Ukiona siti iko wazi muda mrefu ulizia kabla hujaikali, yawezekana kuna sababu inakimbiwa ✍️

Ukiona siti iko wazi muda mrefu ulizia kabla hujaikali, yawezekana kuna sababu inakimbiwa ✍️

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
MPELELEZE KABLA HUJAANZA NAYE MAHUSIANO ILA ASIJUE KAMA UNAMPELELEZA ✍️


Wajuvi husema ukiona siti haikaliwi usikuikurupikie bali peleleza kwa kina kwanini inakwepwa? Ukijua sababu ndio jipime kweli utaweza kuikalia hiyo siti bila kuathirika?


Sababu zilizokimbiza wengi hata wewe zinaweza kukukimbiza kwa sababu kuna watu inafaa wajivumilie wao wenyewe tu sasa ukijifanya bingwa wa huruma au wa kuvumilia kila kitu utajikuta kwenye mateso na mwishowe kudhurika.

Sio vibaya kumpeleleza kabla hujaanza naye safari ila jitahidi kwa 100% asijue kama unampeleleza kwa sababu akijua tu mbali na kujisikia vibaya ila anaweza kujipa uhusika kwa muda ili umuone ndio yule unayemtafuta ilihali sio.

Mpeleleze umjue kwa sehemu kwa sababu huwezi kumjua kwa 100% ila umjue kwa mambo ya msingi kisha upime na wewe ulivyo utamudu?

Ukiacha mengi uyajue mbele ya safari utakuja kuyajua tayari muda umepotea na pengine utashindwa tena kuanza upya bali ukaamua kumvumilia kwa sababu tu huna pakwenda.


Tuko kwenye zama za maigizo mengi kuliko uhalisia hivyo ukijichanganya tu utakutana na MUIGIZAJI atakayepoteza muda wako.


Kuna mabadiliko yanakuja katikati ya safari haya ndio unaweza mpeleleza mtu na usiyajue ila baadaye tu ukaanza kuona tabia mpya hasa pale mtu anapopta pesa au wadhifa ndio huwa kama kichocheo cha tabia zake fiche au ulimbukeni, hapo panahitaji nguvu kubwa kumjua mtu kwenye nyakati zake tofauti anakuwaje? Kupitia maelezo yake unaweza kunfahamu kwa sehemu.


TANBIHI: Asijue kama unampeleleza, zingatia sana hilo.

Mwanasayansi Saul kalivubha.

Mitandaoni kwa majina ya fikia ndoto zako.
 
Ziache hizo siti zikae zenyewe ndo destiny yake, kuzihurumia kunaponza
 
unaeza uliza na ukadanganywa,,na unaeza chunguza na aka pretend 😁
 
🤣🤣🤣mkuu uvimbe unatutesa vijana wengi sana sio siri.
Sisi vijana wa zamani tulikuwa tunajua kuwa makalio makubwa yanaashiria ''huyu hana akili'', hivyo inapofikia suala la kuoa sifa moja tuliyokuwa tunaangalia ni ''mwanamke asiye na makalio makubwa''.
 
Back
Top Bottom