labda kama haujawa mtu mzima. ila kama umeshakua, lazima kuna watu wa karibu mnaoaminiana, hata Daudi alikuwa na Jonathan. kuna wakati usiiamini sana familia yako, inaweza kukugeuka watoto hadi wife, ukajikuta upo peke yako hata sehemu ya kwenda kutema nyongo hakuna, hapo wengi huwa wanajiua. unaweza kuwa tajiri kabisa una pesa nyingi, unakopesheka ila kuna dharura ya zaidi ya mkobo wa bank, wapo watu ambao huwa wanakuomba pesa ya dharura pengine kukomboa mzigo au tatizo lolote la kibiashara, huwa unawapa bila maswali, na wao wanakupa bila maswali, hicho ndicho nilichomaanisha. kuna mtu wangu wa karibu mmoja, mimi huwa anapiga tu simu, naomba niwekee kiasi fulani hapo kwenye akaunti yangu, huwa siulizi maswali, na kuna wakati mimi pia huwa namwambia hivyo hivyo na ndani ya nusu saa akaunti imeshasoma, ni mtu nimesoma naye tangu udogoni, familia zetu ni family friend, tunasaidiana katika shida na raha. ogopa kuishi peke yake peke yako hapa duniani. hata ungekuwa na hela namna gani, unahitaji watu wale unaowaamini na mmeaminiana.