Ama nikupe mfano wa kusubirishia pm yangu:
Wewe una ndoto ya kumiliki gari aina ya Harrier, ikatokea jamaa analo anataka kuliuza, kisha akakupa ofa ulitembelee kwanza miezi miwili ili uone utendaji wake.
Ulipofika na kuanza majaribio, ukagundua kidogo linachemsha, tatizo linalorekebishika, kabla muda wa majaribio haujaisha akatokeza jamaa mwingine akakutangazia kuwa ana RAV4 New model pamoja na KRUGER anaziuza, bei ni sawa ama chini kidogo ya Harrier hiyo ya ndoto yako.
Swali hapo: je hauwezi hata kuziangalia hizo gari mbili kwa sababu tayari una gari ya ndoto yako ambayo haujailipia, au utapenda kuangalia na hizo pia ili kama moja wapo ikikupendeza zaidi ubadili maamuzi wa kununua Harrier?
Je ukibadili mawazo juu kwa ju, huyo mwenye Harrier utamueleza nini?
Kifupi mkuu hautakiwi kupewa ujaribishe kitu unachotaka kumiliki, sababu dosari za kufanya ubadili maamuzi huwa hazikosekani.