Ukiona umefikia stage hii umekwisha

Una familia, hata kama una akiba, ila hauna marafiki kadhaa wa moyoni, mlioshibana, mnaoweza kufichiana siri na aibu, unaoweza kuwaomba pesa ya harakaharaka akakupatie bila kukuuliza maswali, umekwisha.
Ukiona umefika mahali unawaamini marafiki hadi unaweka moyoni jua umekwisha maana hujui kama nao wamekuweka moyoni kama wewe

Trust nobody mwanaume ni jeshi la mtu mmoja
 
Mkuu kuisha ni wazo tu na siyo uhalisia...unaweza ukawaza umeisha na uhalisia ukaobesha bado upo ova.
 
Ukiona umefika mahari unawaamini marafiki hadi unaweka moyoni jua umekwisha maana hujui kama nao wamekuweka moyoni kama wewe

Trust nobody mwanaume ni jeshi la mtu mmoja
labda kama haujawa mtu mzima. ila kama umeshakua, lazima kuna watu wa karibu mnaoaminiana, hata Daudi alikuwa na Jonathan. kuna wakati usiiamini sana familia yako, inaweza kukugeuka watoto hadi wife, ukajikuta upo peke yako hata sehemu ya kwenda kutema nyongo hakuna, hapo wengi huwa wanajiua. unaweza kuwa tajiri kabisa una pesa nyingi, unakopesheka ila kuna dharura ya zaidi ya mkobo wa bank, wapo watu ambao huwa wanakuomba pesa ya dharura pengine kukomboa mzigo au tatizo lolote la kibiashara, huwa unawapa bila maswali, na wao wanakupa bila maswali, hicho ndicho nilichomaanisha. kuna mtu wangu wa karibu mmoja, mimi huwa anapiga tu simu, naomba niwekee kiasi fulani hapo kwenye akaunti yangu, huwa siulizi maswali, na kuna wakati mimi pia huwa namwambia hivyo hivyo na ndani ya nusu saa akaunti imeshasoma, ni mtu nimesoma naye tangu udogoni, familia zetu ni family friend, tunasaidiana katika shida na raha. ogopa kuishi peke yake peke yako hapa duniani. hata ungekuwa na hela namna gani, unahitaji watu wale unaowaamini na mmeaminiana.
 
Una familia, hata kama una akiba, ila hauna marafiki kadhaa wa moyoni, mlioshibana, mnaoweza kufichiana siri na aibu, unaoweza kuwaomba pesa ya harakaharaka akakupatie bila kukuuliza maswali, umekwisha.
πŸ˜€ Kuwa kuna wengine ukiwaomba pesa ni mpaka wakufanyie evaluation kwanza
 
Nimeipenda hii
 
πŸ˜€ Kuwa kuna wengine ukiwaomba pesa ni mpaka wakufanyie evaluation kwanza
huyo unamdelete sio mtu wako wa karibu. yaani wapo wale watu Mungu amekuletea maishani, huwa wanakupigia wewe simu moja tu, natuma kijana hapo mpe kiasi fulani dharura, unawapa, na wewe ukihitaji, ni simu moja tu na hakuna maswali. watu mlioshibana. maishani lazima uwe na watu wa aina hiyo ambao wapo tayari kupigana pamoja na wewe. mimi mmoja wapo wa watu kama hao sio ndugu yangu na sio wa kabila langu na sio wa dhehebu langu. nilishawahi kumwokoa kwenye vibano vingi sana na yeye alishawahi kuniokoa vibano vingi sana kiasi kwamba kila mmoja huwa hayupo tayari kumpoteza mwenzie kama rafiki, na hata wake zetu wanajua, nikitaka kumpa hela nampa wazi tu mbele ya wife naye kutokana na naman alivyowahi kututoa anasema kama ni fulani, mtumie haraka hiyo pesa.
 
Kwel kabisa
 
Nakumbuka nikiwa kidato niliwahi waambia sister zangu nikifika chuo lazima nimiliki gari na nikifikisha 25 ntakuwa kwangu, waliniambia tu kila la heri tutakuja kwako mdogo wetu.

Kwa sasa tukikutana huwa wananikumbusha tunaishia kucheka sana πŸ˜‚

Maisha tunayoyataka na uhalisia ni vitu viwili tofauti. Najua kuna wadau wanawalaumu sana wazee wao kwa kushindwa kununua maeneo miaka hiyo ila muda utasema ukweli.
 
Labda kama wewe ndo haujakuwa au huna uzoefu na maisha mpaka unafikia kusema umeshibana na mtu labda wote mna utoshelevu kimaisha ndo maana ni ngumu kusikia neno family friend kwa masikini maana umaskini na urafiki havikai pamoja
 
Inategemea nyumba gani chief

Kuna nyumba moja inauzwa halafu watu kama 9 wote wanapata nyumba,,najua hujanielewa,inategemea na hiyo nyumba iko wapi
Hukunielewa Sajenti Chotta ninachomaanisha ni wangapi wameuza nyumba za urithi pesa iliyopatikana ikazalisha zaidi ya...Hiyo kitu haipo ni. 1 kati ya 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…