green rajab
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 12,387
- 39,119
Kaona mchwa waharibifu wanabungua kijiji roho ime muuma taratibu hazimruhusu kuchukua hatua kaamua kutafuta spika (wanaharakati) kuvujisha taarifa nyeti sauti ipazwe.. ili wanakijiji wajue hatari iliyopo ndipo tulipo fikia hamna usiri.Hao mabwana wanazo mbinu nyingi za kulazimisha ushauri wao wa kizalendo utiliwe maanani.
Hiyo ya kupenyeza taarifa nyeti kwa vyombo vya habari, wanaharakati na wapinzani ni moja ya njia za awali tena za 'amani'.
Wakiona mambo yanaharibika sana basi watalazimika kutumia mbinu mbaya zaidi. Uwezo huo wanao.
Kwa hali ilipofika sasa ya safari za SIRI za kiongozi kuanikwa tena zikiwa kwenye hatua ya mipango inapaswa kuwa 'wake up call' kwa kiongozi husika.
Kumbuka, mamlaka ya kwenye karatasi hayana maana yoyote ikiwa wale unaowategemea ku enforce mamlaka yako hawako upande wako.