia mradi atakaopewa ausimamie atalazimika kuonyesha mauzo na faida kwa kila mwezi. Asilimia 75% ya faida itakayozalishwa itawekwa kwenye akaunti ya familia ya pamoja.
Asilimia 25% ya faida itakuwa kifuta jasho kwa Memba husika katika mradi huo aliousimamia na ataitumia katika mambo yake binafsi lakini ya Halali.
Yaani kama kwa mwezi faida ni laki Moja, basi Tsh 75,000/= itawekwa kwenye akaunti ya familia huku Tsh 25,000/= akichukua memba msimamizi wa mradi kwa matumizi yake binafsi.

Hata hivyo matumizi ya kila memba wa familia kwa mwezi lazima yawe yameshajulikana na bajeti yake ilishatolewa na kukabidhiwa kila memba kulingana na atakavyopendekeza. Kama mtu atapendekeza apewe Cash atapewa Cash. Na kama atataka awekewe kwenye akaunti yake binafsi vivyohivyo.

25% ya Faida haitahesabika katika sehemu ya pesa atakayopewa mtu husika.

Kwenye faida itatolewa tena 10% kwaajili ya Fungu la Kumi kwaajili ya Zaka kwa Mungu.
Hii itawekwa kwenye akaunti ya Zaka ya familia yenu kwa kila Mmoja wenu.

10% itatolewa kwa Watumishi wa Mungu mnaowaamini Sana kuwa wanatenda Kazi za Mungu. Kama hakuna watumishi hao yaani ikiwa familia itaona kuwa Watumishi hao hakuna na wengi wamekaa kibiashara basi pesa hiyo mtaipeleka kwa wahitaji kama wajane, yatima, chokoraa au wafungwa.

Mtaikusanya kwa mwaka mzima kisha mtanunua kama ni nguo sharti ziwe mpya, au sabuni, au chakula sharti kiwe kizuri na standard na cha heshima, au kitu chochote ambacho ni hitaji la msingi kwa wahitaji.

Lazima mapato yawe wazi.
Ingawaje lazima iwepo Sheria ya baadhi ya mapato yawe siri ya Baba pekee kwa ulinzi na usalama wa Familia.

Nilisema lazima HAKI itendeke kulingana na umri, jinsia, maumbile, nyakati n.k.
Ndio maana kuna baadhi ya maeneo Baba/Mume anaweza Kupata HAKI zaidi kuliko Mama/mke.
Halikadhalika yapo mazingira mke/Mama hupata HAKI zaidi kuliko Mume/Baba.

Hata yapo mazingira ambayo Watoto hupata HAKI zaidi au tuite upendeleo zaidi kuliko wazazi(Baba na Mama).
Mfano, chakula ni kidogo ndani ya nyumba, watoto inatarajiwa wapewe upendeleo zaidi kuliko wazazi.

HAKI inaenda sambamba na upendo. Lakini vyote viwili haviwezi kuwa na Tija kama hakuna AKILI na MAARIFA.

Tukirudi kwenye Mada.

Usimnenee Maneno Mabaya Mkeo mbele za watu ili kulinda heshima yako. Unapomnenea Mabaya Mkeo mbele za watu wakiwemo ndugu zako unamdharaulisha na hiyo itawapa watu kibali cha kumdharau na kukudharau wewe.

Hata Baba yako mzazi au Mama yako mzazi Hana ruhusa ya kumnenea Mabaya Mkeo. Kumtukana au kumkejeli ni dharau kwa familia yako na wewe MWENYEWE.

Ukishaanzisha familia yako lazima uelewe wewe ni serikali inayojitegemea na kujitawala. Hakuna mwenye mamlaka yoyote ya kuingilia nyumba yako.

Ni laana, ni anguko kuu kuruhusu serikali zingine ikiwemo ya wazazi wako kuingilia nyumba au serikali yako.

Kuna sheria ya mipaka, usisogeze Mpaka wa jirani yako Wala jirani yako asisogeze Mpaka wako. Kiroho unapata Laana kusogeza Mpaka wa jirani yako au kuruhusu Mpaka wako usogezwe.

Kusogeza Mpaka ni sehemu ya tafsiri ya kudharauliwa.

Yaani mtu kukuingilia kwa mambo yasiyomhusu. Kukufanyia maamuzi, kumtusi Mkeo au watoto wako. Huko ni kusogeza Mpaka wako. Kamwe usikubali.

Kuna mipaka ya aina nyingi.
Mipaka ya kifamilia, yaani kila familia inamipaka yake. Usikubali familia nyingine hata ya wazazi wako kuingilia familia yako au wewe kuingilia familia ya wazazi wako hiyo ni dharau na Laana.

Kuna mipaka ya mtu Binafsi.
Yaani wewe umemuoa mke wako lakini kuna mambo hupaswi kumuingilia hasa maamuzi yake binafsi. Mfano kama mwanamke amekengeuka, au anataka kukuacha usimlazimishe abaki kwenye maisha yako.
Unaweza mshauri lakini ushauri usizidi mara tatu.
Hivyo ndivyo watibeli tunavyofanya mambo yetu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Siyo kweli. Kuna watu huwa nasikia "jamaa mtu sana, ila mkewe ni bomu." Au pia "huyu jamaa hafai, mtaani wote hawampendi. Ila mke wake ni mtu wa watu, na watu wanakwenda nyumbani kwake kwa heshima ya mkewe."
 
Back
Top Bottom